Usafiri wa mwendokasi kwa sasa ni roho mkononi. Vituo vya kupakia abiria ni hatarishi kwa walemavu, wajawazito, watoto, wazee na wagonjwa

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2019
Posts
248
Reaction score
539
Usafiri wa mwendokasi umekuwa ni usafiri uliojaa changamoto kwa muda mrefu. Pamoja na changamoto zake umebaki kuwa usafiri wa haraka na tegemeo kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.

Kwa sasa kuna uhaba mkubwa wa mabasi kiasi kwamba unaweza kukaa kituoni mpaka masaa mawili unasubiri usafiri hivyo kutengeneza mlundikano mkubwa wa watu wanasubiri kupanda.

Kero imekuwa kubwa sana kwenye kupanda usafiri wa mwendokasi.

Hakuna utaratibu tena wa kupanda kila abiria ameachiwa afanye anavyotaka nobody cares.

Basi linapofika kituoni abiria wanaachwa wagombanie kuingia milangoni wengine wanapitia madirishani.

Kwa mtu ambaye ni mlemavu, mjamzito, mgonjwa au mzee sio usafiri rafiki na salama. Watu wanakanyagana watu wanaumizana na kila aina ya vurugu. Yote haya yanafanyika wasimamizi wa vituo na walinzi wa kampuni binafsi wakitazama kama sinema na mara nyingine wakicheka.

Nashauri serikali aidha iweke wazi kuwa kusimamia utaratibu kumeshindikana hivyo kila mtu apande at own risk ili kunusuru haya makundi maalum.

Gerezani pale mlinzi yule mapete anachochea watu kukanyagana anasema hakuna cha mstari wote ingia, unakuta mzee ameshakaa kituoni masaa matatu anataka kufika nyumbani inabidi nae ajaribu bahati yake kuwai anapigana vikumbo matokeo yake ni majeraha au kupata matatizo mengine.

Suma JKT waliuweza sana huu usafiri kwenye kusimamia nidhamu kama inawezekana warudishwe. Kiukweli ukikuta vitoto au wazee wakikanyagana unabaki unajiulkza aliyepewa dhamana kusimamia huu mradi uwa anapata muda wa kupitia field kuona end product ya kile anachokisimamia?

Kuna siti maalum za wenye magonjwa lakini huo utaratibu ni kama umepotea siku moja moja utaukuta pale gerezani tena akiwepo dada mmoja hivi mwembamba ni makini kidogo tofauti wakiwepo wengine.

Pia pale Temboni asubuhi wanajitahidi sana haswa wakiwepo wale vijana warefu unaona kweli huyu mtu kaja kazini lakini yule mwenye baraghashia nyeusi anachat wakati watu wanasukumana hana habari.

Pale gerezani ikifika jioni kuna kituo kisicho rasmi kinaapkia wanaotoa rushwa gari inafika tayari ipo level seat wakati pale ndio mwanzo wa kituo. Sasa unauza mpaka seat za wajawazito huu ni ubinadamu wa wapi?

Mama Samia mulika waziri mwenye dhamana na DG wa huu mradi ameshindwa jambo dogo kabisa la kusimamia utaratibu. Tuletee mtu anaejua binadamu wanatakiwa waheshimike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…