Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine


Yaani kutoka mbeya hadi mwanza ni sawa na Return ya Dar-Kigali
 
Kumbe ndiyo maana nashindwa kupanda ndege gharama zao zipo juu kweli. Fikiria kutoka Tanzania hadi India ni dola 450 tu
 
Nadhani moja ya sababu ni " ECONOMIES OF SCALE. Mifano uliotoa wanatumia ndege zinazobeba watu zaidi ya 250 and almost full booked. But still, Atcl na wenzake, nauli zipo unfairly high.
We nani alikwambia fly Dubai inabeba abiria 250?
Zipo ndege ndogo na kubwa lakini gharama zinakaribiana kabisa.
 
Bado tunaamini usafiri wa anga ni anasa. Ndiyo maana hadi leo mtu akisafiri kwa ndege anajiona kama ametoboa.

Serikali ilisaidie hili shirika lakini pia iruhusu ama kuvutia uwekezaji katika sekta ya anga. Kama alivyo jaribu fastjet huyu precision nae yupo yupo.

Kwa ubora wa miundombinu ya viwanja kwa sasa kutokea kusini, kaskazin, magharibi. Kanda ya ziwa, kanda ya kati ni fursa adhimu kuwekeza.

Shida naona ukiritimba umejaa kwa kuwalinda ATCL ambao nao ni wachovu tu.
Tuyakaribishe mashirika mengine kwa usafiri wa ndani.

Kafulila utakaporudi hapa njoo na muwekezaji kwa njia yako ya PPP.
 
ATCL ofisini kwao utakuta kuna wazee toka enzi ya nyerere mpaka leo ni wafanyakazi, sasa watu wa namna hii wanawezaje kufanya changes za sasa wakali wao ni wana conservative?
 
Pascal Mayalla naamini wewe umeshapanda ndege, hivyo basi kama ndege umekwisha ipanda tunaomba japo kwa uchache maelezo au maoni ya kwanini gharama ni kubwa kwa upande wa usafiri wa ndege wa ndani...
Mtanisamehe mimi ni mzalendo naitetea ATCL, it operates kwa hasara kutokana na kununua midege mikubwa ya long haul na kuzioparates domestically, zinachosha engine, wear and tear ni kubwa, take off na landing within short distance ina burns tons of fuel, hivyo ni sisi abiria tunafidia the losses.

P
 
Hii ni route ndefu sana kutoka South Amerika hadi West Europe.
wanataka wapande wenyewe tu. Walamba asali.

Hii hata Lucas hapandi
 
Kuna kipindi ulipoteza chaneli,

 
You raised good and nice concerns.

Umefanyia kazi uzi wako...au ni Barafu umerudi kivingine?
 
Shida ni bongo za tuliowapa mamlaka, ni washamba, wanachukulia vitu vingi kama ANASA. Hatuwezi kutoboa, kuagiza ka IST tu kodi mlima, gari linaonekana ANASA.
Wajue umuhimu wa muda ulimwengu huu, kwenye kila kitu anasa hazikosekani, ila zinaenda kwa madaraja.

Mtu kuoanda ndege isionekana anasa, ila anasa iwepo ndani ya mdege kwa madaraja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…