Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tatizo ni Serikali kutaka Kodi kubwa sana kuliko uhalisiaUsafiri wa anga nchini Tanzania ni usafiri ghali na wa gharama ya juu hadi kufikirisha ukilinganisha na mataifa mengine yakihusisha na safari kutoka bara moja hadi bara jingine.
Usafiri wa anga chini ya Air Tanzania kwa kiasi kikubwa ukisaidiana na Precision Air unaonekana kama umewalenga wanasiasa na wafanyabishara wakubwa.
Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Caracas, Venezuela hadi Madrid, Uhispania ni takriban $290 sawa na TZS 864,311 - hiyo ni nchi hadi nchi kwenye mabara mawili tofauti.
Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Bukoba, Tanzania hadi Dar es Salaam, Tanzania ni takriban TZS 631,000 sawa na €212 - hiyo ni mji hadi mji ndani ya nchi.
Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Fort Lauderdale, USA hadi Cartagena au Barranquilla, Colombia ni takriban $69 sawa na TZS 189,000 - hiyo ni nchi hadi nchi.
Safari ya ndege ya unganisho kutoka Mbeya, Tanzania hadi Mwanza, Tanzania ni takriban 1,100,000 sawa na $403 - hiyo ni jiji hadi jiji ndani ya nchi.
Hii ni mifano midogo sana maana kuna safari za kutoka Seoul, Korea Kusini hadi Barcelona kwa TZS 1,023,000.
Swali langu ni kwanini ATCL na washirika wake ndani ya nchi wana gharama kubwa katika usafirishaji! Je wanatumia teknolojia na mifumo tofauti na ghali ukilinganisha na mataifa mengine?
Ni sababu zipi za msingi zinazofanya flights za ndani ya nchi kuwa ghali maradufu kiuhalisia na hata ukilinganisha na mataifa mengine?
Ni maelekezo kutoka juu kuendelea kuwafinya watanzania wazidi kuishi kijamaa?
JamiiForums naomba msaada wa kuwatafuta ATCL, Mamlaka ya Anga na Wizara ya Uchukuzi watupatie ufafanuzi na statistics zinazohalalisha gharama za usafiri wa anga.
Nadhani hoja zako hazina ukweli..Mbona KQ nauli yake ni kubwa sana?Hao ATCL wakati wanafufuliwa na uncle hayati JPM, waliopaswa kumshauri waliogopa na kuhofia kusema iliyo kweli, shirika lilifuliwa bila mpango mkakati, zikanunuliwa ndege ambazo kwa wakati mfupi na wa kati hazikuwa na tija, mapanga shaa q400 ni ndege nzuri sana kwa regional air transport, tozo zilizowekwa kwenye kila siti zingepunguzwa na frequency ya flights ikaongezwa ndege zishinde angani na sio kwenye hangars, Fastjet walimudu kushikilia soko sababu business model yao ilikuwa 'low cost airline ' flights zisizotumia muda mrefu mara nyingi kwa siku , ndio maana waliweza kuwa na flights 4 mathalani kwa DAR MZA.
Halafu inaonekana na inawezekana kuna figisu na favoritism huko kwenye hiyo sector ndio maana washindani hamna.
We mama unaniaminisha kwamba ukubwa ubwege.Unafuu wa usafiri wa ndege haupimwi kwa bei ya nauli pekee.
Mkuu, hapa una maanisha milioni 5 kwa mwezi ni mshahara mdogo hasa? Kiasi cha kutolea mfano kwamba hawezi kumudu safari kwa ndege?Mtu anayelipwa 5 million a month au mfanya biashara inabidi ajitafakari kusafiri sehemu moja kwa 1 million na kurudi 1 million.
Swali litalofuata litakuwa, kwa nini nchi yetu kuna ndege chache?Jibu rahisi tu nchi zenye ndege nyingi nauli huwa chini sababu ya ushindani mkubwa
Nchi alizotolea mfano zina ndege nyingi mno za abiria
Kuwa na pesa haimfanyi mtu kupata huduma yenye thamani ya 150k kwa 400k, kuwa na pesa haimfanyi mtu anunue kilo ya Sukari yenye thamani ya 3500 kwa 10,000.
Uchache wa abiria inaonekana kutokana na gharama zinazowekwa. Naamini leo hili gharama zikipunguzwa kuna miji alitakiwa kuwa na flight kila siku na nyingine flight mbili hadi tatu.
Faiza una Nini lakin?😂😂Ni wapi ulisoma kuwa sababu za kuanzisha upya Air Tanzania zilikuwa ni kushusha bei za nauli ya ndege?