US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

US Naval Bases In Africa (AFRICOM): Sababu, Pingamizi, Faida na Hasara

Hebu tembeeni na mfunguke macho maisha mnayoishi huko nyumbani si maisha watu wanavyoishi nchi nyingine! acheni kushabikia viongozi wabovu ambao wanaliletea taifa zima umasikini wa kutupwa...huku wao wakitalii na kufikia kwenye mahoteli ya gharama kubwa.

Wembe.

Ndugu yangu Wembe Mkali; hata hizo nchi nyingine unazotushauri tutembelee, walikuwa kama sisi wakati fulani miaka hiyo ya kabla ya Kristo; Nasi pia siku moja tutakuwa kama wao.
 
Ladislaus Modest,

Kasome tena hiyo Warumi and my friend in a polite manner try to find out the context why was Paul saying Obey the government, umechukua phrase out of context!

Ndugu yangu gm nilisoma/nimesoma/ninasoma vyema hayo malelekezo ya mtume Paulo kwa Warumi na nikayaelewa vyema ndio maana nimeyanukuu. Bila kusahau kuwa yameandikwa kwa Kiswahili lugha yetu ya Taifa ambayo wengi wetu tumeanza kuizungumza hiyo wakati Mungu anafungua akili zetu ili tuweze kuzungumza mara ya kwanza tangu atuumbe.
 
Ndugu yangu Wembe Mkali; hata hizo nchi nyingine unazotushauri tutembelee, walikuwa kama sisi wakati fulani miaka hiyo ya kabla ya Kristo; Nasi pia siku moja tutakuwa kama wao.


Ladslaus,

Maendeleo hayaji kwa kusubiri muda.Na muda hau-garantee maendeleo.Kwa mfano huwezi sema ikifika mwaka 2050 au 2095 au 3000 Tanzania itakuwa imeendelea!!!

Ni lazima tuwe na mipango na mikakati mahususi ya kuleta maendeleo;uongozi bora,utawala wa sheria,kupambana na kutokomeza rushwa ,kutumia vizuri rasilimali za taifa ni baadhi tu ya mambo ambayo kama tunataka tuendelee hatuna budi kuyapigania na kuyafuata hakuna miujiza katika hilo.

Haya mambo ya kusubiri eti mwana kondoo kuruka toka angani na kutua Tanzania na kutuletea maendeleo ni dhana potofu na kamwe siyo ya kuitegemea.
Ningeshauri usome historia ya baadhi za nchi zilizoendelea utaona kuwa kuna baadhi ya nchi hizo walifikia hatua ya kushika silaha na kupambana wao kwa wao ili kuweka mambo sawa baada ya kuchoshwa na viongozi wao.

Wembe.
 
Rais Kikwete ni chaguo la wananchi na amexchaguliwa kwakura nyingi ambazo haijawahi kutokea katika rais yoyote hapa Tanzania na nikiongozi aliyeletamengi kwa faida ya nchi na wananchi na kwa wale wenye uhasama choyo na wivu mtaendelea kuwa hivyo huyu rais yupo na atakuwapo hadi wisho wavipindi vyake viwili ameleta mengi kwa faida ya nchi katika kipindi kifupi kwa hiyo basi mkitaka msitake wananchi wamempakura.
 
Mkuu BAK, heshma mbele
Naomba nikufahimishe kuwa: Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete NI CHAGUO LA MUNGU (Warumi 13:1-3).

Tusitake kuingiza dini kwenye hili, Kikwete hakuchaguliwa na Mungu bali tulimchagua sisi wenyewe, huu ni msala wetu tuliojitakia wenyewe labda tu admit tu kwamba we made a mistake lakini tusimbebeshe Mungu lawama zisizomuhusu!
 
Ladslaus,

Maendeleo hayaji kwa kusubiri muda.Na muda hau-garantee maendeleo.Kwa mfano huwezi sema ikifika mwaka 2050 au 2095 au 3000 Tanzania itakuwa imeendelea!!!

