US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

Marekani? Kituo cha jeshi? Ili tupigane na nani?

Nilifikiri unapendekeza tuwaruhusu Warusi watusaidie kutumia gesi yetu kama wao walivotumia Yao wakatajirika. Au Hugo Chavezi kutusaidia kutumia mafuta yetu kutajirika. Au Irani kutusaidia kutumia Uranium yetu kutajirika. Au Botswana kutusaidia kutumia madini yetu kututajirisha

American army base? As if itakuza uchumi wetu na kutuondolea umaskini wa kipato
.
Wakuu
Hivi tayari wameshatutia mfukoni.
US wako very active hapa TZ, zile bombings za balozi zao ni false flag operation ili wajikite zaidi katika mahusiano yao na Tz.
Clinton, Bush wamefanya kazi kubwa kuiweka mfukoni TZ, sasa Obama atamalizia tu mission.
Kama kuna watu wanabariki Empire ya US izidi kujitanua Africa kwa kutegemea hawa jamaa watatuletea amani, wanajidanganya.
Soma habari za AFRICOM utaelewa.
Japan wanataka US ifunge bases zao lakini mikataba inawafunga kama Cuba inavyowalazimu kuheshimu US kutumia Guantanamo bay. Wakiingia hawatoki.
 
wajerumani wamejaa jwtz, wachina hali kadhalika. Why friendship with american?
 
Kwangu mimi huo ni uvivu wa kufikiri, kuwa hatuwezi kujipatia maendeleo bila wamarekani.

Mara nyingi humu tumekuwa tukiikosoa serikali kuwa bajeti yake ni tegemezi, sasa tunataka hata tuwe tegemezi ki ulinzi kwa 100%.

Halafu sio kweli kuwa watausaidia kiuchumi, nchi kama kenye in base za kimarekani kwa miaka mingi sana lakini mbona wote tupo kwenye kapu moja?
Nakuunga mkono mkuu.
Nataka mtoa mada atueleze base ya marekani iliyopo pakistani imewanufaisha vipi wapakistani je katika latin america hakuna kituo cha wanajeshi wa marekani na maendeleo ya nchi hiyo yakoje?Kwa kuwategemea marekani unakiri kuwa sisi hatutaweza kujenga uchumi wetu kiasi cha kutunza jeshi letu?
Je Unajua kuwa kuna uwezekano inaweza kutokea vita na sisi tukalazimishwa kuingia katika vita hizo na marekani wakati sisi hazituhusu?
Unategemea itatuendeleza wakati tayari nchi hiyo imetabiriwa kuwa uchumi wake utayumba zaidi ndani ya miaka miwili ijayo.
Sisi tuna rasilimali za kutosha kujenga uchumi wetu na hatuhitaji kutoa ardhi yetu kwa mtu,kinachotakiwa ni usimamiaji makini wa raslimali zetu..
 
Africa hatutaki kuwa 'first target' ya magaidi kwa sababu ya urafiki wa mashaka
 
Mimi nadhani Africom ni opportunity kwa Tanzania.

Italeta ajira, soko la bidhaa zetu (k.m umeme, vyakula, maji) na hata kuchochea maendeleo ya kiteknolojia. Vile vile itaipandisha Tanzania katika chati ya medani za kimataifa, kwamba sisi siyo tu watembeza bakuli, bali ni watu makini unaoweza kufanya nao mambo makubwa.

Tanzania ni kubwa na hatuwezi tukakosa kasehemu kadogo kanakohitaji maendeleo ili tukiainishe kwa ajili ya Africom.
 
Mechi ya Simba na Yanga imetishiwa na "kikundi fulani" kwamba inaweza kukatokea mlipuko wa aina yoyote na kusababisha maafa makubwa kwa majibu wa maelezo ya Kamanda wa Polisi Dar Suleiman Kova. Hii inaonesha ni jinsi gani nchi yetu inavyoanza kubadilika. Also, hatutakuwa na amani tena.

Hatujawa na Civil War, au vita vyovyote, lakini sasa hivi ni outsiders ndiyo wanakuja kuimaliza Bongo.

Nairobi pia hali inaanza kuwa mbaya kama vile Baghdad ya zamani.

Drones attack zimeshaingia EA na Africa.

Nimeanza kuangalia mpango mzima wa hii so called AFRICOM ya Marekani na mpango wao mzima ktk Africa. Najaribu kufanya Research kuangalia nini haswa dhumuni lao hawa jamaa.

Je AFRICOM imekuja kuimaliza AFRICA na TZ? Mbona tangu watie sign na nchi nyingi za Africa mambo yanaanza kubadilika (kuwa mabaya) Africa.

Hivi ni dhumuni la AFRICOM in Africa, TZ in big picture?

Hii clip kutoka you tube inajribu kuelezea kwa ufupi dhumuni lao hawa jamaa.
U.S. Militarization of Africa (clip) - YouTube
 
Back
Top Bottom