Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Hao ATCL wakati wanafufuliwa na uncle hayati JPM, waliopaswa kumshauri waliogopa na kuhofia kusema iliyo kweli, shirika lilifuliwa bila mpango mkakati, zikanunuliwa ndege ambazo kwa wakati mfupi na wa kati hazikuwa na tija, mapanga shaa q400 ni ndege nzuri sana kwa regional air transport, tozo zilizowekwa kwenye kila siti zingepunguzwa na frequency ya flights ikaongezwa ndege zishinde angani na sio kwenye hangars, Fastjet walimudu kushikilia soko sababu business model yao ilikuwa 'low cost airline ' flights zisizotumia muda mrefu mara nyingi kwa siku , ndio maana waliweza kuwa na flights 4 mathalani kwa DAR MZA.
Halafu inaonekana na inawezekana kuna figisu na favoritism huko kwenye hiyo sector ndio maana washindani hamna.
 
tatizo ni Serikali kutaka Kodi kubwa sana kuliko uhalisia
 
Nadhani hoja zako hazina ukweli..Mbona KQ nauli yake ni kubwa sana?
 
Mtu anayelipwa 5 million a month au mfanya biashara inabidi ajitafakari kusafiri sehemu moja kwa 1 million na kurudi 1 million.
Mkuu, hapa una maanisha milioni 5 kwa mwezi ni mshahara mdogo hasa? Kiasi cha kutolea mfano kwamba hawezi kumudu safari kwa ndege?

Kijijini kwetu, tukijua mtu analipwa hivyo, sisi wote tunakuwa ndugu zake wa karibu sana.
 
Mimi niko shinyanga, naomba uniambie na mashirika mengine ya ndenge katika bara la Afrika, Hizo ulizotolea mfano ni nchi kubwa mno kiuchumi, usije ukakuta serikali zao zinatoa posho kidongo ili kupunguza garama kwa wanainchi wake,
 

Ushaambiwa watanzania wengi Wanatatizo la Afya ya Àkili.
Kîla kitu tafuta Pesa.

Hao wenye Pesa wènyewe hawawezi kununua kitu ambacho thamani yake NI Laki Mbili alafu anunue Laki tano hayo ni matumizi mabovu ya Pesa na Àkili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…