Gazeti la Mwanachi limetoa hiyo habari na USAID walitatoa Mpunga wote.
By Mwandishi Wetu
More by this Author
Dodoma. Mwezi mmoja baada ya mradi wa USAID Boresha Afya kumaliza muda wake, Serikali ya Marekani imesema imetenga Dola milioni 198 (sawa na Sh456.3 bilioni) kwa ajili ya miradi miwili kwa miaka mitano ukiwemo mpango wa Afya Bora kwa Wanufaika (C3HP).
Mradi wa Boresha Afya uliofadhiliwa na Serikali ya Marekani kwa Dola milioni 222 sawa na Sh450 bilioni mwaka 2016 hadi Septemba 2021, ulitekelezwa katika mikoa 12 ukiboresha huduma za afya ikiwemo vvu/ukimwi, kifua kikuu na uzazi wa mpango.
Akizungumza kwenye hafla ya kufunga mradi huo leo Alhamisi Novemba 11, 2021 jijini hapa, Mkurugenzi Mkaazi wa USAID Kate Somvongsiri alisema Serikali ya Marekani ipo katika hatua za mwisho za kuzindua miradi ambayo itaweza kuendeleza mafanikio ya Boresha Afya.
“Mpango huo mpya wa Afya Bora kwa Wanufaika (C3HP) utatekeleza vvu/ukimwi, kifua kikuu, uzazi wa mpango, afya ya mama na mtoto mchanga na mtoto na shughuli za mabadiliko ya tabia zako jamii itahusisha kanda ya ziwa, Kaskazini na Kati na nyanda za juu kusini,” amesema Kate.
Kate amesema uwekezaji wa mapema katika afya na ustawi wa Watanzania tangu wakiwa na umri mdogo una faida ambazo huchangia katika maisha yao yote na kufanya jamii kwa ilukumla kustawi zaidi.
“Ni kipaumbele kwa Serikali zote mbili za Tanzania na Marekani, hii inaonekana katika mkakati wa ushirikiano wa maendeleo wa nchi wa USAID wa miaka mitano,” amesema Kate.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Ummy Mwalimu aliyefunga mradi huo, ameishukuru Serikali ya Marekani kuweka fungu jingine kwa ajili ya miradi hiyo ya afya na kuahidi kuwa Serikali ya awamu ya sita itaweka mazingira mazuri kuwezesha wadau na wafadhili kwa lengo la kuimarisha utoaji huduma za afya kwa Watanzania.
“Niwasihi watu wa Serikali mnaohusika kupitisha miradi hii kuhakikisha mnaidhinisha nyaraka ili pale ulipoishia mradi wa USAID Boresha Afya muendelee na miradi mipya ili kuendeleza mlipoishia,” alisema Ummy Mwalimu.
Mkurugenzi mkazi wa EGPAF Tanzania, Sajida Kimambo amesema wanatarajia kuwekeza zaidi katika huduma ya vvu hasa kwa watoto.
“Tumefurahi uwepo wa mradi mpya endelevu kwa mikoa 12 tunaamini utajenga yale mazuri na utawezesha kuendelea pale tulipoishia, mradi wa USAID Boresha Afya umesaidia Watanzania wengi na ulitumia njia madhubuti na ubunifu wa hali ya juu kushughulikia changamoto zilizokuwepo.
“
Malengo makuu ilikuwa ni kuongeza upatikanaji na kuboresha huduma bora za afya katika ngazi ya jamii, ili kufikia kufikia malengo yake miradi ilijumuisha huduma za vvu/ukimwi, afya ya uzazi, kifua kikuu na uzazi wa mpango,” alisema Kimambo.
Naye Mkurugenzi wa Mradi wa USAID Boresha Afya, Dk Marina Njelekela alisema mradi huo wa miaka mitano umeweza kusaidia zaidi ya Watanzania milioni 8.3 walipata huduma za kupima VVU ambapo karibu watu 340,000 waligundulika kuwa navirusi na wote walianzishiwa matibabu.