US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

Maelfu wampokea Rais Bush baada ya kutua Tanzania
*Usafi wa ziada wafanywa maeneo atakayotembelea
*Chadema wamtumia ujumbe amrejeshe Ballali


Na Waandishi Wetu


RAIS wa Marekani, George W Bush jana aliwasili nchini Tanzania katika ziara ya kitaifa itakayochukua siku nne.


Ujio wa Bush nchini unatokana na mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete alioutoa mwaka jana akiwa nchini Marekani na una lengo la kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Marekani na mafanikio ya msaada katika kudhibiti maradhi ya ukimwi na malaria.


Bush aliwasili katika Uwanja wa Julius Nyerere saa 12:45 jioni akiambatana na mkewe, Laura; na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Condoleezza Rice na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Kikwete.


Kabla ya ndege ya Rais Bush kuwasili uwanjani, ndege aina ya Boeing 747 Air Force Two namba 29000 iliwasili na maafisa wa Marekani zaidi ya 300.


Muda mfupi baadaye, ndege ya Rais huyo, Air Force One yenye namba 28000 na jina lake iliwasili. wakati inatua magari kama 10 ya makachero wa Marekani yaliifuata kwa kasi na kugeuza kisha kuegeshwa kwa pamoja.


Kupitia mlango wa nyuma kwanza waliteremka watu zaidi ya 100 kutoka katika ndege hiyo; na baadaye ndipo Rais Bush akatokea mlango wa mbele.


Uwanja huo wa ndege ulikuwa chini ya ulinzi mkali na katika maeneo yote ambayo Bush angefikia ulinzi ulikuwa ukiongozwa na makachero kutoka Marekani, na mataifa mengine mbalimbali walipo makachero wa nchi hiyo. Pia makachero wa Tanzania, baadhi wakitoka Zanzibar walifurika katika uwanja huo.


Baada ya kulakiwa na mwenyeji wake Rais Kikwete na mkewe, Salma Kikwete, Bush alipokea salamu za heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama kisha akapigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride la majeshi ya Tanzania.


Yawezekana Rais Bush akawa kiongozi wa kwanza kupigiwa mizinga 21 na kupeperushiwa bendera baada ya saa 12 jioni kwani kwa kawaida shughuli hiyo hufanyika kabla ya muda huo.


Baada ya hapo alisalimiana na mawaziri waliokuwa wamevalia vitambulisho, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Jaji Mkuu, Augustino Ramadhan, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo na viongozi wengine wachache.


Baada ya kumaliza kusalimiana, waliondoka na msafara wake wenye magari makubwa yaliyowashtua watu waliofurika nje ya uwanja huo kushuhudia mapokezi hayo.


Msafara huo ulitanguliwa na magari ya polisi na usalama wa taifa 10, mengine yaliyotoka Marekani. Rais Bush alipanda kwenye gari maalum aina ya Cadillac mojawapo kati ya mbili zilizokuwa katika msafara huo.


Mapema, maeneo ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam yalikuwa na watu wachache, hali iliyoonyesha wazi kuwa baadhi ya wananchi wengi walikuwa na hofu kutokana na ulinzi mkali, matukio ya ugaidi na baadhi ya barabara kufungwa.


Hata hivyo, katika maeneo ambayo Rais Bush alipita kutokea uwanja wa ndege mbali na barabara kufungwa kwa ajili ya magari, watu kadhaa walijiotokeza kumlaki, lakini waliambulia kuona magari na giza lilikuwa limeanza kuingia.


Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walielezea kuwa, ni bora Bush awe anakuja mara kwa mara Tanzania kama usafi utaimarishwa kwa aina waliyoona jana.


Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini hapa ilikuwa ikisafishwa tofauti na ilivyozoeleka na kulikuwa na ulinzi mkali kufuatia eneo hilo kuwa katika ratiba ya kutembelewa na Rais Bush kesho.


Baadhi ya wafanyakazi walikuwa wakipiga deki barabara za ndani ya hospitali, wodini, pamoja na kupanda nyasi kando kando ya barabara inayoingia hospitalini hapo.

