Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Choo ni moja kati ya sehemu muhimu katika makazi yoyote ya watu iwe nyumbani, Ofisini, sehemu ya biashara na maeneo mengine. Choo huweza kutumika kibinafsi (privately) au kijumuiya (Publicly) kutegemeana na eneo husika.
Choo kinapotumika kibinafsi shida na changamoto inakuwa sio kubwa ukilinganisha na kinapotumika kijumuiya. Katika mazingira yetu zipo sababu nyingi zinazotufanya kwa namna fulani kutumia vyoo vyetu kijumuiya. Mfano, Chuo, shule, Ofisi, soko, nyumba ya kupanga n.k.
Kumekuwa na tabia hatarishi za matumizi ya vyoo vya jumuiya kiasi cha kuhatarisha afya na kuleta kero ya matumizi kwa wengine.
Kwahiyo ili kulinda afya yako na ya wengine unapotumia choo unashauriwa kufanya mambo yafuatayo:
1. Kuhakikisha uwapo wa maji ambayo yatayokuwezesha kutumia kwa kujisafisha baada ya haja na kunawa mikono baada ya kutoka. Fanya jitihada za kutafuta maji kabla ya kutekeleza haja yako.
2. Mwaga maji mengi baada ya kutekeleza haja ili kuifanya haja yako (mikojo au Kinyesi) kwenda na kutoonekana kabisa na watumiaji watakaofuata.
3. Kukausha maji maji kwenye sinki la choo na sehemu nyingine kwa kutumia tissue au kifaa cha usafi Ili wengine wakija wasikute majimaji.
4. Nawa mikono yako kwa sabuni baada ya kumaliza haja yako ili kutoondoka na uchafu.
Mengineyo kuhusu usafi wa choo:
- Ili kutunza mazingira na usafi wa mazingira ya choo inashauriwa kwa vyoo vya nyumbani hasa Wapangaji kuwepo na kandambili au kifaa Cha kuvaa mguuni maalumu mlangoni Ili kuepusha watu kuingiza uchafu kutoka nje.
Kwa vyoo vya public kama stendi na maeneo ya kazi na watu wengi kunapaswa kuwepo na mtu maalumu wa kusimamia kuhakikisha usafi mara kwa mara.
Pia soma: Choo ni Zaidi ya Mahali pa Kuhifadhi Taka
👌 Asikwambie mtu nyumba ni choo