Zomba, acha utani, watu wapo siriaz hapa!!!!
Wasomi hawajui watendalo jamani, tuwasamehe tu!!!!!
Njaa zao hawa wapuuzi ndiyo maana wanakaa kusifia tu CCM na kuishia kuvaa maguo ya CCM Diamond Jubilee then kesho wanafukuzwa pesa haziko kwenye account za wanafunzi wao .Wasomi kila wakiwekwa kwenye TVT wanasifia JK huku wanaota kupata vyeo ?Kama kusoma ni huko basi mimi simo wacha nikae huku huku .
Na Kizitto Noya
UMOJA wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), kwa kushirikiano na taasisi mbalimbali za kijamii na za Kutetea Haki za Binadamu, umepinga ziara ya Rais George Bush wa Marekani aliyewasili jana nchini.
Umoja huo ulieleza kutoridhika kwake na ziara ya rais huyo jana katika mdahalo wao ulioandaliwa kwa kushirikiana na wanaharakati hao kwenye Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.
Akisoma tamko la pamoja, Mwenyekiti wa UDASA, Datmas Nyaoro, alisema Umoja wa Wanataaluma chuoni hapo unaamini kuwa kidemokrasia Tanzania haina jambo lolote jema la kujifunza kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa rais huyo wa Marekani.
"Hii inatokana na ukweli kwamba, chini ya utawala wa Rais Bush, haki za Wamarekani weusi zimeendelea kuvunjwa, idadi ya wafungwa kutoka katika jamii za Wamarekani weusi imeongezeka huku huduma za kijamii hasa afya na elimu zikidorora," alisema.
Kwa mujibu wa UDASA, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ufadhili kutoka nchi zinazotoa misaada yenye masharti kandamizi kama Marekani, hivyo mkataba wa dola za Marekani 608 milioni unaotarajiwa kusainiwa kati ya Rais Bush na Tanzania akiwa nchini, hauna maana yoyote zaidi ya kuendeleza ukandamizaji huo.
"Tunaamini pia katika kujitegemea na kujitawala wenyewe. Kuongezeka kwa kiwango cha misaada kutoka Marekani katika kipindi hiki ambacho uchumi wake umedhoofika na upinzani dhidi ya ubabe wake umeongezeka, kunatufanya tuamini kwamba ufadhili huu una agenda ya siri ambayo ni Africom," aliendelea kusema Nyaoro.
UDASA ilitoa wito kwa Watanzania kulinda misingi ya uhuru na utaifa, kulinda na kutetea utu, haki, usawa, amani na umoja wa Afrika badala ya kuendelea kuikumbatia Marekani na kupoteza misingi iliyojengwa tangu enzi za mababu.
Awali wakizungumza katika mdahalo huo, baadhi ya wanaharakati na wawakilishi wa taasisi za kijamii walisema kuwa ziara ya Rais Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania isipokuwa kwake binafsi na taifa lake la Marekani.
Kwa upande wake, Amiri wa Shura ya Maimam, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema ziara ya Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania zaidi ya taifa kujitengenezea maadui kwa kuunga mkono sera ya ugaidi.
Alisema sheria ya ugaidi nchini inapaswa kuangaliwa upya kwani inapingana na sheria za nchi na ndiyo inayosababisha mapigano katika mataifa mengi duniani.
Hussein Mmasi wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema Bush hana utaratibu wa kufanya ziara zenye manufaa kwa nchi wenyeji na kuwa ziara hii ni mwendelezo wa utaratibu huo wenye misingi ya kuzinyonya nchi maskini.
Profesa Azaveli Lwaitama, Mhadhiri wa UDSM, aliitaka serikali kuchagua marafiki wa kweli wanaoweza kutoa ushauri wa haki kuhusu maendeleo yake badala ya marafiki wanafiki kama taifa la Marekani.
Alisema Rais Bush amekuja nchini kwa kivuli cha misaada, lakini ukweli ni kwamba ana agenda kubwa yenye masilahi binafsi na taifa lake.
Ndani ya ukumbi kulikofanyika mdahalo huo kulikuwa na mabango kadhaa yaliyoelezea hisia za wanaharakati hao juu ya ziara ya kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani.