Ni lazima tuwe na mipango na mikakati mahususi ya kuleta maendeleo;uongozi bora,utawala wa sheria,kupambana na kutokomeza rushwa ,kutumia vizuri rasilimali za taifa ni baadhi tu ya mambo ambayo kama tunataka tuendelee hatuna budi kuyapigania na kuyafuata hakuna miujiza katika hilo.

Haya mambo ya kusubiri eti mwana kondoo kuruka toka angani na kutua Tanzania na kutuletea maendeleo ni dhana potofu na kamwe siyo ya kuitegemea.
Ningeshauri usome historia ya baadhi za nchi zilizoendelea utaona kuwa kuna baadhi ya nchi hizo walifikia hatua ya kushika silaha na kupambana wao kwa wao ili kuweka mambo sawa baada ya kuchoshwa na viongozi wao.

Wembe.

Ndugu yangu WembeMkali, ujue kuwa tokea kale (wakati wana wa Israel wanatokea Misri) rushwa ilikuwepo; na hata sasa katika nchi unazoziona kuwa zimeendelea rushwa ipo (mfano wa yaliyotokea kwenye kura za Marekani kati ya Rais wa sasa George W. Bush na aliyekuwa mgombea wa chama cha Democrat Al Gore; mfano mwingine ni aliye waziri mkuu wa sasa wa nchi ya Italia Bw. Silvio alishawahi kushutumiwa kwa mambo ya ufisadi).

Maendeleo ni hali ya Mtu au Jumuiya fulani, au Nchi fulani kuwa/kupata kitu au jambo fulani linaloweza kuwezesha 'maisha yao' ya kuishi katika sayari hii kuongezeka hata kwa mwaka mmoja, mfano Chakula bora, Maji safi na salama, Malazi bora, Elimu; na kuweza kumpiga vita adui maradhi. Hivi vyote kwa asilimia kubwa WaTanzania tunavyo.

Kwa sasa tumshukuru Mungu kuwa Tuna Madini na hivi karibuni tutapata mafuta ambavyo siku moja kila barabara hapa nchini kwetu Tanzania itakuwa ya lami na kila nyumba itakuwa ina umeme.
 
Tusitake kuingiza dini kwenye hili, Kikwete hakuchaguliwa na Mungu bali tulimchagua sisi wenyewe, huu ni msala wetu tuliojitakia wenyewe labda tu admit tu kwamba we made a mistake lakini tusimbebeshe Mungu lawama zisizomuhusu!

Ndugu yangu Kana-Ka-Nsungu;
Usisahau kuwa sisi nasi ndio mikono ya Mungu;
Nasi pia ni miungu na wana waliye juu.
 
Ndugu yangu WembeMkali,
Maendeleo ni hali ya Mtu au Jumuiya fulani, au Nchi fulani kuwa/kupata kitu au jambo fulani linaloweza kuwezesha 'maisha yao' ya kuishi katika sayari hii kuongezeka hata kwa mwaka mmoja, mfano Chakula bora, Maji safi na salama, Malazi bora, Elimu; na kuweza kumpiga vita adui maradhi. Hivi vyote kwa asilimia kubwa WaTanzania tunavyo.

Kwa sasa tumshukuru Mungu kuwa Tuna Madini na hivi karibuni tutapata mafuta ambavyo siku moja kila barabara hapa nchini kwetu Tanzania itakuwa ya lami na kila nyumba itakuwa ina umeme.


Mchungaji Ladslaus upoo...au hizo habari hapo chini kwako ni poa tu!!!! .
Muwe na huruma kwa wananchi hawa,na tuache siasa za ushabiki kwa viongozi wabovu wanaotuletea hali mbaya namna hii huku wao wakinawili na kutalii nchi hadi nchi eti kwa sababu za kuleta maendeleo.


Tanzania: Inflation hits hard in Arusha

Arusha Times (Tanzania), by Edward Selasini - September 15, 2008.
Dar es Salaam (Tanzania) - The ravages of inflation, now about to hit double digit, are earnestly being felt by Arusha residents many of them saying they have never seen such difficult times.