Kulikuwa na ugawaji wa mashuka mapya kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo huku pia kukiwa na wafanyakazi wapya wasio Watanzania hasa katika maeneo ambayo yanaelezwa kuwa Bush atatembezwa. Maeneo hayo ni maabara, kitengo cha dawa na eneo la masuala ya ukimwi.


“Niko hapa toka Jumatatu nimekuja kumuuguza baba yangu lakini nimeanza kuona mabadiliko makubwa sana kuanzia Jumatano, ambapo tulipewa mashuka mapya; na kumekuwa na usafi mkubwa ambao umekuwa unafanywa hapa,” alisema John Andrew.


Katika hospitali hiyo kumekuwa na pilikapilika za hapa na pale ambayo imekuwa inafanywa na wafanyakazi hao kuhakikisha kwamba mazingira yanakuwa safi.


Kulikuwa na maduka machache yaliyofunguliwa katika mitaa ya Kariakoo na pilikapilika za watu ambazo huwa kubwa siku za mapumziko kama jana hazikuonekana kuwepo.


Katika hatua nyingine, Kitengo cha Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana kilimtaka Rais Bush kuisaidia Tanzania kumrejesha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Daud Ballali waliyesema kuwa yuko Marekani kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha zilizogunduliwa katika Benki Kuu ya Tanzania aliyokuwa anaiongoza kabla ya uteuzi wake kutenguliwa.


Katika ujumbe huo, pia walimtaka Bush kusaidia uchunguzi kuhusu kampuni hewa ya kufua umeme maarufu kama Richmond Development Company LLC inayodaiwa ilikuwa na usajili nchini mwake.


Habari hii imeandikwa na Mkinga Mkinga, Editha Majura na Festo Polea
 
0987mnbhjg543a1fh0.jpg




a98mjhnbg652he7.jpg




Ndege ya Bush ilipotua Dar



iuy768jha3qf6.jpg





87uya4sb4.jpg



Rais Bush na Mkewe wakipunga mara baada ya kuwasili Dar na kuanza kushuka

kwenye ngazi za Airforce one.




we43a5cl4.jpg



Kagua gwaride basi!




b6tyr51od8.jpg


Condi alikuwepo akisalimiana na Sofia Simba.



b6jy678ag4.jpg



JK na Mgeni wake.





bush2barrival2bsa0.jpg



Ma-first lady nao walikuwapo nyuma.



54mg650348bf5.jpg




Huku ndiko walikokuwa Wamemficha Michuzi na kundi lake la wapiga picha.


PHOTOS CREDIT: MICHUZI BLOG
 
_44431920_bush_protest_416ap.jpg



But not everyone was pleased to see the US president -
these Muslim women took to the streets to protest.
Mr Bush will also visit Rwanda, Ghana and Liberia.




_44431919_bush_pres416ap.jpg


There were big smiles for the cameras as Tanzanian President
Jakaya Kikwete greeted Mr Bush amid flag-waving crowds.



_44431917_bushclothes_416ap.jpg



His image was even printed on the traditional dresses worn
by women who came to the airport for a ceremony to mark his arrival.
 
Bila shaka matunda ya ziara hii yatawanufaisha wabongo wote.

Bush touting U.S. aid in Tanzania
By BEN FELLER, Associated Press Writer
Sunday 17 Febrruary 2008

DAR ES SALAAM, Tanzania - President Bush, targeting disease and poverty in travels across the African continent, touted a soft-power agenda Sunday in Tanzania where he received a hearty, red carpet welcome by a crowd waving tiny U.S. and Tanzanian flags.

Bush opened his second day in Africa in the seacoast city of Dar es Salaam, the capital of Tanzania, which represents the kind of place Bush is visiting on his six-day trip: a stable democracy that's grateful for U.S. health and economic aid.

