USA sio Mungu wakikosea tuwapinge, kwenye hili nasimama na Mahakama ya Kimataifa ya ICC

USA sio Mungu wakikosea tuwapinge, kwenye hili nasimama na Mahakama ya Kimataifa ya ICC

Na kwa nini atamke baada ya Netenyau kwenda US? Hii ni kudhihirisha dunia kuwa, umoja wao hauwezi kuvunjika. Kwa dunia ya sasa si demokrasia tu, bali ni nguvu ya uchumi na kijeshi ndio inayofanya kazi.
G20 itafanyia Afrika Kusini, kutokana na migongano ya kimatamshi kati ya SA na US hivi karibuni; inasemekana hakutakuwa na mwakilishi kutoka US.​
 
Baraza lake mawaziri nani shoga? Kama anawafukuza jeshini mpaka majenerali wakubwa mashoga/wasagaji tena kwa kuwadhalilisha ndiyo aweke shoga kwenye cabinet? Prove it.
Waziri wa fedha, Scott Bessent
 
USA ishakuwa kama Banana Republic by the Strength and Loopholes alizonazo President anaweza akawa anafanya mambo ya ajabu ajabu..., sasa kama hivyo ndivyo ifike wakati kama dunia tuangalie ni wapi tunataka kwenda pamoja na wanaoona sawa huko ndio pa kwenda twende.., waioona hivyo basi na wabaki peke yao...

Na kufanya hivyo ifike wakati taasisi za kidunia ziwe na meno na sio sasa hivi ni kama puppets na appendages za kina USA wenye VETO...

Mfano United Nations Afrika ndio tuna nchi nyingi zaidi huko lakini hatuna Veto Power (What a Joke)
 
Baraza lake mawaziri nani shoga? Kama anawafukuza jeshini mpaka majenerali wakubwa mashoga/wasagaji tena kwa kuwadhalilisha ndiyo aweke shoga kwenye cabinet? Prove it.
Weka video inayomuonyesha akiwafukuza majenerali mashoga
 
Kumbe wewe sio mzima nimeamini!
Kwa akili hizi huwezi kufanikiwa.
Hivi unaona kabisa unaweza kuongea mbele ya Taifa kama Marekani?..
Wewe endelea kuwatukana CCM na PT ....huko Marekani usiende kabisa.
Ni hayo tu
Mimi ni mwanaCCM ila katika hili Mdude yuko sahihi 100%. Saa nyingine tumia akili kabla ya ku-comment
 
Kosa lake nini kutoa maoni yake dhidi ya Marekani? Kwani wewe umefanikiwa nini so far ambacho Mdude hawezi kufanikiwa? Una mawazo ya kikoloni kwa kuamini kuwa mtu akiwa na mawazo kinzani juu ya Marekani hawezi kufanikiwa maishani, kwani Marekani niMungu?
Haya toa maoni kwa Marekani..Trump anakusikiliza..atayafanyia kazi usijali
 
Mimi ni mwanaCCM ila katika hili Mdude yuko sahihi 100%. Saa nyingine tumia akili kabla ya ku-comment
Mlizoea kula vya watu ndio maana leo unamuona Mdude yupo sahihi...endeleeni kusubiri dezo...
Kama unapenda maoni ya Mdude Mbona akitoa maoni kwa Rais au PT mnamteka na kumpiga mpaka anachakaa ...dezo inaua jombaa..wewe sio Mmarekani hayakuhusu
 
Mahakama ya kimataifa siyo mahakama ni mahakama ya kutoa waranti za kuwakamata viongozi mabwege.
 
Mkuu hao USA achana nao
Uchaguzi mkuu umekaribia
Mi nadhani ungewekeza huko ni nanna gani CCM itoke madarakani
 
Mlizoea kula vya watu ndio maana leo unamuona Mdude yupo sahihi...endeleeni kusubiri dezo...
Kama unapenda maoni ya Mdude Mbona akitoa maoni kwa Rais au PT mnamteka na kumpiga mpaka anachakaa ...dezo inaua jombaa..wewe sio Mmarekani hayakuhusu
Ongelea mada iliyopo sio kuingiza hisia zako za kichoko kwenye uzi usiohusika.
 
Trump amewawekea vikwazo vya kifedha na Visa kwa maafisa wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC baada ya mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa viongozi wa juu wa Israel Israel na washirika wengine wa USA.

Mtakumbuka kwamba mwaka jana 2024 mahakama hiyo ya kimataifa ilitoa hati kukamatwa kwa viongozi wa juu wa Israel na Hamas kwa uhalifu dhidi ya binadamu maeneo ya Palestine na Israel katika vita inayoendelea eneo hilo. Kwa tafsiri hiyo ni kwamba USA walitaka hati ya kukamatwa kutoka mahakama ya kimataifa ICC iwalenge viongozi wa Hamas peke yao na Israel iachwe kwa sababu tu ni mshirika wa USA.

Huo ni uwendawazimu, hawa USA si ndio walimuwekea vikwazo mtekaji Albert Bashite A.K.A Makonda RC wa Dar es salaam kwa makosa ya utekaji na kuua watu? Sasa kwanini wao na washirika wao hawataki kuchukuliwa hatua kwa makosa hayohayo? Au wao wana kinga ya kutoshtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kibinadamu kwenye sheria za kimataifa? Ama mahakama ya ICC iliwekwa kwa ajili ya uhalifu wa kivita Africa tu? Kwamba Ulaya na USA ni watakatifu hawastaili kushtakiwa katika mahakama ya ICC?

Mtu & kiongozi yoyote mwenye akili timamu asiye mnafiki wa kutegemea fadhila za Trump atasimama na mahakama ya ICC. Uhalifu ni uhalifu tu unapaswa kupingwa hata kama uhalifu huo unafanywa na askofu au sheikh.

Kwenye hili binafsi nasimama na mahakama ya kimataifa ICC dhidi ya uhalifu wa binadamu unaofanywa na taifa lolote dunia. Vikwazo vya USA kwa mahakama ya ICC haviwezi kuwa kikwazo cha kupinga uhalifu dhidi ya binadamu. Lakini pia USA sio mbinguni wala peponi kwamba ni lazima nifuate baadhi ya misingi hata kama ni ya kijinga ili nifike. USA imepoteza uhalali wa kupinga uhalifu kwa kuwatetea viongozi wa juu wa Israel waliofanya uhalifu wa kibinadamu na Hamas kule Israel na Palestine.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.

Unapambana na Israel unapambana na Mungu mkuu soma maandikooooo

Hiooo imeishaa
 
Yani hapo wala sio AMERICA, NI ISRAEL ndio imesema

Kwa kifupi Israel inaiednesha USA kwa remote, US presidents watasema chochote wanachoamriwa na Israel.

Kwa kifupi USA is colonised by Israel
 
Tunawagonjwa wanaokula shudu milioni 10+ halafu tumnunie bosi?
Condom pia tunategemea msaada
 
Back
Top Bottom