Prices of all commodities have sky-rocketed and a large section of the population especially those in the low income bracket can hardly make ends meet. Inflation country-wide stands at 9.5% It all started with the sharp rise of petrol and diesel now selling at Tsh.1,750 and Tsh.2,150 respectively compared to about Tsh.1,200 for both around this time last year. The rise in fuel has led to hiked transport costs for commodities and commuters all over the region.

A Njiro resident, Mama Pili Ramadhani, found at the Central Market place by this reporter, said that she used to spend Tsh.50,000 for vegetables a week for her family but when she recently found that the money could not meet the family needs she went shopping herself only to realize that she now needed Tsh.80,000 for the same buy.

"This is ridiculous I still find it difficult to believe that vegetables have become so expensive. This is a very difficult year for Tanzanians. Every day now we wake up to brand new prices. Where are we heading to?, she asked. To others the country may be going the Zimbabwe way. But may be not yet. In Zimbabwe inflation rate is 2200000%.

A vendor at the central markeArusha Times (Tanzania), by Edward Selasini
t, John Kimaro, said commodity prices have gone up several times this year and there is no need of talking about last year. He compared current commodity prices with what they fetched a few months ago. A kilogram of sugar (prices two months ago in brackets) now sells at Tsh.1,200 (1,000/-), maize flour per kg Tsh.700 (500/-), rice Tsh.1,500 (1,200/-), wheat flour Tsh.1,000 (800/-), bread Tsh.750 (500/-) and meat Tsh.4,000 (2,800/-).

Vendors at the central market say they are selling commodities expensive because they buy expensive at source. For example, they now buy a 100kg sack of rice at Tsh.130,000 whereas a few months ago a similar sack cost Tsh.90,000. A sack of Irish potatoes Tsh.35,000 while two months ago they bought the same quantity at Tsh.28,000.

Taxis and commuter buses have doubled and many people have now resorted to walking all possible distances.

But Arushans may not yet have seen economic hardships. Economists recently warned over possible rise in inflation in the near future that would leave Tanzanians in desperate a situation of not being able to afford even the most basic commodities.

Economists argue that food prices are spiraling because the country is experiencing external shocks due to the dramatic fall in the purchasing power of the Tanzanian shilling in the last six years. One hundred thousand shilling in 2004 is estimated to be worth only about 65 thousand shillings this year.

 
Ndoa hii kati yetu na Marekani inatoka wapi?

Joseph Mihangwa Septemba 17, 2008
Raia Mwema~Sauti ya Watu

TANZANIA na Afrika kwa ujumla imeambiwa na mataifa makubwa tajiri izinduke na kupiga mwendo hima kuyasaka maendeleo. Imeagizwa na kufundishwa ifuate nyayo za Nchi Zilizoendelea kuiwezesha kuzifikia hapo zilipo; nayo imeitika wito huo.

Imeitika kwa sauti kubwa na nidhamu mpya kiasi kwamba wakati mmoja Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, alitunukiwa na nchi hizo heshima ya kuwa Mwenyekiti Mwenza wa Tume ya Utandawazi pamoja na Waziri Mkuu wa nchi tajiri ya Finland, Bibi Tarja Halonen.

Wengi wameona kwamba kuundwa kwa Tume hiyo ni moja ya mbinu za kuziingiza nchi (maskini) za Dunia ya Tatu katika mfumo wa ubepari wa kimataifa, kwa kauli mbiu ya “Ubia katika maendeleo”. Ni kiasi gani nchi hizi maskini zimenufaika kwa ubia huo? Jibu zinalo zenyewe, lakini mimi nafikiri zimeimeza ndoana na kuingizwa kwenye utumwa mpya.

Zamani, tuliambiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba “lazima tukimbie wakati wao nchi tajiri wanapotembea”, ili tuzifikie. Tofauti na sasa, Mwalimu hakuwa na mtizamo wa maendeleo kwa njia ya ubia na nchi tajiri, bali kwa njia ya umoja, ushirikiano na mshikamano wa nchi maskini zenyewe, kwa kuwa “umoja ni nguvu”.

