USAHIHI: Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali amepangiwa Majukumu mengine na siyo kutumbuliwa. Anaweza kuwa na Majukumu makubwa kuliko ya Awali

USAHIHI: Aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali amepangiwa Majukumu mengine na siyo kutumbuliwa. Anaweza kuwa na Majukumu makubwa kuliko ya Awali

Kutegemea kupiga fix JF bila shaka utakua ama huijui JF au huna Ubongo
Jibu hoja. Hivi Kwanini CHADEMA hajuwi kujibu hoja na badala yake mnakuwa mnarukaruka tu? Unaulizwa hiki halafu wewe unajibu kile.hivi huko CHADEMA huwa mnafundishwa ujinga?nani mwalimu wenu?
 
Katika wanyama wa ajabu ni tumbili kazi Yao kuruka Toka tawi Hili na kurukia kule naona mleta mada Kwa kuruka ruka matawi hujambo umesharuka Toka tawi la Kafulila Sasa umerukia tawi.la aliyekuwa msemaji wa Serikali tawi lingine utakalorukia baada ya hapo sijui ni wapi Ngoja tusubiri
Bakuli 😂😂
 
Sie tunajua "ametumbuliwa" kwa sasa, by the way yule ni mwajiriwa wa serikali ajira yake inakoma mpaka pale atakapotimiza miaka 60. Hivyo mwajiriwa yoyote wa serikali akitumbuliwa lazima apangiwe majukumu mengine tofauti na wateule wa kisiasa kama ma-RC, DC etc wao wakitumbuliwa wanakaa benchi. Hivyo basi "mtumbuo" wa Mtumishi wa umma (mwajiriwa) sio sawa na "mtumbuo" wa Mtumishi wa umma (mwanasiasa).....mwajiriwa automatically atakuwa na majukumu mengine hata kama isipotangazwa.

Tuseme tu AMETUMBULIWA
Kwanza sisi hatuna shida na Matinya hatuhuusu, tunacholalamika ni hizi teuzi, tengua hamisha za hovyo na gharama kubwa kwa walipa kodi
 
Ndugu zangu watanzania,

Nimeona ni kama kiswahili kimekuwa kigumu kidogo kwetu watanzania japo ndio lugha yetu ya Taifa au huwa tunasoma taarifa kwa juu juu tu,kama kawaida yetu ya baadhi yetu watanzania ya uvivu wa kusoma habari au taarifa kwa umakini na utulivu.

Nimepita baadhi ya maeneo na kwenye kurasa mbalimbali za Mitandao za baadhi ya watu,nimeshangaa wakitumia maneno kuwa aliyekuwa msemaji mkuu wa serikali ametumbuliwa,jambo ambalo siyo kweli .

Ukweli na usahihi ni kuwa taarifa ya ikulu inasema kuwa AMEPANGIWA MAJUKUMU MENGINE,ambapo majukumu hayo bila shaka yatatangazwa muda wowote ule kwa umma, ili umma ujuwe mtumishi wao ni nani katika nafasi fulani.

Na unaweza kuta majukumu hayo mengine mapya yanaweza kuwa makubwa sana kuliko majukumu aliyokuwa nayo Awali. Kwa hiyo tuendelee kuwa na subira na utulivu kusubiri majukumu hayo mapya.

Kuelewa hiki nilichokizungumza basi angalia katika orodha hii ya majina hapo chini uende mpaka namba (IV )uone lugha iliyotumiwa katika taarifa ya Ikulu .View attachment 3018479View attachment 3018479

Kazi iendelee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hivi we kilaza kuna kazi inaitwa NYINGINE?
Hakuna ubishi kuondolewa kule alikokuwa na kupangiwa kazi ambayo haijulikani ni kutumbuliwa until kazi atakayopangiwa itakapojulikana.
 
Hivi we kilaza kuna kazi inaitwa NYINGINE?
Hakuna ubishi kuondolewa kule alikokuwa na kupangiwa kazi ambayo haijulikani ni kutumbuliwa until kazi atakayopangiwa itakapojulikana.
Yeye ni PS hivyo huwa anapost chochote atakachoambiwa na boss wake
 
Back
Top Bottom