Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Ukiwa DRC Congo ni rahisi kupanda ndege kuliko ukiwa Tanzania , hata ukiangalia Kodi za magari tunayoagiza Tanzania iko juu kuliko nchi nyingi ,
Zinabeba madini ya kongo abiria ni subsidiary tu

Kenya Airways wenyewe maafisa wao walishadakwa mizigo wanajaza madini yaliyoibiwa kongo wewe abiria unakaa kwenye kiti kama human shield tu

Ndege nyingi safirisha abiria kongo wezi wa madini abiria unapewa lift tu ndio maana waweza weka kanauli kadogo kuzuga .Pesa ya mzigo wa madini wanaolipa wezi wa madini yaweza kuwa sawa na safari 10 za abiria za ndege kwenda na kurudi kongo

Mambo ya ndege yana mengi usiangalie nauli tu ukaona ndogo basi unarukaruka na kudhalilisha ATCL yako wasioiba cha mtu
 
Ni kwamba mnapenda kubisha, au?

Hizi ni nauli za Dar es Salaam to Bukoba:

Hii ya kwanza ni ya Alhamisi, October 17th; inauza TZS 497,600.00 kama ukiinunua sasa hivi kwa kuchelewa.


Hii ya pili ni ya November 12th; inauza TZS 372,300.00 kama ukiinunua leo.


Hizo laki sita za kwenda Bukoba ziko wapi? Hebu tuweni fair bhana.

Source: Air Tanzania
 
Acha porojo,
 
Kuna wakati mwingine una lazimika kusafiri kwa dharula. Utakataje mapema?
Duniani kote ukipata dharula mara nyingi unakuta demand ipo juu kwa kuwa tickets nyingi zinakiwa zimeshanunuliwa. Bei itakuwa juu.

Lakini kama ni low season, uwezekano wa ticket kuwa bei chini ni mkubwa hata kama utakata na kusafiri papo kwa papo. Low season demand inakuwa chini.

Hii ni kwa airlines zote duniani, siyo Tanzania pekee.

Tuweni fair.
 
Kuna wakati lilikuwepo shirika la community airlines hapa nchini, lilifanya safari zake mji hadi mji, walipata wateja wengi sana tokana na bei zao kuwa rafiki, hata wale ambao hawakuwahi kufikiria kupanda ndege ilikuwa ni wakati wao kupanda ili kuweka historia kwenye maisha yao...nadhani walipigwa hujuma wakakimbia...wenye kumbukumbu sahihi wanaweza kuja kulielezea vzr shirika hili.
 
Logically; na ATC wakiweka bei ndogo watahujumiwa wakimbie.
 
Caracas to Madrid
4347 miles / 6995.82 km / 3777.44 nautical miles.

Bukoba to Dar es Salaam
638 miles / 1027 kilometers / 555 nautical miles.

So the other fact inayobaki ni mafuta na services ndiyo ina-determine gharama?!
Swali lingine la kujiuliza kwanini hao wenye nauli za chini wafanyakazi wao/pilot walipwe vizuri kuliko wa kwetu, bilashaka kuna tatizo mahali.
 
Caracas to Madrid
4347 miles / 6995.82 km / 3777.44 nautical miles.

Bukoba to Dar es Salaam
638 miles / 1027 kilometers / 555 nautical miles.

So the other fact inayobaki ni mafuta na services ndiyo ina-determine gharama?!
Mkuu naona umejipanga kutetea uzi wako 100% i support ila bahati mbaya tumezaliwa katika watu waoga sanaa wa tanzania, hivi "nautical miles' ndo unamanisha nini?
 
Ndege ilikuwa mbovu Antony Diallo kiongozi mkubwa wa CCM , serikalin kama waziri ,mbunge na mfanyabiashara mkubwa wa Mwanza enzi hizo alinunua toka air Tanzania ikiwa grounded na ATC waliona haina uwezo hata kuruka kwenda nje kutengenezwa akaigharamia iruke akaanzishisha Community Airlines kwa nzege moja tu hiyo na ilichapa kazi lakini kibovu ni kibovu tu ikamshinda baadaye ikamfia mikononi mwake
 
Swali lingine la kujiuliza kwanini hao wenye nauli za chini wafanyakazi wao/pilot walipwe vizuri kuliko wa kwetu, bilashaka kuna tatizo mahali.
Kuna risk kubwa sana kwa pilots unaendesha ndege mbovu, au zisizo brand za abiria za made in Korea au China etc roho mkononi

Compensation ya mshahara lazima iwe kubwa kwa pilots na cabin staff
 
Gharama za uendeshaji ikiwemo airport charges na wafanyakazi lukuki ni sababisho. Ni shida sana!!!!
Hili ni ukweli kabisa.

Haya mashirika ya ndege ATCL na Precision Air yana wafanyakazi wengi sana.

ATCL kila mtu anajikuta bosi.

Precision Air ina ndege nne tu zinazo operate. Lakini ina wafanyakazi wengi sana.

Sasa kwa hali kama hii, Lazima tu watapandisha gharama ya nauli.
 
Mimi sio mtaalamu wa mambo ya ndege ila nitatoa mfano mdogo sana ili uweze kujua mojawapo ya sababu. Pata picha basi la mkoani kama Dar Express ya Ars - Dar iwe inapiga trip za ndani ya Dar kama daladala huku likiwa hata halijajaa... nadhani unaona gharama zitakuwa kubwa kwenye uendeshaji. Mfano mwingine ni watu kutumia V8 zao kwa safari za mbali lakini wakiwa town utakuta wanatumia IST, Cresta na mengine madogo. Kwa ufupi gharama za ndege ni kubwa sana.

Sababu nyingine kwa wahusika kwenye maamuzi kutokuwa na akili za kibiashara. Wangepunguza bei kidogo ili ndege zijaze na ziwe bize. Hata kama ni hasara nadhani ingepungua kiasi fulani.
 
Tukiwaambia tuige mawazo ya wateule na taifa teule la Israel mnatuona wabaya.

Upuz huu huwezi kukuta El Al
 
hakuna cha theory za demand na supply. mbona fastjet aliweza. ishu ni kwamba hakuna kitu kinachosimamiwa na serikali kikafanikiwa. mashirika yote ya serikali ni dhoofu hali. ukiritimba na ushenzi vinanajisi ufanisi. shirika linaendeshwa kama duka.
sasa kama serrikali inaingilia kati kuua supply a dominate market unasemaje hakuna theory...wengine wakija wanaondolewa ili demand izidi supply
 
Sasa hapo utashangaa Fast Jet alifanya kazi nchi hii hii lakini bei ilikua chini na hakuendesha shirika kwa hasara. Watu walikula sana mwewe Mwanza Dar kwa siku zilikua safari 4 hivi kwenda na 4 kurudi na zote ndege zinajaa abiria
jiulize alienda wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…