The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
- Thread starter
- #21
Kwa nini unasema wameua mmoja? Polisi US walishaua weusi wengi! Ni tabia ya miaka yote na nadhani ungekuwa makini, ungeelewa kwamba sababu ya maandamano siyo huyo mmoja, ni maandamano kupinga mfumo bahati mbaya ni mfumo wa rangi. Hili siyo suala la sheria, siasa, vyama, n.k.
Sifahamu kama unaelewa na kufahamu unachoongea hapa....
Ukitafuta na kuelewa maana ya "SIASA" utafungua ufahamu wako na kubadili namna ya kuchangia....
Iweje masuala ya watu kuandamana ili kupinga mfumo wa ubaguzi wa rangi isiwe ni masuala ya kisiasa?
That's pure politics...
Siasa ndiyo maisha. Siasa ndiyo inaamua mfumo wa maisha ya watu. Siasa ndiyo inaamua mifumo ya watu ya kiuchumi, kisheria, kielimu na mingine yote ya taifa lolote...
Wanachoandamania wamarekani sasa ni kupeleka ujumbe kwa watawala (wanasiasa) kuwa wanahitaji mabadiliko ya mfumo wa kisheria ktk masuala ya HAKI na USALAMA WA RAIA nk nk...
Kuuana binadamu duniani na hapa tunaongelea warekani ni jambo la kawaida na haijalishi anayekufa ni mtu mweupe (mzungu) ama mweusi....
Sana sana labda tunachoweza kukubaliana hapa ni tofauti ya "ratio". Lakini kwa vifo kama cha huyu mwafrika, hata wazungu wanakufa sana kwa wao kwa wao kuuana....
Na kusema hivi simaanishi wala kukataa kuwa hakuna ubaguzi kwa misingi ya rangi...
Upo, kama ambavyo hata katika nchi nyingi za Kiafrika upo kwa Waafrika kubaguana wao kwa wao kwa sababu mbalimbali. Yote hiyo ni siasa tu.....
Kifo cha huyo ndugu mmoja ni kwamba kimeleta msukumo tu watu kudai mabadiliko....
Kusema kinachoendelea sasa USA siyo mambo ya kisiasa, basi ni wazi kuwa wewe hujui maana ya "SIASA"....