Bush, who arrived Saturday night to the delight of thousands ringing the roadside, met Sunday with Tanzanian President Jakaya Kikwete. Bush came with help in hand — nearly $700 million aid to help Tanzania build up its infrastructure. Bush also was visiting a hospital in the city center, discussing his anti-AIDS initiative and visit families of victims of the 1998 U.S. embassy bombing here.

Unlike in the United States, where his approval rating hovers near his record lows, Bush is treated here with reverence. Men and women wear clothing bearing his image.

Tanzania, where the economy is growing but many live in sickness and poverty, is the only country on Bush's tour to merit two days of Bush's time. Playing to audiences here and lawmakers back home, he is aiming to showcase U.S. compassion and the results it produces.

Kikwete's prominence is on the rise as the new head of the African Union, and his session with Bush is expected to cover violence and repression in troubled Kenya, Chad and Zimbabwe.

The two met in the president's historic residence, overlooking the Indian Ocean.

The shadow of Kenya, just to the north, loomed large. Both parties in that nation's disputed presidential election — one that led to bloodshed — are working on a power-sharing deal. Bush is sending Secretary of State Condoleezza Rice to Kenya on Monday to back the effort.

Tanzania, an agriculture-driven country of roughly 40 million people, is trying to broaden its ties to the U.S. across political, economic and military fronts. It is the latest country to reap benefits from the Millennium Challenge Account, one of the initiatives underpinning his trip to Africa. It provides U.S. aid to countries that govern justly, shun corruption, help their people and support economic freedoms.

The nearly $700 million compact, which Bush is signing Sunday, is the largest in the program's history. Much of it will underwrite improvements to the country's transportation.

Yet the timing is awkward, given all the emphasis on good governance.

Just this month, Kikwete dissolved his entire Cabinet over a corruption scandal involving a contract with a nonexistent firm supposedly based in the United States.

Tanzania is also one of the countries targeted by Bush's emergency AIDS relief effort, which has helped provide medicine and care to millions. More than two-thirds of all people infected with HIV live in sub-Saharan Africa. The region accounts for more than three quarters of all AIDS-related deaths in 2007.

He began his African agenda in Benin in West Africa. After his time in Tanzania, Bush plans to visit Rwanda, Ghana and Liberia.
r2560492658.jpg


ASSOCIATED PRESS
 
Hivi thread hii iliishia wapi;

BUSH kuahirisha safari ya Tanzania (serikali haitaki mjue hili)

Nani aliianzisha? katufunga kamba, kaifuta thread hata samahani hajatupa kwa kutu-mislead kwa habari za kusadikika. Hatari kubwa!

Huyu, anaona haya kujibu?
 
Kumbe Rais Bush alikuja kututembelea kwa sababu ya tunasumbuliwa na Maralia na AIDS sana.

Je Lowasa naye alikuwapo eapoti?
 
ALeqM5gMN9uZwTCYDEdXa4_UGfcF6w6E2A

189Bush_Africa.sff.standalone.prod_affiliate.71.jpg

Bush_Africa.sff.standalone.prod_affiliate.71.jpg

189Bush_Africa.sff.standalone.prod_affiliate.71.jpg


US President George W. Bush and Tanzanian President Jakaya Kikwete on Sunday signed a five-year, 698-million-dollar US aid package for the east African country.

The Millennium Challenge compact aims to reduce poverty and boost economic growth with investments in road improvements, extending electrical service to communities that do have power, and increasing access to potable water, according to the US-run Millennium Challenge Corporation.

The two leaders signed the agreement -- the largest MCC ever -- at the start of a joint press conference after talks in the Tanzanian capital Dar es Salaam, the second stop on Bush's week-long, five-country trip to Africa.

Kikwete declared the pact would improve poor infrastructure that has been an "obstacle" to the country's development and said it showed "how deep you have Tanzania in your heart."

"You will be remembered for many generations" for helping Tanzania and Africa as a whole, Kikwete told Bush.

"We act not out of guilt, but out of compassion, Mister President," Bush told his host. "We are partners in democracy."