Maskini atachangia nini katika ubia kati yake na tajiri, kama si jasho na damu yake tu, na hatimaye kifo? Siafu ni wadudu wadogo, lakini kwa umoja wao na kujiamini waweza kufanya makubwa kwa maisha yao.

Wakati Serikali ya Awamu ya Tatu iliukaribisha utandawazi kwa uwazi na ukweli” bila kuficha, awamu ya nne imeukumbatia kwa vitendo kwa “ari mpya, nguvu na kasi mpya”, na kuisababisha nchi kukosa itikadi, msimamo na dira ya maendeleo kiuchumi na kijamii. Je, haikusemwa kwamba kwa nahodha asiyejua bandari aendako hakuna upepo ulio mwafaka kwake? Hiyo ndiyo hali tulimo sasa.

Wakati huo huo, Tanzania imetokea kuwa kipenzi kikubwa cha Marekani na nchi za Magharibi kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya uhuru wake. Imekuwa nchi ya kwanza duniani kutembelewa na Rais wa Taifa kubwa la Marekani (George W. Bush) kwa siku nne mfulilizo. Naye Rais Kikwete amekuwa Rais wa kwanza Tanzania (na pengine duniani) kufanya ziara nyingi nchini Marekani, kwa wastani wa ziara tatu kwa mwaka, katika kipindi cha miaka miwili tu ya utawala wake. Kuna nini kuhusu uhusiano huu, kati ya Daudi na Goliati? Na ni nini siri ya ndoa hii?

“ Umekuja hapa kuiwakilisha nchi nzuri ya Tanzania, na pia umekuja kuuwakilisha Umoja wa Afrika. Kwa hiyo tumekuwa na majadiliano (nawe) kuhusu masuala anuai juu ya uhusiano wetu…”. Alisema Rais Bush, wakati akimkaribisha Kikwete Ikulu ya Marekani Agost1 29, mwaka huu.

Naye Rais Kikwete alijibu akisema, “Umefanya mengi kwa Afrika, mengi kwa Tanzania. Unapolinganisha, hakuna Rais wa Marekani ambaye amefanya mengi kwa Tanzania na Afrika kama ulivyofanya”.

Je, mengi kwa mazuri au kwa mabaya?. Sina hakika kwa hilo, lakini mimi na wenzangu wengi tunashawishika kuamini kwamba Marekani, chini ya Rais John Fizgerald Kennedy (1961–1963) ilifanya mengi mazuri na makubwa kwa Afrika na Tanzania kuliko Serikali ya Bush.

Ubabe, Udikteta na ubeberu wa sasa wa Bush ni mazuri gani hayo, ya kujaza katika nchi yetu makampuni ya madini ya kuhodhi yanayopora rasilimali zetu usiku na mchana, baadhi yakiwa makampuni ya familia ya Bush mwenyewe?.

Nani anafurahia mpango wa Bush wa kuweka vituo vya kijeshi nchini mwetu (AFRICOM) eti ili kupambana na “ugaidi”, na kumwezesha kuendeleza ubeberu wake ukanda wote wa bahari ya Hindi barani Afrika, toka Mogadishu (Somalia) hadi Cape Town?. Hivi leo Marekani ndio Kiranja Mkuu wa ubepari na Utamaduni wa Kimagharibi.

Changamoto ya maendeleo leo ni kuboresha maisha ya watu wetu; lakini tatizo ni kwamba mifumo yetu ya maendeleo inashinikizwa kwetu na mashirika ya Brettonwoods ambayo ni Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la kimataifa (IMF), yote yakiongozwa na kudhibitiwa na Marekani. Yanatoa kipaumbele kwa maendeleo ya miradi badala ya ubora wa maisha ya watu.

Kwa nchi kama yetu, inayothamini utu na ubinadamu, na kwa kuwajali wasiojiweza, kugawana kwa haki na wema matunda ya maendeleo ya uchumi, ni kwamba jaribio lolote la kutaka kubeza misingi hii litakuwa sawa na mpango wa kujimaliza sisi wenyewe.

