The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, ameviambia vyombo vya habari kuwa; Marekani imekubali kwa makusudi kuruhusu meli za mafuta za Iran kupita katika Mlango wa Hormuz bila kuzuiliwa kijeshi kwa sasa.
Hatua hii imechukuliwa ili kudhibiti bei ya mafuta duniani isipae zaidi (baada ya kufika zaidi ya $100 kwa pipa) na kuzuia mfumuko wa bei wa kimataifa. Uamuzi huu umekuja baada ya kipindi cha mapigano makali mwezi Februari na Machi 2026 kati ya Marekani/Israel na Iran, hali iliyokuwa imehatarisha kufungwa kabisa kwa njia hiyo ya maji.
Bessent amesisitiza kuwa Marekani inajipanga kuunda muungano wa kijeshi kusindikiza meli za mataifa mengine, huku ikitegemea mataifa kama China yasaidie kulinda usalama wa njia hiyo kwa manufaa ya soko la nishati.