USAID ni sehemu ya network ya ujasusi ya Marekani.
Trump na wafanyabiashara wenzake kina Musk wanafikiri kila kitu ni suala la biashara na miamala ya pesa ya moja kwa moja (transactional governance). Siamini sana kama ni wajinga kiasi cha kutojua miundombinu ya kimkakati (strategic framework) inayoimarisha Marekani kuwa super power duniani.
Nadhani wanatikisa kiberiti tu na kujifurahisha kuhusu nguvu ya Marekani waliyo nayo mikononi mwao hivi sasa. Wakibweka kidogo, dunia inatetemeka wao wanasikia burdani tupu!
Huwezi kuiondoa USAID. Kwa mfano zile data za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiulinzi za nchi mbali mbali zinazokusanywa na CIA zinapatikanaje?
Leo hii State Department ya Marekani wanaweza kukutajia hata idadi ya mashoga nchini kwako kwa usahihi wa >70%. Wana hata majina ya wadau maarufu (notable personalities) katika sekta hiyo nchini. Wana kompromats kibao za viongozi na wanasiasa wetu wanazotumia kuwaweka sawa wasikwamishe maslahi ya Marekani. Wanasiasa wetu wanapopanda majukwaani na kubweka propaganda zao, Marekani wanawasanifu kwa mbali almuradi hawatishii maslahi yao.
Halafu mtu aje na ujinga wa kuifuta USAID? Won’t happen.
ARV, madawa, kinga na chanjo muhimu vitaendelea kutolewa tu. Watu wa Marekani wanakula bata na kuzurura dunia nzima. Ni muhimu kwao kupunguza maambukizi duniani kote - kwa maslahi yao pia. Hiyo pesa inarudi mara kadhaa kwa dhulma kibao wanazofanya duniani.