Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

Katika mikakati ya kupambana na ugonjwa wa Corona (Covid-19) serikali kupitia Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani linasimamia kuhakikisha kila gari ya abiria inabeba abiria kulingana na idadi ya siti zilizopo.

Mfano leo huku Wilaya ya Kigamboni ikitokea daladala imejaza zaidi ya uwezo wake na wengine kusimama, wote waliosimama wanaamriwa kushuka na kusubiri usafiri mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Safi sana hii
 
Tupo kwenye hiace tunaenda sehemu ni level seat,mwanzo tulikuwa tunajazana balaa
 
Igweeeee Wakulungwa.

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza. Mimi naaanza kama hivi.

Yaan leo daladala level seat kama tupo UK..

Shikamoo CORONA!!!

20200331_094933.jpeg
 
kunguni wa ulaya,
Corona inatucheki tu ikisema hiiiii,kwa kifupi hatupo serious.

Kwani hapo JKNIA na KIA midege kutoka kwa mabeberu imeacha kutua?
 
kama kichwa cha habari kinavyo jieleza naiomba serekali yangu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuchukua tahadhari kubwa juu ya huu ugonjwa hatari wa covic19

Hasa ushauri wangu utazingatia hasa katika vyombo vya usafiri binafsi ningependa kutoa ushauri kulingana na adha ya usafiri hasa uliopo katika jiji letu la dar kua ni mgum,ningeomba serekali iangalie kwa jicho la tatu jambo hili.

Iruhusu magari ya majeshi yetu ya polisi magereza jwtz yaweze kusafirisha abiria kwa kipindi hichi cha mpito kigumu.

Mana leo ni siku ya kwanza tu ya kutekeleza maagizo ya kukaa level city lakini tumeona chungu yake. Itakua vyema sana kama kitasikika kilio hiki itasaidia kwa kiasi kikubwa

Mwisho natoa angalizi kwa wananchi wenzangu tue waangalifu na tuchukue tahadhari na tuzidishe maombi kwa Mungu.

Kwani ni yeye tu ndie anaweza kutuvusha katika kipindi hiki kigumu.

Mwisho nampa pole Wazir wetu wa afya muheshimiwa ummi mwalimu kwa changamoto anazopitia katika kipindi hiki kigum sana

Mungu akupe nguvu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni bora serikali wafanye wasitishe watu wote wasiende makazini ili kuepusha kuenea kwa ugonjwa wa Corona kuliko kuzuia usafiri wa umma uwe level seat.

Leo kuna adha kubwa ya usafiri kwa sababu ya level seat. Ni hatari sana kwa maendeleo ya uchumi

kitochi
Uwe unafikiri kabla ya kuropoka..watu wasiende kazini,unajua athari zake wewe!!???
 
Kwani abiria mkikaa level seat hamwezi kuambukizana corona? Mi naona hio ni kuwanyanyasa abiria na wamiliki wa vyombo hivyo kwa maana akiingia muathirika wa corona akapiga chafya mle kwenye gari ataambukizwa yeyote yule eitha amekaa amesimama.
 
Back
Top Bottom