Usaili kwa walimu uliokuwa ufanyike Oktoba mpaka Novemba wasitishwa mpaka hapo watakapotangaziwa tena

Usaili kwa walimu uliokuwa ufanyike Oktoba mpaka Novemba wasitishwa mpaka hapo watakapotangaziwa tena

imekuaje

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
221
Reaction score
426
Usaili wa walimu Umehairishwa mpaka hapo utakapotangazwa.

Afya mpaka leo hakuna Pdf.

Je, kipi kiko nyuma ya haya?

1. Serikali haina Hela.

2. Utumishi wamelemewa.

.
IMG-20241017-WA0154.jpg


.
IMG-20241017-WA0151.jpg
 
Hili la walimu inaonekana walikurupuka walikuwa hawajajiandaa vyema.
Lakini pia inatakiwa waliangalie vyema kwa maana kuna walimu tunaweza kusema wapo outdate mfano kulikuwa na mabadiliko ya sera ya elimu 2014 kipind ambacho kuna wanachuo walikuwa wanamalizia chuo lakini waliomaliza 2015-2020 nadhan wanamawazo ya mitaala ya 2015 kurudi nyuma wakati karibia mabadiliko ya mitaala imefanyika mara mbili 2016 na sasa 2023 je huyu mwalimu utamsaili kwa kutumia mbinu zipi za 2015 au 2023? Katik hilo waliangalie kwa umakini
 
Sekretarieti ya Ajira katika Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bota wasitisha usaili kwa walimu uliokuwa ufanyike kati ya Oktoba na Novemba mpaka hapo watakapotangaza tena.
IMG_3984.jpeg
 
ya mitaala ya 2015 kurudi nyuma wakati karibia mabadiliko ya mitaala imefanyika mara mbili 2016 na sasa 2023 je huyu mwalimu utamsaili kwa kutumia mbinu zipi za 2015 au 2023? Katik hilo waliangalie kwa umakini
Sio kweli mkuu ,unless hujui maana ya mtaala na sera, mtaala ni long plan while sera ni short plan,Kwa Sasa Bado tunatumia mtaala wa miaka ya 90+ isipokuwa Kwa mtaala ulio Anza kutumika mwaka huu tu Kwa wanafunzi wa kidato Cha kwanza na wale darasa la 1-3 tu ndo Wana mtaala mpya
 
Nchi inawenye nchi
Walanchi na wananchi
 
Hii ni kupisha uchaguzi tu mzee baada ya hapo taratibu zote zinarudi kama zilivyopangwa
Uchaguzi unahusiana vipi na usaili, kuna kitu kipo nyuma ya hili, uchaguzi unasimamiwa na Tamisemi na usaili ni Tume ya ajira hizi ni idara mbili tofauti.
Mbona wizara nyingine mambo hayajasimama yanaenda vilevile.
 
Narudia Tena yote hayo ni tisa la kumi ni wasiwaache wajomba na mashangazi waliomaliza tangu 2015 ,2016 2017, 2018,2019 .This is a red Dark red sin.

Hawa watu ni kama vichanga waliotolewa mimba wakatipwa chooni.
Hawa watu ukiwaona or ukiwa Nao jirani Utaelewa ninalosema. Ni aina mbaya ya dhulma. Maana Kila kitu maishani mwao kimesimama na umri Nao unawapungia mkono.😭😭😭😭
 
Back
Top Bottom