US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

Maandamano yanafanyika na wamechoma bendera ya marekani maeneo ya palm beach hapa bongo- na wanaendelea mbele walikuwa wanaimba na kuongea maneno ya kiislamu wanaelekea njia ya ali hassan mwinyi..........
 
Hivi kwanini watanzania tunashindwa kuzitumia methali tulizotunga wenyewe?

Banyani mbaya kiatu chake.....?
 
“ Sema mwanahabari “
“ Shetani anakuja saa ngapi ?”
“ unaonaje msimamo wa waisilamu ?”

Huyo ni rafiki yangu mmoja alinipigia simu jana usiku katika maongezi yetu kwanza alianza kwa maneno na maswali hayo hapo juu , mimi nilibaki nimeduwaa tu kwanini anamwita bush shetani .

Sikutilia maanani sana anavyomuita bush shetani , kwa sababu hilo neno sasa limeshakuwa la kawaida na ni propaganda tu kama zingine , nilishituka alivyoniuliza kuhusu msimamo wa waisilamu katika suala zima la ujio wa bush .

Nilimwambia maneno machache kwanza atambue Tanzania ni nchi ambayo haina dini , ni nchi huru na watu wake wako huru , mtu anaweza kusema na kuongea chochote bila kuzuiwa ili mradi asivunje sheria za sehemu husika kila sehemu inasheria zake kutegemea na eneo alipo msikitini , kanisani , jamatini kila sehemu na lake .

Kwa kuwa watu wake wako huru , hata waisilamu nao wako huru kusema kile wanachotaka , kama wamekifanyia utafiti na kuwa na uhakika nacho na kwa uhakika walifanya maandamano jana kuelezea hisia zako kuhusu sera za taifa hilo za kimataifa .

Inawezekana hata leo wakaandamana tena kwa sababu hatujui jana walikubaliana nini baada ya maandamano yao , kwahiyo tusiwapuuze tu na kuacha mambo haya yafe hivi hivi .

Kama taifa lazima lifikirie kilio cha hawa waisilamu wachache kwa sababu ni sehemu ya Tanzania , kizazi hichi kitakuwa na fikira hizo na chuki hizo dhidi ya taifa la marekani kwa miaka mingi ijayo , mfano niliona moja ya malalamiko yao ni kuhusu baadhi ya masheikh kukamatwa na miradi yao kufungwa

Je nani anapenda miradi kama ya zahanati , shule na maendeleo mengine zifungwe kwa sababu ambazo haziko wazi kama hawa waisilamu wanavyojaribu kusema ? wao wanahusisha hayo na bush .

Pamoja na yote haya waisilamu wasimlaumu bush na serikali yake kwanza wajiulize kuhusu hawa masheikh wao waliokamatwa kama wanavyosema na miradi yao iliyofungwa , waweke mbali hisia zao za kidini watuambie hawa mashekh ni kina nani na ni mali ghani za waisilamu zilizofungwa au kusimamishwa .

Wasipokuwa wazi basi tutaendelea kuamini kwamba tatizo sio bush tatizo ni la waisilamu wenyewe na mambo yao , haswa hivi vikundi vichache , na hivi ndio vikundi ambavyo vilituletea balaa uwanja wa taifa katika sakata la kwenda mecca .

Hivi vikundi lazima tuwe navyo makini sana , na tuviangalie kwa karibu wasiposikilizwa wanaweza kuanza kulipa visasi kama tunavyoona katika nchi zingine haswa mashariki ya kati
 
Sio kawaida yangu kukesha wakati wa mwisho wa wiki , lakini ijumaa ya wiki hii nimelazimika kukesha kuangalia mambo mbali mbali yanayoendelea katika mji wa dare s salaam na vitongoji vyake kabla ya ujio wa raisi wa marekani .

Katika pita pita zangu nimeona vitambaa vimeandikwa maneno kama WELCOME THE PRESIDENT OF UNITED STATES sijui kwanini wanafupisha maneno mimi nachojua ni THE PRESIDENT OF THE UNITED STATES OF AMERICA matangazo hayo yako sehemu nyingi sana na kwa kweli watoto zetu wanaoenda mashuleni au kutembelea mijini watakuwa hawana elimu sahihi wanapoona united states pekee badala ya united states of America .

Bado nashangaa ninapojaribu kufananisha ziara ya bush na ya agha khan alivyokuja mwaka jana , ukiangalia agha khan jinsi walivyomwandalia mabango mazuri mazuri yaliyonakshiwa wengine mpaka matangazo katika televisheni , inawezekana agha khan ni kiongozi wa kidini ndio maana waumini wake waliamua kumwangukia kiasi hicho

Lakini nimeona tofauti kidogo ya vibango katika barabara ya ali hassan mwinyi ndio kuna mabango lakini madogo katika taa za barabarani lakini yenye lugha ambayo sio ya kuridhisha kama UNITY TANZANIA USA , COOPERATION TANZANIA USA , muungano Tanzania Marekani , ushirikiano Tanzania Marekani , watoto wadogo wanapoona vitu vile au mtu asiyeelewa chochote akisoma maneno yale atabaki na maswali tu .

Mpaka sasa ninapoandika hivi hali ya usalama katika baadhi ya maeneo ya jiji la dare s salaam sio shwari sana , mfano kuna jengo moja refu pembezoni mwa palm beach hotel wale watu wanaoishi juu wamelazimishwa kuhama eneo lile kwa muda kutokana na ujio huu na nyumba za jirani huduma zao za mawasiliano sio ya uhakika zaidi .

