Usafiri wa Dar - Mtwara umenikosha roho

Usafiri wa Dar - Mtwara umenikosha roho

Nimecheka sana sehem flan unasema ukiwa shule ungekuja kuwa Jambaz la kike kwa babe uliokuwa nao shule khaaa,,,,! Ujue kipindi cha makuzi Kijana anajiona anaweza kila kitu lkn umri unavyoongezeka kila kitu kinabadilika inabaki stori tu,,,,!

Yaani inabaki story kwa kweli.
Halafu unajua Mtwara sio kubwa kiviile enzi hizo, basi ukifanya jambo, unafahamika haraka
 
huyohuyoooo.
Pale Indian nilikuwa nakaa kota za wafanyakazi wa TRA....hapa mwanzo

mi mwenyeji sana hiyo mitaa,nyie ndio intake ya kina rafael mwango,bathlomea mihayo,peter lalubare, nk!!
 
wana radio station km tatu hivi ila mi naikubali pride fm yaani iko kimtwara zaidi vipindi vyao vimejikita sana kwa kusini hawana kuiga km radio safari wanawaiga clouds kila kitu ubunifu zero
hongera sana andrew mturi na crew yako ya asubuhi

Andrea Mturi ni mchoraji mzuri sana huyu jamaa,baadae aka okoka baada ya dada yao kufariki na kuwahusia waokoke,wakati huo niko Mtwara tulikua tunapiga sana nondo pale kwa mzee nani sijui jina lime nitoka kwa kina ras bano ligula pale.
 
Hingera jk na magufuri kwa kuwakumbuka watu wa kusini. Tukumbukeni na sisi wakiteto, safari ya kutoka dar mpaka kiteto kipande cha kuanzia runch ya nacompaka kiteto nasi tuwekewe rami.
usafiri wa kusini umekuwa mzuri baada ya kukamilika daraja la mto rufiji na barabara yake wakati wa mjomba BENI lkn le profesa imemshinda km 15 tu miaka tisa sifa hii haimuhusu
 
kwa kuchelewesha kukamilika kwa kipande cha km15 miaka tisa aiseeeeee kweli CCM majanga

Naam, hilo lisikutishe. Hata Aladin alipomjengea mfalme jumba la dhahabu alimwachia kipande kidogo amalizie mwenyewe. Hicho kipande tunawawachia UKAWA wamalizie. Mnaweza?
 
For what?? Kwani yeye ndio kajenga barabara??

Si barabara, mabarabara, mashule, vyuo vikuu, zahanati, mahospitali, madaraja, ma flyover, umeme mwingi kuliko wakati wowote ule, gas.
 
Naam, hilo lisikutishe. Hata Aladin alipomjengea mfalme jumba la dhahabu alimwachia kipande kidogo amalizie mwenyewe. Hicho kipande tunawawachia UKAWA wamalizie. Mnaweza?
but hope mmeogopa coz kipo mbioni kukamilika au ndio uvumi ulioenea kuwa wale wachina pale msituni wanafanya yao
 
Kwa kweli Madam B Mtwara unaifaham vizuri. Vipi hivi karibuni ushawahi kutembelea tena. Kuko vizuri sana kwa sasa! Ila nadhan kwa miaka inayotajwa nadhan mimi nilishamaliza kitambo kidogo sekondari miaka ile ya 97. Wakat ule Mtwara Tech nilikosoma madem hamna, munasubiri hadi.siku ya Disco munaruhusiwa kuondoa stress kwenda kucheza na Mtwara Girls. Wakati ule Manispaa ya Mtwara sekondari ni tatu tu yaani Mtwara Tech, mahasim wetu Sabasaba na Mtwara Girls. Ilikuwa bonge la raha tunafanya michezo pale TTC!

Miaka ile sisi tunasoma primary ulikuwa ukivuka Magomeni ni pori, Kanisa la Magomeni lilikuwa peke yake ni miembe tu, maembe unapiga mateke tu. Kutoka kanisa ni pori hadi pale Kijiji cha Ufukoni( Ufukweni kwa Kiswahili kilichozoeleka) kutoka pale ni pori hadi ufike Mikindani. Kutoka Mikindan ni pori hadi Mpapura yaani pale Msijute ambapo leo kuna mji na bar ile ya Mr Kweka ni.msitu mtupu. Ama kwa hakika mambo yanabadilika.

Leo hii kutoka mjini hadi Mikindani kilometa 12 ni mji mtupu na pia Mikindani hadi Msijute kilometa 7 hadi ulipo mji kinapojengwa kiwanda cha Alhaj Aliko Dangote ni almost mji tu! Ama kwa hakika Mtwara Kumekucha- KUCHELE!
 
Hahaha Madame B umenikumbusha mbali MsangaMkuu lol..inaonekana unepiga sana kusini
chingas usemayo kweli kabisa japo sijayaoanda bado hayo mabasi ila nayaona barabarani ni mazuri

Ila pamoja na yote maisha Mtwara ni ghali sana...kila kitu ghali lodge ghali msosi ghali...muda mwingi lodge zimejaa nadhani shauri ya wachimba gesi..ni kama mji umevamiwa haukuwa umejiandaa kwa maingilio makubwa ya watu..

Lingine huduma kwa wateja bado sana kwa watu wa Mtwara..ni sheeder...

Ila kwenye viwanja kweli sasa ivi ghali sana vimepanda bei

Kuna moja hiyo muuza duka ananiambia chenji hana na akaniambia nikatafute chenji halafu ndio nije ninunue kitu kwake.Kusini kule kachumbari wao hufupisha kachumba, unataka chips na kachumba.
 
Last edited by a moderator:
Inabidi tumkumbuke Kikwete.

Kweni mabasi ya JM luxury Coach ni ya Kikwete?

kama ni Barabara tunajua kuwa zote zimejengwa na kodi ya wanainchi ile ambayo hubaki baada ya kuchakachuliwa kwa saana na hawa mafisadi wa CCM
 
Kweni mabasi ya JM luxury Coach ni ya Kikwete?

kama ni Barabara tunajua kuwa zote zimejengwa na kodi ya wanainchi ile ambayo hubaki baada ya kuchakachuliwa kwa saana na hawa mafisadi wa CCM

Wanasiasa ni watu wa ajabu. Unajisifia kujenga barabara au kununua dawa hospitali, wakati huo ni WAJIBU kabisa wa kuwa kiongozi kwa kuwa pesa za nchi ni kutokana na kodi mbalimbali za wananchi na rasilimali yake.
 
Back
Top Bottom