Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
Ijumaa iliyopita Biden alitangaza kuziuzia nchi za Ulaya (EU) gesi iliyo katika hali ya kimiminika (Liquefied natural gas, LNG) kiasi cha mita za ujazo bilioni 15 ili kupunguza utegemezi wa nchi za Ulaya kwa gesi ya Russia. Tangazo hilo limekuja ktk kipindi ambacho Putin amewaambia nchi za Ulaya na nyinginezo ambazo zimeonesha uadui kwa Russia kuwa watake wasitake watalipia manunuzi ya gesi yake ktk ruble (sarafu ya Russia)
Baada ya tangazo la Biden, wazungu waishio nchi za EU hawakufurahika kihivyo. Cha ajabu waMarekani wa 'Tandahimba' na waUkraine wa 'Kantalamba' walipiga vifijo na vigelegele na kudai kuwa nchi za EU hazitonunua tena gesi ya Russia, zimetoshelewa na Marekani ktk mahitaji ya gesi.
Sasa Marekani yasema kuwa zile mita za ujazo bilioni 15 za gesi iliyo ktk kimiminika (LNG) zitazouzwa na Marekani (kwa mwaka) kwenye nchi za EU, zitakava kiwango cha bilioni 15 za gesi ya hivyohivyo (LNG) ambayo Russia ilikuwa ikiziuzia nchi za EU, lakini sio zile mita za ujazo bilioni 150 za gesi ya Russia ambayo husafirishwa kwa mabomba makubwa kwenda EU.
Hivyo EU hawana namna ya kumkwepa Putin juu ya kutoa ruble ili wauziwe hizo mita za ujazo bilioni 150 za gesi (isiyo ktk kimiminika, isioyo LNG).
========