Kwahiyo bush anakuja nchini na huduma zetu za msingi tunanyimwa kama simu , internet na usafiri wa uhakika , hivi janga lolote likitokea serikali na watu wake watatueleza nini ? watu wameshindwa kwenda kutoa huduma sehemu Fulani kisa bush ?

Nyumba ya mtu inaungua na moto Inawezekana ikaungua yote bila kupata huduma yoyote ile kwa sababu barabara za kupita ni ngumu , wenyewe watashindwa kuwasiliana na watoa huduma hii kisa simu zimefungwa au huduma sio ya uhakika .
 
Bush on Africa tour



US President George W Bush kicked off his six-day five-nation
tour of Africa in Benin, where he was welcomed by President Thomas
Boni Yayi at the airport in Cotonou.







Mr Bush said Africa's many conflicts were not the main focus
of his tour: he also wanted to highlight success stories.






President Bush and First Lady Laura were greeted by,
among others, a group of Beninese children.







Mr Bush's talks in Benin were expected to include the fight
against malaria and Aids. Washington has provided millions
of dollars of aid to the west African country.







President Bush was presented with the Grand Cross of the National Order
of Benin by President Boni Yayi. Mr Bush later adjusted his counterpart's sash in jest.







After his talks with Benin government leaders,
Mr Bush set off for Tanzania. He will also visit Rwanda, Ghana and Liberia.
 
President Bush arrives today
 


Tatizo kubwa linaikabili dunia hii ni unafiki. Wengi wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. Wana akili zao timamu, la uelewa lakini kawataki kuelewa.

Vikundi vilivyofanya maandamano ni sawa na presure group yoyote ingeweza kutokea manzese, kariakoo, msasani au masaki. Hakuna suala la dini wala itikadi ya chama hapa. Ila tu wengi wa walioandama walionekana wana mavazi yanayoashiria kuvaliwa na watu wa dini fulani. Sielewi kwa nini watu wasingalie ajenda ya waandamani kama ina mantiki au la. Badala yake msisitizo umekuwa kwenye dini yao.

Ni ukweli usiopingika kuwa Waislam wengi duniani wameumia kutokana na sera za Bush.

Kumkataa kuja nchini si jambo geni. Ameshawahi kukataliwa nchi kadhaa. Wanaoshabikia ujio wake wasubiri ngome ya ACM itakapotua mlangoni kwao.
 
Ulinzi ni Mkali sana uwanja ndege .Njia nyingi za Jiji la Dar zimefungwa .Zulia jekundu sasa liko tayari na itifaki imekamilika .Muda wowote ndege ya Bush Airforce one itatua kwenye ardhi ya Tanzania .

Ndugu wana Jambo niko juu kabisa kwenye jengo la uwanja huu wa JKN .Kweli ulinzi ni mkali na nimepata bahati sana kupewa ID na kuweza kuwapa habari hii.
 

Vipi kuhusu safari nyingine za ndege hapo uwanjani, zinaendelea kama kawaida au ndege zetu zimefunikwa maturubai!?
 
Vipi kuhusu safari nyingine za ndege hapo uwanjani, zinaendelea kama kawaida au ndege zetu zimefunikwa maturubai!?


Life is at a stand still .Wacha ndege hata waenda kwa miguu.Polisi ni wengi na watu ambao nadhani ni CIA, FBI nk wamezagaa na ma suti yao .Kila aliyeko eneo anatakiwa kuwa katika eneo la mpangilio.Naona akina Mama wamepangwa ndani ya nguo za kitenge nadhani ndiyo kama National Dress .

Vikosi vyetu vya Jeshi viko tayari kwa mizinga na nyimbo z Taifa .

JK ndiyo sasa anaingia uwanjani .Watu wamejaa hamasa na bendera ziko angani kama hawana akili nzuri .

Bush kesho atakuwa amana hospital .
 
Naona makachero wa Marejani wana test ngazi ya kugusa ndege ili Bush arudi na watanzania wanacheza ngoma zetu kwa kasi ya ajabu .Vikundi ni vingi kiasi na hawa jamaa wa FBI na CIA wamezagaa mno
 
Vipi zile vuguvugu za wanaharakati wanaopinga ujio wa Joji!?
 
Vipi zile vuguvugu za wanaharakati wanaopinga ujio wa Joji!?


Wale wenye vurugu zao hapa hawapo na sijaona bango hadi sasa .Wote walioko hapa ni watu wa kufurahi tu . Kuna ndege ya utangulizi imesha tuwa hapa nadani ni ndege maalumu.Naambiwa hapa kwenye sikio langu kwamba Bush atatua muda wowote kuanzia sasa yaani 5 minutes from now .
 
Naama JK sasa anatoka na anakuja kusogoa na wenzake akina Sitta na wengine akiwa anamtegemea Bush any minute from now .
 

I hope atakuwa maeneo ya mbagala kizuiani saa hizi...
 
wee........Mitomingi simu yako bado..............ina mawasiliano!!!
 
Sipati picha hapo airport palivyo najua hata wakina Taibaigana hawatii timu huko ndani...mdau endelea kutupasha wadau tuliombali na eneo la tukio
 
Naona migari yao mikubwa ile imesha kaa tayari hapa .Dege limesha tuwa na Bush is out now na Mkewe wanapunga mikono
 
JK anawatambulisha kwa viongozi 13 ambao ndiyo walio takiwa .Bush anaonyesha usanii .Anamkumbatia JK na sasa utambulisho umeisha .
 
Sasa wamepanda jukwaani wanangoja nyimbo za taifa .Bush amejikwaaa kidogo aanguke lakini nadhani kukimbia kwake kumemsaidia alidunda .Sasa wimbo wa Taifa wa Marekani .Ulinzi ni tight sana sana sana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…