Baadhi ya mabango hayo yalisomeka 'Mfumo tulionao wa demokrasia wakilishi haufai, tunadai demokrasia shirikishi... Bush sitisha vita Iraq, Amani na Haki siyo vita'.
One of the index how to measure the development of the country is to listen to opinion of the academicians and professionals; if our so called highly learned professionals will reason as per the above [if is true that the way they think]; then we are not only backward, we are in a stone age!
Wasomi wametoa mawazo yao,
Wana haki na uhuru wa kusema na kutoa dukuduku lao kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kwa nini tuyahukumu mawazo yao mapema,kwa sababu tu eti Bush kasaini mkataba mkubwa wa dola million 698??ulizia wana usalama wakwambie alivyoingia Bush na nafasi yao ilikuwa wapi?FBI wanapanda hadi juu ya mapaa ya ikulu yetu eti kwa kuwa tunapewa msaada.Misaada ije mingi lakini watuache tupumue na uhuru wetu.Wasitutuhayarishe,Mgeni gani anakuja na chakula chake?Ina maana hamwamini rais wetu aliyemwalika?Surely oppression drives the wise into madness, and a bribe corrupts the heart,better is the end of a thing than its beginning, I believe the patient in spirit is better than the proud in spirit.
Tusije shahabikia msaada wa kuimarisha miundo mbinu huko kusini mwa Tanzania,kumbe kuna madini ya Uranium yamengunduliwa na wanataka urahisi ya kuyasomba kwa kuweka miundo mbinu imara.
Tunapenda wageni waje wengi nchini kwetu ila tusipate madhara ambayo tunahisi yanaweza kutugharimu huko mbeleni kama Taifa kwa ujio wao.
..................FBI wanapanda hadi juu ya mapaa ya ikulu yetu...............
EBU ANGALIENI UKOMBOZI WA BUSHI KATIKA HII ATTACHMENT,HATA KAMA ANATAKA URANIUM POA TU,KWANI SISI TUTUIFANYIA NINI ?
Tusije shahabikia msaada wa kuimarisha miundo mbinu huko kusini mwa Tanzania,kumbe kuna madini ya Uranium yamengunduliwa na wanataka urahisi ya kuyasomba kwa kuweka miundo mbinu imara.
Na Kizitto Noya
Umoja wa Wanataaluma chuoni hapo unaamini kuwa kidemokrasia Tanzania haina jambo lolote jema la kujifunza kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa rais huyo wa Marekani.
Haki za Wamarekani weusi zimeendelea kuvunjwa, idadi ya wafungwa kutoka katika jamii za Wamarekani weusi imeongezeka huku huduma za kijamii hasa afya na elimu zikidorora.
Kwa mujibu wa UDASA, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ufadhili kutoka nchi zinazotoa misaada yenye masharti kandamizi kama Marekani, hivyo mkataba wa dola za Marekani 608 milioni unaotarajiwa kusainiwa kati ya Rais Bush na Tanzania akiwa nchini, hauna maana yoyote zaidi ya kuendeleza ukandamizaji huo.
Kuongezeka kwa kiwango cha misaada kutoka Marekani katika kipindi hiki ambacho uchumi wake umedhoofika na upinzani dhidi ya ubabe wake umeongezeka, kunatufanya tuamini kwamba ufadhili huu una agenda ya siri ambayo ni Africom
Ziara ya Rais Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania isipokuwa kwake binafsi na taifa lake la Marekani.
Ziara ya Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania zaidi ya taifa kujitengenezea maadui kwa kuunga mkono sera ya ugaidi.
Alisema Rais Bush amekuja nchini kwa kivuli cha misaada, lakini ukweli ni kwamba ana agenda kubwa yenye masilahi binafsi na taifa lake.
Amani na Haki siyo vita'.
Zomba, acha utani, watu wapo siriaz hapa!!!!
Wasomi hawajui watendalo jamani, tuwasamehe tu!!!!!
Shaaaaaaaaaaaaaame!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.Vipi,kuhusu,mafisadi?.Mbona,hamkai,kuwajadili?.Acheni,ubaguzi,nyie,wanazuoni.Jadilini,kwanza,mafisadi,kwenye,madini,kama,CHENGE.