USAID haiwezi kufutwa kwa Executive Orders; watetezi kwenda Mahakamani kuzuia uamuzi wa Donald Trump

USAID haiwezi kufutwa kwa Executive Orders; watetezi kwenda Mahakamani kuzuia uamuzi wa Donald Trump

Hili ni kinyume cha sheria. Si Donald Trump wala Elon Musk anayo mamlaka ya kufuta USAID; ni Bunge (Congress) pekee linaloweza kufanya hivyo kwa kupitisha sheria.

Kesi za kisheria zinaendelea, ili kujaribu kuzuia hili.

JFK alitoa amri ya kiutendaji kuunda USAID, kisha baadaye Bunge lilipitisha sheria iliyoifanya USAID kuwa taasisi huru. Hivyo, kufuta USAID kungehitaji sheria ya Bunge (si amri ya kiutendaji).
Naungana na Trump kwamba USAID kuna kitu nyuma yake. Hakuna mtu anaweza lazimisha kukupa msaada bila kufaidika na msaada anaokupa.

Kuna watu chumi zao zimeguswa pabaya
 
Hao Russia ni matapeli tu hawana msaada wowote wanaotoa tofauti na kuuza silaha.

China yeye ni msanii tu, yeye anachofanya ni kujenga miundombinu feki ambayo ndani ya miaka mitatu imeisha kisha anaendelea kudai pesa yake aliyotumia kukujengea na riba yake ya kufa mtu.

China na mwandani wake Russia hawana lolote na kama hao ndio wa kutegemewa kujaza ombwe inayoachwa na Marekani mbona ni kichekesho na huku wananchi wao wenyewe tu ni choka mbaya.
Sijaona ubaya wa China. Ulitaka akujengee miundombinu bure au bila riba?? Wewe una akili ya ndezi
 
Hao Russia ni matapeli tu hawana msaada wowote wanaotoa tofauti na kuuza silaha.

China yeye ni msanii tu, yeye anachofanya ni kujenga miundombinu feki ambayo ndani ya miaka mitatu imeisha kisha anaendelea kudai pesa yake aliyotumia kukujengea na riba yake ya kufa mtu.

China na mwandani wake Russia hawana lolote na kama hao ndio wa kutegemewa kujaza ombwe inayoachwa na Marekani mbona ni kichekesho na huku wananchi wao wenyewe tu ni choka mbaya.
Waafrika ni watu wasio na mchango wowote wa kimaendeleo ulimwenguni. Yani watu zaidi ya bilioni kulilia misaada na kuifanya kuwa haki yao nayo inaonekana ni sawa
 
Ikiwa Marekani itajiondoa katika kusaidia mataifa ya Afrika, kuna uwezekano mkubwa kwamba mataifa kama China na Urusi yataongeza ushawishi wao barani humo. Hii inaweza kubadili uwiano wa kisiasa na kiuchumi, huku mataifa ya Afrika yakigeukia nchi hizo kwa msaada wa maendeleo.

Kwa sasa, hatima ya USAID haijulikani. Wafuasi wa shirika hilo wanatoa wito kwa bunge la Marekani kuingilia kati ili kulinda programu zake, wakisisitiza kuwa misaada ya kimataifa ni muhimu si tu kwa masuala ya kibinadamu bali pia kwa maslahi ya kimkakati ya Marekani duniani
Mataifa hayahitaji msaada wowote. Tunachohitaji ni mahusiano mazuri ya kibiashara na kubadilishana technology basi.

Sisi ni matajiri na hata hiyo misaada sio misaada lazima kuna collateral. Hakuna mbepari anaetoa hata shillingi 100 yake bure.
 
Donald Trump wala Elon Musk
Hawa Jamaa mboni Marekani wameifanya km ya kwao na sio ya Wamarekani, wamenifanya nitafakari sana yaan wanayoyafanya kwa kukomoa watu duniani sijawaelewa kabisa tena huyo Elon Musk ndio maana alipigwa pin asilete lile dubwasha lake huku, dollars 518 million zinatolewa na Marekani kuja Tanzania kupitia USAID sijawahi kusikia imetangazwa popote
 
Waafrica tujitegemee acheni kulialia
Sio suala kuhusu wa Africa tu hii iliundwa kufanya kazi za kijasusi za kimarekani kwa kutumia misaada lakini kukiwa na egenda za USA, haikuwa shirika la kutoa tu ila miaka hiyo imetumika kufanya mambo mengi tu yako mazuri na mabaya. Ziko hata baadhi ya taasisi vidogo hata hapa kwetu wanatoa misaada lakini wana malengo mengine pia ziko mpaka taasisi za hawa LGBT misaada na agenda zao. Iko haja ya watu kusoma history why shirika lilianzishwa?
 
Mwaka juzi tu Urusi ametoka kusamehe deni la zaidi ya $bilion 20 kwa nchi za Afrika ,sasa sijui hizo hela zote walikopa kwa ajili ya Ak47?
Hata hivyo Urusi awasaidie kwani nyinyi hamna mikono ya kufanya kazi kujenga nchi zenu?
Yaani Urusi iwakamue kodi raia wake kwa ajili ya kuwahudumia nyinyi ,hali yakuwa nyinyi kodi zenu mnanunulia,magoli, ma v8 ya mabilion kila mwaka na kuiba kupeleka Uswizi?
Huo upumbavu Urusi hawezi ufanya maana alisha ufanya huko nyuma uka mgharimu na kusababisha soviet kuanguka.
Mwaka Juzi World Bank iliipa Africa $bilioni 72, US iliipa Africa $bilioni 60.
 
