Ni kweli kusema tatizo sio USAID wenyewe huenda tatizo tukawa sisi wabongo tuliopewa nyazifa mbalimbali pale boresha afya, lakini bado Boresha afya wenyewe wanayohaki ya kulaumiwa juu ya uzembe huu. Mfano kwa mkoa wa Ruvuma yapo Mashirika ambayo yanafanya kazi na boresha afya kama NICE na ROA lakini tangu watu wamalize mikataba yao hawajalipwa pesa za nauli na posho mbalimbali wakiwemo Biomedical providers na CBHSP's, labda uzembe huu au upigaji huu umetokea kwenye mashirika haya ya NICE na ROA ila ikumbukwe USAID anafanya kazi na DELOITTE kama consultant wake. Point yangu ni hii, wa kulaumiwa wa kwanza ni USAID BORESHA AFYA SOUTHERN ZONE na partner wake DELOITTE, lakini pia haya mashirika yaliyofanya kazi na USAID pia wakulaumiwa na wanapaswa kuwajibishwa juu ya hili. Tendeni haki lipeni watu stahiki zao, mnawafanyakazi wenye mkataba na wasio na mkataba na wote wana haki ya kulipwa kwasababu walifanya kazi zenu vile mlivyowatuma.