Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine



Gharama za uendeshaji ikiwemo airport charges na wafanyakazi lukuki ni sababisho. Ni shida sana!!!!
 
Huu ni uchochezi inataka utukoseshe kura, hii mada ungeleta baada ya uchaguzi, hata hivyo wananchi walishirikishwa kupanga na sasa tunaleta uchaguzi ili iwe rahisi kurekebisha palipozidishwa, kajiandikishe ufaidi matunda ya ndege zako.
 
Ahsante.
Ila ungekuwa unaweka na distance between the cities compared to Tanzania
 
Nchi ya wahuni hii ndugu....
Kuna aircraft engineer kipindi cha Magu alisema kuirusha ile airbus kubwa Dar Mwanza ni hasara...wakampoteza kwa muda....alipopata ufahamu akaomba kustaafu
 
Mkuu umeuliza swali zuli Sana
 
Kwani ni lini adui ujinga alifutwa Tanzania?
 
Mindset za watawala wanaona usafiri wa ndege ni anasa, hivyo hizo anasa wanatakiwa kuzifaidi wachache. Hii pia ipo kwenye umiliki wa magari hapa nchini, inakuaje TRA hujatengeneza gari lakini unachukua kodi sawa na bei ya kununulia hilo gari!!. Nchi hii watu tunafanywa maskini kwa makusudi kabisa. Watawala wameona sisi kuendelea kuwa maskini ndio mtaji wao kuendelea kutawala na kujilimbikizia mali ili kila siku tuwaabudu wao kama miungu watu.
 
Naona hujazungumzia distance, labda ni distance issue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…