Hawa Jamaa mboni Marekani wameifanya km ya kwao na sio ya Wamarekani, wamenifanya nitafakari sana yaan wanayoyafanya kwa kukomoa watu duniani sijawaelewa kabisa tena huyo Elon Musk ndio maana alipigwa pin asilete lile dubwasha lake huku, dollars 518 million zinatolewa na Marekani kuja Tanzania kupitia USAID sijawahi kusikia imetangazwa popote
Kuna ujinga mwingi sana unaoendelea huko Marekani chini ya Trump.
 
Hiyo pesa ya bilion $20 ilikuwa msaada au mkopo?
Msaada ilikuwa kwenye afya, elimu nn? Pesa za Marekani hutangazwa kabisa ila sijawahi ona msaada wa China wala Russia.
Mkopo wa nini?
Acha kupiga watu changa la macho
Watu wanakopeshwa silaha na mrussia
Hata mimi sijawahi kusikia mkopo au msaada wa Russia Tanzania, labda ni silaha maana ndio huwa biashara yake inafanyika kimya kimya.
 
Sio suala kuhusu wa Africa tu hii iliundwa kufanya kazi za kijasusi za kimarekani kwa kutumia misaada lakini kukiwa na egenda za USA, haikuwa shirika la kutoa tu ila miaka hiyo imetumika kufanya mambo mengi tu yako mazuri na mabaya. Ziko hata baadhi ya taasisi vidogo hata hapa kwetu wanatoa misaada lakini wana malengo mengine pia ziko mpaka taasisi za hawa LGBT misaada na agenda zao. Iko haja ya watu kusoma history why shirika lilianzishwa?
Ni ujasusi gani wa Marekani ambao unafikiri utashindikana endapo USAID itaondoka Africa??
Unafikiri Marekani haina majasusi Urusi, Cuba, Venezuela na Iran??
 
Ni ujasusi gani wa Marekani ambao unafikiri utashindikana endapo US itaondoka Africa??
Unafikiri Marekani haina majasusi Urusi, Cuba, Venezuela na Iran??
Kuna sababu ziliwafanya 1961 kuanzisha haya wakati wa vita baridi, ilikuwa kutumia misaada na hapo hapo kupeleka agenda za kiutawala na mambo mengi haikuwa misaada tu, ilikuwa nakupa hiki ila fanyeni hili. Ni kama mabalozi wengi ni majasusi lakini wanakuja kama mabalozi.
 
Mfano Agenda gani za utawala wa Marekani zimeletwa na USAID Tanzania?

Kama ni mwanaume usiyewajibika kwa familia halafu umeenda kuomba msaada kwa tajiri ni sahihi akikuambia nakupa msaada wangu lakini sitaki ukautumie kulewa pombe au kununua malaya, nataka ukalishe familia, kulipa kodi na ada ya watoto. Sioni tatizo hapo.
 
USAID Haifanyi kazi Africa tu, kitulizeni.
Mkuu waafrika ni wajinga sana wameshupaza shingo Nyooonyooo. USAID IPO mpaka Asia, na wanaoandamana ni wamarekani wenyewe. Hizi ni ajira za watu watanzania tusiwe na mawazo hasi juu ya haya mashirika. Ndugu zetu wanapata chanjo, matibabu na mambo kadha
 
Mataifa hayahitaji msaada wowote. Tunachohitaji ni mahusiano mazuri ya kibiashara na kubadilishana technology basi.

Sisi ni matajiri na hata hiyo misaada sio misaada lazima kuna collateral. Hakuna mbepari anaetoa hata shillingi 100 yake bure.
Suala la kubadilishana technology sahau, technology unaitafuta mwenyewe au unaiba kama wanavyofanya Wachina. Kwanza Africa kuna technology gani ya kubadilishana na wengine.
 
USAID ni sehemu ya network ya ujasusi ya Marekani.

Trump na wafanyabiashara wenzake kina Musk wanafikiri kila kitu ni suala la biashara na miamala ya pesa ya moja kwa moja (transactional governance). Siamini sana kama ni wajinga kiasi cha kutojua miundombinu ya kimkakati (strategic framework) inayoimarisha Marekani kuwa super power duniani.

Nadhani wanatikisa kiberiti tu na kujifurahisha kuhusu nguvu ya Marekani waliyo nayo mikononi mwao hivi sasa. Wakibweka kidogo, dunia inatetemeka wao wanasikia burdani tupu!

Huwezi kuiondoa USAID. Kwa mfano zile data za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiulinzi za nchi mbali mbali zinazokusanywa na CIA zinapatikanaje?

Leo hii State Department ya Marekani wanaweza kukutajia hata idadi ya mashoga nchini kwako kwa usahihi wa >70%. Wana hata majina ya wadau maarufu (notable personalities) katika sekta hiyo nchini. Wana kompromats kibao za viongozi na wanasiasa wetu wanazotumia kuwaweka sawa wasikwamishe maslahi ya Marekani. Wanasiasa wetu wanapopanda majukwaani na kubweka propaganda zao, Marekani wanawasanifu kwa mbali almuradi hawatishii maslahi yao.

Halafu mtu aje na ujinga wa kuifuta USAID? Won’t happen.

ARV, madawa, kinga na chanjo muhimu vitaendelea kutolewa tu. Watu wa Marekani wanakula bata na kuzurura dunia nzima. Ni muhimu kwao kupunguza maambukizi duniani kote - kwa maslahi yao pia. Hiyo pesa inarudi mara kadhaa kwa dhulma kibao wanazofanya duniani.
 
Kwa akili yako nyembamba unadhani Republicans wote watapiga kura kama CCM inavyopiga kura kwenye bunge la Tulia Ackson?
Ngoja tuone kama watapiga kura kwa kusikiliza hizia zako na akili zako nene. USAID ndiyo inaenda kibla hivyo. ....
 
Back
Top Bottom