Ndugu zangu watanzania,
Nimeona ni kama kiswahili kimekuwa kigumu kidogo kwetu watanzania japo ndio lugha yetu ya Taifa au huwa tunasoma taarifa kwa juu juu tu,kama kawaida yetu ya baadhi yetu watanzania ya uvivu wa kusoma habari au taarifa kwa umakini na utulivu.
Nimepita baadhi ya maeneo na kwenye kurasa mbalimbali za Mitandao za baadhi ya watu,nimeshangaa wakitumia maneno kuwa aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali ametumbuliwa,jambo ambalo siyo kweli .
Ukweli na usahihi ni kuwa taarifa ya ikulu inasema kuwa AMEPANGIWA MAJUKUMU MENGINE,ambapo majukumu hayo bila shaka yatatangazwa muda wowote ule kwa umma, ili umma ujuwe mtumishi wao ni nani katika nafasi fulani.
Na unaweza kuta majukumu hayo mengine mapya yanaweza kuwa makubwa sana kuliko majukumu aliyokuwa nayo Awali. Kwa hiyo tuendelee kuwa na subira na utulivu kusubiri majukumu hayo mapya.
Kuelewa hiki nilichokizungumza basi angalia katika orodha hii ya majina hapo chini uende mpaka namba (IV )uone lugha iliyotumiwa katika taarifa ya Ikulu .
View attachment 3018479View attachment 3018479
Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.