"My hope is that such an initiatvive will be part of an effort to transform parts of this country to become more hopeful places," said the US leader.
Source: AFP

President Bush, targeting disease and poverty in travels across the African continent, touted a soft-power agenda Sunday in Tanzania where he received a hearty, red carpet welcome by a crowd waving tiny U.S. and Tanzanian flags.

Bush opened his second day in Africa in the seacoast city of Dar es Salaam, the capital of Tanzania, which represents the kind of place Bush is visiting on his six-day trip: a stable democracy that's grateful for U.S. health and economic aid.

Bush, who arrived Saturday night to the delight of thousands ringing the roadside, met Sunday with Tanzanian President Jakaya Kikwete. Bush came with help in hand - nearly $700 million aid to help Tanzania build up its infrastructure. Bush also was visiting a hospital in the city center, discussing his anti-AIDS initiative and visit families of victims of the 1998 U.S. embassy bombing here.

Unlike in the United States, where his approval rating hovers near his record lows, Bush is treated here with reverence. Men and women wear clothing bearing his image.

Tanzania, where the economy is growing but many live in sickness and poverty, is the only country on Bush's tour to merit two days of Bush's time. Playing to audiences here and lawmakers back home, he is aiming to showcase U.S. compassion and the results it produces.

Kikwete's prominence is on the rise as the new head of the African Union, and his session with Bush is expected to cover violence and repression in troubled Kenya, Chad and Zimbabwe.

The two met in the president's historic residence, overlooking the Indian Ocean.

The shadow of Kenya, just to the north, loomed large. Both parties in that nation's disputed presidential election - one that led to bloodshed - are working on a power-sharing deal. Bush is sending Secretary of State Condoleezza Rice to Kenya on Monday to back the effort.

Tanzania, an agriculture-driven country of roughly 40 million people, is trying to broaden its ties to the U.S. across political, economic and military fronts. It is the latest country to reap benefits from the Millennium Challenge Account, one of the initiatives underpinning his trip to Africa. It provides U.S. aid to countries that govern justly, shun corruption, help their people and support economic freedoms.

The nearly $700 million compact, which Bush is signing Sunday, is the largest in the program's history. Much of it will underwrite improvements to the country's transportation.

Yet the timing is awkward, given all the emphasis on good governance.

Just this month, Kikwete dissolved his entire Cabinet over a corruption scandal involving a contract with a nonexistent firm supposedly based in the United States.

Tanzania is also one of the countries targeted by Bush's emergency AIDS relief effort, which has helped provide medicine and care to millions. More than two-thirds of all people infected with HIV live in sub-Saharan Africa. The region accounts for more than three quarters of all AIDS-related deaths in 2007.

He began his African agenda in Benin in West Africa. After his time in Tanzania, Bush plans to visit Rwanda, Ghana and Liberia.
Associated Press writers Ben Feller in Cotonou, Benin, and Ali Sultan in Zanzibar, Tanzania, contributed to this report.
 
Nasikia ratiba yake kwa Africa ni kama ifuatvyo
Benin - Cotonou: arrival ceremony, meets president
Tanzania - Dar es Salaam: meets president, tours hospital; Arusha: tours hospital, textile mill and girls' school
Rwanda - Kigali: meets president, visits genocide memorial
Ghana - Accra: meets president, state dinner
Liberia - Monrovia: meets president, visits university.

Katika izo 5 days visits am told 3 days anaspend Tz?
Na Tz tumeambulia zaidi ya nusu ya siku zake Africa.
Kuna kitu apo
 
Nasikia ratiba yake kwa Africa ni kama ifuatvyo
Benin - Cotonou: arrival ceremony, meets president
Tanzania - Dar es Salaam: meets president, tours hospital; Arusha: tours hospital, textile mill and girls' school
Rwanda - Kigali: meets president, visits genocide memorial
Ghana - Accra: meets president, state dinner
Liberia - Monrovia: meets president, visits university.