Kuna hatari iliyo dhahiri juu ya kumeza kichwa kichwa mfumo wa maendeleo ya Nchi Zilizoendelea ndoano, ugwe na bildi. Ni mfumo unaotukuza kukua kwa uchumi kwa njia ya viwanda na mapinduzi ya kilimo kama njia pekee ya kupunguza umasikini.

Zaidi ya hilo, mahusiano ya kibiashara yalizipendelea nchi za Ulaya kama ilivyo leo. Kwa mfano, mapinduzi ya viwanda ya Uingereza, yasingewezekana bila kutegemea pamba rahisi kutoka India na Misri. Tuna uwezo gani kupitia njia hiyo?.

Sawa, tunataka maendeleo ya viwanda na kilimo ili tuendelee; lakini tunaambiwa, ili tujihakikishie nafasi katika mfumo wa biashara wa dunia na tuweze kuucheza mchezo kwa kuzingatia sheria za soko, eti na sisi lazima tufanye mageuzi ambayo yanazingatia masharti ya WB na IMF, ikiwa ni pamoja na kuruhusu biashara huria, kuondoa vizuizi katika soko, kupunguza ushuru wa bidhaa na ushuru wa forodha, kubinafsisha huduma za jamii, kupunguza matumizi ya Serikali na kuuza mashirika ya umma.

Mageuzi kama mageuzi, sio kitu kibaya; lakini mageuzi yanayoasisiwa na kusimamiwa na mashirika ya akina George W. Bush, hayatutakii mema. Kwa hali ilivyo sasa, na iwapo tutakubali masharti hayo, katika miaka minne ijayo idadi ya mabilionea nchini itaongezeka mara 10 ya idadi ya sasa, na idadi ya masikini, nayo itaongezeka mara 20 au zaidi, ajira itasinyaa na wengi kutupwa nje, na hayo mabilioni ya fedha za Mheshimiwa Kikwete yaliyotolewa kwa lengo la kupanua ajira hayawezi kufua dafu. Wala misaada ya George W. Bushi haitasaidia kama ilivyotokea nchini Mexico huko nyuma.

Mwaka 1994, uchumi wa Mexico ulipoharibika, nchi za Magharibi ziliingilia kati kwa haraka, kwa kutoa msaada wa Dola za Kimarekani bilion 50. Hata hivyo, nusu ya fedha hizo ziligawiwa makampuni ya Kimarekani yaliyowekeza nchini humo ili yasifilisike. Fedha hizo hazikusaidia taifa wala hazikumsaidia mwanachi wa kawaida, bali zilitumiwa na hao hao waliozitoa. Mfano wa Mexico unatuzindua kuelewa matakwa halisi ya nchi za Magharibi zinapotoa misaada kama ya sasa tuliyopewa na Bush.

Tunaambiwa, kwa kuzingatia vyema masharti ya WB na IMF, nchi yetu imeweza kufutiwa madeni lukuki na misaada kutiririka kwa wingi, tukafunguliwa milango ya kukopa zaidi. Pamoja na hayo, tujiulize; kwa nini maisha ya watu wetu hayajabadilika na uchumi unazidi kudidimia? Na haya mapenzi kati yetu na akina Bush yanatusaidiaje? Je, hayatugeuzi kuwa Mexico nyingine?.

Kwa nchi inyoendelea, marekebisho ya uchumi kwa maagizo ya WB na IMF ni neema kwa matajiri, ni maumivu kwa watu wa tabaka la kati, (wafanyakazi) na ni maangamizi kwa watu wa tabaka la chini katika jamii, tabaka linaloundwa na wakulima na wafanyabiashara wadogo.

Ni kwa sababu hii sasa nguvu za uchumi na siasa zimekamatwa na matajiri, kwa maana utajiri sasa unanunua siasa na madaraka, na siasa inanunua utajiri. Ni kwa sababu hii kwamba, mafisadi wanapeta wakati sheria dhidi ya uhalifu kama huo zipo.

Programu hizi za marekebisho ya uchumi zinaweza kuonekana nzuri kinadharia, lakini ni za wasiwasi na zisizoaminika kwa mantiki na kwa utekelezaji. Na kwa sababu tunazifuata kwa shinikizo, ni dhahiri kwamba, ufukara na mafukara wataendelea kuwa nasi daima.

