Usafiri wa anga wapata mkombozi? DAR to KIA(JRO) to DAR - TZS 88,000/=

Ndege inatarajiwa kuwasili Tar 24/nov na itaanza safari tarehe 26/nov.Nimeeshaagiza niwekewe ticket za mwezi mzima week end, niwe nakuja kuoga maji chumvi.
 
Haya ndio maendeleo tunayoyataka.Kama Air Tanzania wangetaka waonekane kweli ni shirika la wazawa,wangeyafanya haya.Inauma sana kuona yanaletwa na watu wa nje.
 
Ni kweli kabisa,Nimepiga simu kuconfirm,wamesema wanategemea kuanza either wiki ya mwisho ya November au early December!!
Hiyo cost inawezekana kabisa,kazi kwa zile airline zingine na small operators!!!

hiyo tax na other charges ni sh ngapi usikute ukiijumlisha hyo unafikia nauli ya kawaida hebu ulizia utujuze wakuambie tax na other charges utalipa sh ngapi
 
aiseeeeeee babaangu nitakuja dar kwa mara ya kwanza na ndege ngoja nijichange change kwa kuuza ndizi nije dar kwa pi kwapipa kweli
 
Huduma za ndege duniani kote huwa ni cheap sana, tulibakia Tanzania na kuonekani ni usafiri wa anasa!

Exactly. Tena nchi nyingi za Ulaya, kusafiri incountry kwa basi ama treni ni expensive kuliko kwa ndege. Sababu moja ni kwamba, kwa njia za ardhini, inakuwa ni zaidi ya safari; inajumuisha na aesthetic values, ambazo unazipata.
Tena hata kwa nchi kwa nchi, kwenye miji iliyo mipaka, usafiri wa ndege ni nafuu sana. Mfano, mtu anakaa Bremen na kufanya shughuli zake Zurich. Kwa ndege ni kama dakika 50 hadi 60+.

Kwa Tanzania, usafiri wa ndege unaonekana ni wa wenye pesa tu.

Serikali ingekuwa makini, ingefanya kinyume na hali ya sasa. Mfano, mtu anayesafiri kwa basi kutoka Dar hadi Iringa-Mbeya kwa basi, analipa si zaidi ya Tsh. 100,000. Na hii ni hata kwa wageni kutoka nchi za nje; hawa watu wanapita Hifafhi ya Taifa ya Mikumi na kuona wanyama kwa bei nafuu kabisa. Licha ya hiyo, wanapita na kuona pia mandhari ya Mlima Udzungwa, kwa bei sawa na bure. Na mandhari nyingi za kupendeza wanamopita barabarani.
Vivyo hivyo kwa wasafiri wa kutoka Arusha kwenda Mugumu via Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mamlaka ya Uhifadhi ya Ngorongoro. Hawa nao wanapata aesthetic values kwa bei chee kabisa.

Serikali makini ingewekeza katika usafiri wa anga; kisha iweke usafiri wa ardhi (basi na treni) uwe wa luxury, hususani kwa maeneo ambayo aesthetic values zake ni kubwa mno kutolipiwa zaidi.
 
hakuna cha ajabu hapo mbona johhanesburg mpaka port elizabeth (zaidi ya km 1000) ni kama $40 pamoja na VAT.

Wabongo tumeshazoea kuona usafiri wa ndege ni anasa. Ni kwa ajili wa matajiri tu; pengine watunga sera na mipango wa nchi hii wanataka kuendeleza 'status quo' hadi kwenye usafiri huo.
 
Wanataka ku-mu-overtake Dhaifu kwa kusafiri na pipa .... ... ... .. khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Sasa hapo kimenuka kitu gani wakati hiyo ni habari njema? heading utafikirimagazeti ya udaku bhana. tujifunze kuandika heading zenye maana.
 
Air Tanzania imeshatoka Mwagwipande au bado iko India kwa matibabu?
 
Hii nauli ni kawaida kabisa. Ingia mtandao wa easyjet au flybe uone kutoka London kwenda Glasgow ni bei gani. Kwa ulaya nauli ya ndege ni ndogo kuliko ya train. Mnajua kutoka Dar Mwanza ni bei kubwa kuliko kutoka London kwenda New York. Bongo bado tunaona usafiri wa ndege ni anasa kumbe siyo. Hii nauli inawezekana kabisa. Wangefanya Dar - Bukoba ingetusaidia sana.
 
Vip route ya mwisho wa reli itakuwa dolari ngapi?
 
Wakuu,
Nimeskia hawa jamaa wameanza operations zao Tanzania na flights one way gharama ni ndogo hakuna mfanowe.
Nimejaribu kutafuta taarifa hadi sasa nimegoogle bila mafanikio.
Anayefahamu atujulishe routes na gharama kwa kuanzia.
 
Nani anapenda kupoteza pesa yake kupiga simu kuuliza jibu wakati swali analo? Anyways, kwa vile Tanzania ni Bongolalaland huenda kuna mtakaowapata. Tell it to the birds sir.

Sioni ubaya kama watatekeleza. Muhimu watadumu kwa muda gani? Otherwise kama ni neema let it be!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…