Usaili wa utumishi (kwenye interview ya mchujo) unawalenga wanafunzi na wahitimu wapya

Usaili wa utumishi (kwenye interview ya mchujo) unawalenga wanafunzi na wahitimu wapya

Uponyaji na uzima

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
666
Reaction score
1,255
Nimehudhuria usaili kadhaa wa utumishi kwa kazi nilizoomba kupitia ajira portal wiki hii. Ni kazi za ICT officers.

Kwenye mchujo (written interview) wanauliza maswali ambayo ni ya wanafunzi, yale maswali yanayohusisha kukariri vitu vingi na terminologies.
 
Ndio usahili (written) upo hivyo.....ulitaka wakuulize kuhusu uzoefu wako kwenye written ?
Serikali inaajiri watu waliokariri mambo na hawajui chochote katika mazingira ya kisasa ya utendaji kazi ni jambo baya.

Hawa wahitimu wapya wasiokuwa na uzoefu kabisa wanaenda kufundishwa kazi na wafanyakazi waliopo serikalini sasa hivi.

Tunafahamu jinsi utendaji wa hawa watu wetu serikalini hivyo hawa wapya watakuwa kama hao hao. Vicious cycle.
 
Anachoongea mtoa mada kina logic, km amemaliza miaka 4/5 iliyopita ni kazi kukumbuka terminology hizo anazosema.
Afadhali mkuu umenielewa. Wanatakiwa kuwa na aina tofauti za usaili kulingana na uzoefu wa mhusika.

Wanaita watu wenye 8+ years experience na certifications kama ITIL, Cisa, PMP etc halafu wanakuuliza terminologies ambazo hazihusiki kabisa kwenye modern IT.
 
Upo sahihi boss, hapo kwenye aina tofauti za usaili nimekuelewa
 
Kwahio unadhani vijana ambao hawajapata nafasi ya kufanya kazi Ni sahihi kuulizwa maswali yanayohitaji mtu mwenye uzoefu wa kazi?
Anachoongea mleta mada ni kuwe na balance

Huwezi kuweka post ambayo ni skills based ambayo inahitaji experience halafu umuulize mtu maswali ambayo yanamuhitaji akazikeshee modules alizozisoma miaka 6 nyuma

Mfano TTCL wanatafuta labda mtu wa ICT au Marketing lakini wanampa utumishi watafutie candidates lakini wao mwisho wa siku wanaangalia mambo ya darasani. Unadhani watapata mtu competent
 
Kwahio unadhani vijana ambao hawajapata nafasi ya kufanya kazi Ni sahihi kuulizwa maswali yanayohitaji mtu mwenye uzoefu wa kazi?
Mimi napendekeza usaili uwe tofauti kulingana na uzoefu wa waombaji. Wasiokuwa na uzoefu wapimwe kwa waliyosoma darasani na hawa wa makazini wapimwe kwa uzoefu wa kikazi.

Hii itasaidia serikali kupata watu wenye uwezo wa kutoa matokeo chanya.
 
Anachoongea mleta mada ni kuwe na balance

Huwezi kuweka post ambayo ni skills based ambayo inahitaji experience halafu umuulize mtu maswali ambayo yanamuhitaji akazikeshee modules alizozisoma miaka 6 nyuma

Mfano TTCL wanatafuta labda mtu wa ICT au Marketing lakini wanampa utumishi watafutie candidates lakini wao mwisho wa siku wanaangalia mambo ya darasani. Unadhani watapata mtu competent
Good point [emoji117]
 
Serikali inaajiri watu waliokariri mambo na hawajui chochote katika mazingira ya kisasa ya utendaji kazi ni jambo baya.

Hawa wahitimu wapya wasiokuwa na uzoefu kabisa wanaenda kufundishwa kazi na wafanyakazi waliopo serikalini sasa hivi.

Tunafahamu jinsi utendaji wa hawa watu wetu serikalini hivyo hawa wapya watakuwa kama hao hao. Vicious cycle
Freshers nao wanastahili fursa Kama vijana wengine
 
Freshers nao wanastahili fursa Kama vijana wengine

Kweli bro, freshers wengi wamesaidiwa natamani entry level jobs wazidi kuzipata lakini pia mashirika yetu yanahitaji watu wenye uwezo na ubunifu pia

Kumbuka haya mashirika yanapotoa huduma mbovu au yanapoendeshwa pasipo usimamizi thabiti. Tunaumia nchi nzima kwa sababu wote tunatoa kodi ili watu wapate mishahara

Leo hii shirika la serikali lina mtu wa ICT ila kakitu kadogo tu inabidi wachukue mtu kutoka nje au waombe consultancy, hizo gharama unadhani nani analipia kama sio mimi na wewe
 
Back
Top Bottom