Wale tuliowapa kura zetu ili watuwakilishe na kutusemea, tuwaulize watuambie bila kutafuna maneno: “watatuokoaje na balaa hili, balaa la kujitakia, mithili ya mwanakondoo ajipelekaye machinjioni?

Ni ujinga kujiweka kando na kuwa watazamaji, kwa sababu tu wakubwa wa Ulaya na Marekani, kupitia WB na IMF, wamesema “Serikali ijiondoe katika kupanga uchumi, biashara na kuachia nguvu ya soko”. Shinikizo hili halijulikani hata katika historia ya Dunia ya ubepari.

Inafahamika kwamba, mwandishi wa kitabu cha “Wealth of Nations” (Utajiri wa Mataifa), ndiye pia aliyeandika “The Theory of Moral Sentiments” (Nadharia ya uadilifu wa utashi). Adam Smith, baba wa fikra wa imani ya Ubepari, katika vitabu viwili hivi mashuhuri, anasema serikali yoyote ile ina wajibu wa kutekeleza majukumu makuu matatu yafuatayo na yasiyoepukika: Kulinda na kutetea raia wake dhidi ya mashambulizi na uvamizi kutoka kwa jamii zingine huru; kumlinda kila mwanajamii kutokana na maonevu anayoweza kufanyiwa na mwanajamii mwenzake.

Na mwisho, ni kuanzisha na kuimarisha miundombinu na asasi za umma kwa ajili ya kutoa huduma muhimu kwa manufaa ya wote, huduma ambazo vinginevyo, kwa sababu hazilengi faida kibiashara, haziwezi kuvuta au kupata wawekezaji wenye uchu wa kipato, ingawa ni muhimu kwa maisha na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Kama huu ndio mtazamo wa mabepari katika nchi zao wenyewe juu ya nafasi na jukumu la serikali katika maendeleo, kwa nini wanashinikiza na sisi tumekubali (kwa ulimbukeni?) kufuta Mashirika yetu ya utoaji huduma muhimu za jamii, tofauti na wanavyofanya wao?.

Hapa tena tunawataka wale tuliowaweka madarakani watueleze, kwa nini wamekubali kubinafsisha kila kitu, tena kwa bei ya kutupa, huduma ambazo ni muhimu kwa maisha na maendeleo ya wananchi kwa ujumla?.

Uchafuzi wa mazingira unaofanywa na wawekezaji kiholela katika nchi kama yetu, una athari kubwa kwa makundi ya jamii maskini, yanayoishi au kufanya kazi sehemu za vijijini na sehemu za mazingira tete mijini. Angalia jinsi uchafu wa kemikali za viwandani, na madawa ya mimea yanavyoweza kuathiri afya za wafu wetu. Angalia pia shughuli za migodi zinavyoharibu ardhi na mwisho wa yote tuachiwe mashimo tu ardhini, wakati wao wamekwishavuna kila kitu .

Tunachopaswa kujiuliza hapa, sio juu ya utekelezaji wa programu za uwekezaji kwa ari, nguvu na kasi ipi; au kwamba ni vipi tutajirika na lini; bali tujiulize: ni vipi mabadiliko hayo ya sera za kiuchumi, na ndoa tunayofunga na nchi tajiri, vinashabihiana na hali halisi ya nchi yetu?

Lakini zaidi ya yote, ni muhimu tuendelee kuwakumbusha wanasiasa wetu, kwamba hatuwezi kujiita watu huru kisiasa na kiuchumi, kama uchumi na utamaduni wetu unatawaliwa na kutumikia matakwa ya kigeni. Na kwa sababu hiyo, ndoa yoyote kati yetu na wageni hao ni haramu na ubatili mtupu.

