US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

Wazee niko Live nimechelewa kwa sababu sa kiusalama lakini niko sasa . Bush hajacheza sindimba bado .Nyimbo zimeisha sasa na mizinga tayari .
Heshima zinatolewa tayari kwa Bush kwenda kukagua gwaride
 
Mzee Kichaka naona anakagua gwaride sasa . Mlinzi wake naona anakimbia kwa nyuma kuwahi mambo ya Kichaka mana yuko faster
 
wamerudini stejini sasa kwa salute nadhani baada ya hapa ni ngoma .Ila nimeshangaa Joji kichaka kamfuata Mdada fulani ndani kwa ndani na kukumkumbatia sijui nani yule .Kwa umbali ule sikuweza kumuona vyema ila itabidi ifanye unyoka kumjua baadaye
 
Mrindimo wa wimbo wa Taifa la Joji Kichaka uko hewani sasa baada ya kukaguwa gwaride .Ila nashanaga Joji amechangamka sana sasa sijui ni style yake au nini .
 
Namuona Salma na laura wako pamoja nao wamekakamaa sina uhakika wanawasiliana kutumia lugha gani maana Salma ni mtupu kwa kweli labda awe kachapwa shule nzito siku za hapo juzi kati .
 
Lunyungu unaona sasa vikosi hivyo vinatoka kwa ku match sijui nii kinafuatia .Lunyungu uko upande gani tuonane kama hutajali ?
 
Lunyungu na mitomingi thanks much,hope next time tutakuwa na teknoloji ya kuturushia hapa kwa live video/picture in a real time sio kwa maandishi tuu kama leo,Bush kuchangamka ni kawaida yake si unajua ni mtoto wa kihuni na ameshakamatwa mara nyingi sana(offmic) akiongea trash...alikuwa muhuni tuu tena mlevi haswa wa kupata DUI na hata kuoa alichelewa,alikuwa cheerleader vilevile pale yale
 
Hivi thread hii iliishia wapi;

BUSH kuahirisha safari ya Tanzania (serikali haitaki mjue hili)


Nani aliianzisha? katufunga kamba, kaifuta thread hata samahani hajatupa kwa kutu-mislead kwa habari za kusadikika. Hatari kubwa!
 
Wana JF
Nio tena hewani niliondoka ghafla maana movements zilisha anza hapa .Nawaombeni radhi sikuweza kusimulia zaidi ila nategemea kuwapa yatakayo jiri kuanzia usiku huu na kesho kama nitapata upenyo .
 
Namuona Salma na laura wako pamoja nao wamekakamaa sina uhakika wanawasiliana kutumia lugha gani maana Salma ni mtupu kwa kweli labda awe kachapwa shule nzito siku za hapo juzi kati .

weewew hatari nimecheka saana, mbona unatudharaulia first lady wetu
 
bush1vs8.jpg

Bush's arrival
Jaffar Mjasiri Sunday News said:
Saturday,February 16, 2008 @20:01
US President George W. Bush arrived in Dar es Salaam today evening, for the first state visit ever by a sitting American president. His huge ‘Airforce One’ touched down at 6.35 pm, with the hallmark United States of America running all the length of the plane. President Bush and First Lady Laura Bush alighted from the plane at 6.45 and waved to the huge waiting crowd that waved back as ladies responded with traditional ululation. The US President and his wife, followed by the Secretary of State Condoleeza Rice walked off the Airforce One onto a red carpet.

Thereafter, President Kikwete introduced his guest to Tanzanian officials and President Bush introduced his delegation to his host. The two presidents hugged each other moment before inspecting the guard of honour, followed by similar act by their wives. They mounted the dais for the ceremonial presidential salute, the national anthems - starting with the American one, which were played as 21 guns were fired in honour of the visiting president.

The presidents then jointly inspected the guard of honour mounted by the Tanzania People’s Defence Forces. President Bush was led to the traditional troupes arranged for him by his host and all along the visiting president felt very much at home with intermittent laughs and jokes. He shakehands and hugged some members of the dancing group who had turned up to entertain them as a token of appreciations. Both the presidents were driven from the airport on President Bush Limousine.
 
weewew hatari nimecheka saana, mbona unatudharaulia first lady wetu

Mtu wa Pwani am being honest maana huyu Mama she is design Mama wa lango la Jiji hata actions zake .never acted like FirstLady na hapo ndiyo nami wasi wasi ukaniingia kwamba wanatumia lugha gani kuwasiliana?
The woman a pure CCM fanatic na hata hajui kwamba kuna Tanzania .I have seen her in several gatherings.
 
Sasa wamepanda jukwaani wanangoja nyimbo za taifa .Bush amejikwaaa kidogo aanguke lakini nadhani kukimbia kwake kumemsaidia alidunda .Sasa wimbo wa Taifa wa Marekani .Ulinzi ni tight sana sana sana .

Kajikwaa?
Zuria lina kisiki? au chini ya zuria kuna tuta la kiraka cha lami kisicho kuwa even hapo uwanjani?
 
Kajikwaa?
Zuria lina kisiki? au chini ya zuria kuna tuta la kiraka cha lami kisicho kuwa even hapo uwanjani?

Wa Madilu yes alijikwaa na nadhani kuna kashimo ama kiraka kikubwa hawakuweza ku surface vyema .

Nilikuwa naangalia TVT sasa mtangazaji yule kweli ni kichaka kama si yai .Anasema hajawahi kuona msafara unaenda kwa kasi namna ile na anashangaa magari makubwa .Mimi nadhani sasa wawape nafasi za kwenda nje kidogo ili wawe na kujiamini badala ya kuwa watupu kiasi hiki .
 
Hapana mimi ni mwananchi na siwezi kuvaa nguo za CCM.

Wewe na Lunyungu wote mmevaa mashati ya kijani, msibishe.
Kwa vile mlichelewa wakati wa kugawiana mashati, mlipewa size kubwa XXXXL (Ya Kifisadi)kwa upenzi wa rangi ya kijani mmeyavaa hivyo hivyo. Ni kweli hapo uwanjani hamuonekani kuvaa mashati ya kijani, ila mnaonekana mmevaa kanzu za kijani.

KWa hiyo mkitaka kuonana Joyce kwa Joyce mtafute yeyote aliye vaa kanzu ya kijani.

Hii Hii hii hii kwii kwii kwii
 
Back
Top Bottom