Katika izo 5 days visits am told 3 days anaspend Tz?
Na Tz tumeambulia zaidi ya nusu ya siku zake Africa.
Kuna kitu apo

Mbona hizo habari za huyu BEN FELLER, Associated Press Writer
Sunday 17 Febrruary 2008
zinasema "Tanzania, where the economy is growing but many live in sickness and poverty, is the only country on Bush's tour to merit two days of Bush's time."

Na wewe na wengi wengine wanasema siku 3, mbona mnatuchanganya, sasa sijuwi nani wa kumfata.
 
Ondoeni shaka muda si mrefu tutajua nini hasa kina mweka Bush siku zote hizi Tanzania .Mimi bado nauliza gharama zitakazo kuwa zimetumika kumkaribisha .Jana Helicopta ilikuwa angani muda wote akiwa airport .Je hizi si gharama ambazo naziongelea ambazo tunataka kuzijua ?
 
Mbona hizo habari za huyu BEN FELLER, Associated Press Writer
Sunday 17 Febrruary 2008
zinasema "Tanzania, where the economy is growing but many live in sickness and poverty, is the only country on Bush's tour to merit two days of Bush's time."

Na wewe na wengi wengine wanasema siku 3, mbona mnatuchanganya, sasa sijuwi nani wa kumfata.

Mkuu,

Huo ni uandishi tu lakini wote hapo juu wako sahihi. Unaweza ukasema siku mbili kwasababu unahesabu siku kama ina masaa 24. Lakini pia inaweza kuwa siku tatu kwasababu amekaa tarehe tatu tofauti Tanzania yaani Jumamosi, Jumapili na Jumatatu.

Hivyo hivyo Benin mmoja anaweza kusema alikaa siku moja wakati mwingine akaandika alikaa masaa matatu. Wote wanaongelea kitu hicho hicho.

Ni sahihi kabisa kuandika katika siku tano za kukaa Afrika, kwa Tanzania kakaa siku tatu. Hizo ni siku nyingi sana kwa ratiba ya Bush na ni habari nzuri kwa Tanzania.

Ninaamini kuna watu wengi wamefaidika na watafaidika na hii ziara na kikubwa zaidi publicity tunayopata hatuwezi kuinunua hata kwa dola ngapi.

Kwenye hili napenda kuipongeza serikali yetu pamoja na wanancho wote kwa kufanikisha hii ziara.

Tutumie hii nafasi ya pekee kuendeleza yale yaliyo mema kwa watu wetu na kupanua sector ya utalii ili kuongeza pato la nchi pamoja na ajira.

Ni mara chache sana nchi ya Afrika inakuwa kwenye news za dunia kwa mambo ya maana, wiki hii Tanzania imeweza kuwa kwenye news kwa mambo ambayo ni positive na sio majanga tuliyoyazoea kwa Afrika.
 
Na Kizitto Noya

UMOJA wa Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), kwa kushirikiano na taasisi mbalimbali za kijamii na za Kutetea Haki za Binadamu, umepinga ziara ya Rais George Bush wa Marekani aliyewasili jana nchini.

Umoja huo ulieleza kutoridhika kwake na ziara ya rais huyo jana katika mdahalo wao ulioandaliwa kwa kushirikiana na wanaharakati hao kwenye Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.

Akisoma tamko la pamoja, Mwenyekiti wa UDASA, Datmas Nyaoro, alisema Umoja wa Wanataaluma chuoni hapo unaamini kuwa kidemokrasia Tanzania haina jambo lolote jema la kujifunza kutokana na kuwa rafiki wa karibu wa rais huyo wa Marekani.

"Hii inatokana na ukweli kwamba, chini ya utawala wa Rais Bush, haki za Wamarekani weusi zimeendelea kuvunjwa, idadi ya wafungwa kutoka katika jamii za Wamarekani weusi imeongezeka huku huduma za kijamii hasa afya na elimu zikidorora," alisema.

Kwa mujibu wa UDASA, Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ufadhili kutoka nchi zinazotoa misaada yenye masharti kandamizi kama Marekani, hivyo mkataba wa dola za Marekani 608 milioni unaotarajiwa kusainiwa kati ya Rais Bush na Tanzania akiwa nchini, hauna maana yoyote zaidi ya kuendeleza ukandamizaji huo.

