Hii thread ilinipotea sikuiona tena mpaka leo Nyamayao aliponikumbusha na kuitafuta...Mengi (kama sio yote) yameshaongelewa humu hasa na RR na Ikunda. Literature kuhusu usafi wa nyeti za mwanamke kusema kweli iko diverse, na kwa kiasi fulani imeathiriwa sana na bishara ya products mbali mbali za kutunza usafi wa kiungo hicho kitamu. Mimi naomba nistick kwenye facts tu zilizothibitishwa kisayansi:
- Uke, kutokana na umbile lake (anatomy) umejitengenezea kama mazingira yake separate ambayo hayataki kuchokozwa ili uke ubaki kwenye hali yake ile ile. Mazingira hayo ni:-
1. Ngozi ya hali ya maji maji (mucosal cells zake zinaproduce umaji maji na kuwa wet)
2. Asidi (uke uko acidic pH 3.8 - 4.5)
3. Vijidudu wakazi (normal flora mabao mainly ni fungus candida albicans na aina kadhaa za bacteria)
4. Mabadiliko ya kihormone (hormones za kike/uzazi)
- Uke naturally hutunza balance hii kwa kuwa na uwezo wa kujisafisha wenyewe (self cleansing) ili kupunguza uhitaji wa mwanamke kujisafi mara kwa mara na/au kujichokonoa na hivyo kuongeza hatari ya kuharibu balance.
- Balance ya vitu hivyo vitatu vya kwanza ndio vinadetermine afya ya uke katika kujilinda na magonjwa mbali mbali....na kuwa katika hali nzuri bila mwasho wala kunuka. Balance hiyo huzuia vijidudu wakazi (normal flora) wasizaliane kupita kiasi na kusababisha madhara kwa uke (kuwasha na/au kunuka), na balance hiyo pia huzuia vijidudu wengine toka nje mfano kwenye kinyesi au mkojo wasishambulie uke kirahisi. Na hiyo balance huwa haiathiriwi na hicho kitu cha nne (hormonal changes) hata unapokuwa kwenye hedhi (MP). Kwa kifupi balance hiyo haiathiriwi na mwili wa mwanamke unavyofanya kazi kikawaida.
- Balance hiyo mara nyingi (kama sio mara zote) uathiriwa na vitu toka nje ya hayo mazingira ya uke..mfano tendo la ndoa, vidole (kupima oil), wipes, tampoons, na mara nyingi sana vitu vinavyotumika wakati wa kuosha hasa kuosha kwa kuingiza vidole (douching) ukitumia products mbali mbali wanawake wanazotumia kuosha huko (sabuni medicated or not, maji yenye antiseptics mfano dettol au chloride nyingi, na products nyingine). Haya matendo uingilia ile balance, na mara nyingi uingilia vaginal pH kwa kupunguza uacid wake kuelekea neutral au alkaline.
- Balance ya uke ikishaharibiwa/ikiingiliwa...basi hao vijidudu wakazi (normal flora) ambao ni bacteria na fungus huzaliana kupita kiasi, na kwa kuwa ngozi ya uke ni laini na maji maji basi inakuwa rahisi kuishambilia na kusababisha mwasho na/au kunuka. Kuzaliana kwao na kukua kwa kasi pamoja na kushambulia ngozi laini ya uke kunafanya iwe vigumu kurudisha ile balance tena mpaka dawa za hospitali zitrumika kuua na kuzuia ukuaji wa wa normaql flora ili kuruhusu balance ijirudie tena....sasa hapa ndio trick na ugumu mzima ulipo.
Wanawake psychologically wakipatwa na ugonjwa wowote wa ukeni hujiona wachafu au ugonjwa umechangiwa na kuwa wachafu...na hivyo kitu cha kwanza ni kuongeza usafu wa huko chini...lakini ndio wanajikuta wanafanya mambo yanakuwa worse kwani balance ndio inaharibiwa zaidi na tatizo kuwa baya zaidi.
Literature kuhusu kusafisha uke zipo nyingi na tofauti...na zinaweza kuwa kweli kwa mazingira zilipofanyika. Kuna tafiti zinasema wanawake wasioshe uke kabisa, hizi zimebase kwenye fact kuwa uke ni self-cleansing na self-maintaning the vaginal balance.
Studies zimefanyika kuonyesha kuwa walikuwa hawaoshi walikuwa na episodes chache za magonjwa ya ukeni hasa fungus (candidiasis) kuliko waliokuwa wanaosha, na episodes za magonjwa zilikuwa fupi kwako ukilinganisha na waoshaji.
Kuna studies nyingine zimeonyesha unahitaji kuoshsa mara chache..mara moja, mbili,...kwa siku etc...lakini outcome sio tofauti sana na wasioosha. Kwa hiyo inategemea daktari ushori anaokupa unabase kwenye studies zipi.
Ndio maana kimtazamo nakubalina na RR na Ikunda kwa na ratiba ya kuosha uke (yaani kuingiza kidole ukeni 'douching' hata kwa maji tu bila sabuni au product nyingine yeyote) mara chache iwezekanavyo. Kuosha kijujuu (bila kuingiza vidole/douching) kama ukikojoa unaweza fanya hivyo mara kadhaa mfano kila unapokojoa, hakuna madhara ili mradi maji unayotumiaq ni safi. Na epuka kabisa kutumia sabuni, maji yenye dettol au products nyingine kuosha uke na maji yake kuingia ukeni kwa kidole.
Hakikisha unatumia mafuta/lubricant salama wakati wa tendo (nazungumzia njia ya kawaida...wala si tig* sababu tu nimetaja lubricants)...epuka lubricants zenye asili ya mafuta (petroleum jelly) kutumika ukeni, na condom zisizothibitishwa kiafya au zilizoexpire. Epuka anal-to-vaginal shift kama unatumia matundu yote. Squitting haina tatizo lolote kwani mkojo kwa kawaida ni sterile, yaani hauna vijidudu unless ukiwa na UTI.
Ukiwa na fungus wa ukeni (mara nyingi ni candisiasis ambao ni normal flora waliozaliana kupita kiasi...fungus wa ukeni mara nyingi si wakutokea nje kwenye maji machafu) basi ujue kuwa balance ya vaginal environment imeharinika, basi fanya unayoshauriwa kitabibu kutunda balance hiyo wakati wa matibabu.