0713-526972

jmihangwa@yahoo.com
 
Waungwana, when shall we get our priorities right as Africans? when shall we learn to make good out of adversity? when shall we stop complaining and get to business? in this world we live in, "no one is his/her brothers/sisters keeper". JK ameenda US mara ngapi tangia apate urais? mbona hatujawahi kuandamana? Juzi JK categorically denied any possibility of AFRICOM being stationed in Tanzania. Alitudanganya au? we ought to believe I guess! Because we havent seen the opposite! US president being in our country in four days, for smart people, its enough adverts for our limping tourism sector! Its the reality wajameni. It will depend on how we utilize this oppotunity. Tutafute mazuri ya kutusaidia katika hii ziara, mabaya tuachane nayo!

Yes, Bush has his own shortcomings and problems, but is it our priority-really?? Why cant we strategize how to make this trip beneficial to our people?, why cant our professors, advice the govt (in any form..) what kind of agendas our govt should set with GWB? That Darfurians, Somalis, Congolese people are dying, is an open secret, but why blame Bush yet people who are killing each other are Sudanese et al? tumeshawahi kuandamana ku-condemn sera za serikali ya Khartoum dhidi ya watu wake? au China inayosupply silaha kwa Sudan?

Professor kupinga hiyo ziara ni haki yake ya kikatiba, na mimi kutokubaliana naye Professor ni haki yangu ya msingi. But what Iam against ni double standards za wasomi wetu na hao wanaojifanya wanajua na kumpenda Mungu kuliko wengine. Mfano Israel inawanyanyasa Wapalestine, hakuna ubishi any peace loving person must know that and do something, but what Bashir did/doing to Southerners in Sudan for decades and decades and now in Darfur sijawahi kuona mtu akiandamana especially hapa kwetu Africa!

Sorry guys, I might have gone out of topic, lakini ukweli huu unafiki wetu (perhaps ujinga) wetu sisi Waafrika umezidi!

We move on!


africom to be stationed in Tz or somewhere in Africa should start from the AU boss. Ya kwetu yametushinda ya jirani tutayaweza? Ukoloni mamboleo en route.
 
asante mwana kijiji, kali za wajumbe imepitia sababu za prof hapo juu,huyu jamaa naweza kusema ametumia akili sana katika kuaanda vigezo vyake ,kweli shule ilitumika katika uandikaji ijaribu kupotosha jamii kwa kujizungusha tu,huyu bwana ni udini tu ndio unao msumbua basi.na pia lazima ajue pia opion sio lazima iwe jibu la swali au mada husika,especialy ktk specz,naomba atafute detail za prof eve white kama hatakwenda kinyume ,hapo opinion alizungumzia kwa kina nini maana ya opion ,



duh, imekuwa haya tena....kazi ipo.
 
wasomi wetu wapumbavu ndiyo maana wakamwachia nyerere avunje uhusiano na Israel, ona hasara tunayo pata sasa.


inawezekana Tanzania kuwa na wasomi wapumbavu? nashanga.
 
Kama ningekuwa JK ningeileta AFRICOM TAnzania. KWa sababu hawa jamaa they have millions of ways to come to Africa. Balozi zao karibu zote barani Afrika zinaelements za ujeshi na CIA. Uzuri ni kuwa wakija tutaongeza pato la taifa, kwa sababu hawatakaa bure, kuna mengi tu yatakuja na uwepo wake. Bila shaka na mabaya yake yatakuwepo


is this for real? waje ili tuongeze pato la taifa au tulipoteze hilo pato dogo tulilonalo?
 
nashangaa tu maneno makali hayo, je kuruhusu AFRICOM kuwa Tz kwa mfano, itakuwa njia mojawapo ya kuongeza pato la taifa?
.....Mama, yawezekana ikawa njia mojawapo ya kumrudisha Bush madarakani!!
 
.....Mama, yawezekana ikawa njia mojawapo ya kumrudisha Bush madarakani!!


he he heee, asante!

AFRICOM deal have to be re-thought, kama shida yetu ni kupata miundombinu reliable, hii ndio ingelikuwa fursa ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania?
 
Ujio wa Bush uliletea mamillioni ya dola za kimarekani, je AFRICOM si ndio ingeleta mabillioni ya pesa ambayo yangeleta maisha bora kwa kila Mtanzania?
 
Back
Top Bottom