"Tunaamini pia katika kujitegemea na kujitawala wenyewe. Kuongezeka kwa kiwango cha misaada kutoka Marekani katika kipindi hiki ambacho uchumi wake umedhoofika na upinzani dhidi ya ubabe wake umeongezeka, kunatufanya tuamini kwamba ufadhili huu una agenda ya siri ambayo ni Africom," aliendelea kusema Nyaoro.

UDASA ilitoa wito kwa Watanzania kulinda misingi ya uhuru na utaifa, kulinda na kutetea utu, haki, usawa, amani na umoja wa Afrika badala ya kuendelea kuikumbatia Marekani na kupoteza misingi iliyojengwa tangu enzi za mababu.

Awali wakizungumza katika mdahalo huo, baadhi ya wanaharakati na wawakilishi wa taasisi za kijamii walisema kuwa ziara ya Rais Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania isipokuwa kwake binafsi na taifa lake la Marekani.

Kwa upande wake, Amiri wa Shura ya Maimam, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema ziara ya Bush nchini haina manufaa kwa Tanzania zaidi ya taifa kujitengenezea maadui kwa kuunga mkono sera ya ugaidi.

Alisema sheria ya ugaidi nchini inapaswa kuangaliwa upya kwani inapingana na sheria za nchi na ndiyo inayosababisha mapigano katika mataifa mengi duniani.

Hussein Mmasi wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema Bush hana utaratibu wa kufanya ziara zenye manufaa kwa nchi wenyeji na kuwa ziara hii ni mwendelezo wa utaratibu huo wenye misingi ya kuzinyonya nchi maskini.

Profesa Azaveli Lwaitama, Mhadhiri wa UDSM, aliitaka serikali kuchagua marafiki wa kweli wanaoweza kutoa ushauri wa haki kuhusu maendeleo yake badala ya marafiki wanafiki kama taifa la Marekani.

Alisema Rais Bush amekuja nchini kwa kivuli cha misaada, lakini ukweli ni kwamba ana agenda kubwa yenye masilahi binafsi na taifa lake.

Ndani ya ukumbi kulikofanyika mdahalo huo kulikuwa na mabango kadhaa yaliyoelezea hisia za wanaharakati hao juu ya ziara ya kiongozi huyo wa taifa kubwa duniani.

Baadhi ya mabango hayo yalisomeka 'Mfumo tulionao wa demokrasia wakilishi haufai, tunadai demokrasia shirikishi... Bush sitisha vita Iraq, Amani na Haki siyo vita'.
 
wasomi wetu wapumbavu ndiyo maana wakamwachia nyerere avunje uhusiano na Israel, ona hasara tunayo pata sasa.
 
Sasa hawa wanatake tena! Au wanataka tutangaze kuwa Marekani ni maadui zetu! Kama ni kuipinga Marekani wameshachelewa. Hii misaada imeanza siku nyingi, walikuwa wapi siku zote. Mwacheni Bush aje atalii Bongo, huwezi jua bwana labda pesa zetu za kuitangaza nchi CNN zitarudi.
 
Hawa itakuwa ni wa Islam tu!, wasituletee udini hapa.
 
WHERE WERE YOU all these days..........mmeacha kuandama kwenye issue zinazotuandama kila kukicha..............mnasubiri Bush..............shame on you!!
 
Shaaaaaaaaaaaaaame!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.Vipi,kuhusu,mafisadi?.Mbona,hamkai,kuwajadili?.Acheni,ubaguzi,nyie,wanazuoni.Jadilini,kwanza,mafisadi,kwenye,madini,kama,CHENGE.
 
Sikutegemea watu wenye taaluma kupoteza muda wao kupinga ziara hii.They have a lot to discuss na kuyatolea mapendekezo yanayohusu taaluma zao badala ya kutuletea upuuzi huu.

Inaripotiwa elimu yetu kushuka kiwango kutokana na mambo kama haya.
 
Back
Top Bottom