Usajili huu unaofanywa na Simba ni mapendekezo ya kocha gani? Ni uhuni na kukosa weledi, wamechanganyikiwa

Usajili huu unaofanywa na Simba ni mapendekezo ya kocha gani? Ni uhuni na kukosa weledi, wamechanganyikiwa

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Sote tunajua wazi simba hawana kocha tangu pablo kutoka real Madrid afukuzwe.

Kwa hivyo nafasi yake yupo kocha wa muda ambaye alikuwa msaidizi yaani matola.

Wakati haya yakiendelea huko yanga wanafanya usajiri wa lazarous kambole ambaye ni pendekezo la kocha nabi, kwa maana yanga wanafanyia kazi mapendekezo ya kocha wao.

Hii ni maana halisi ya uweledi katika kazi kama ambavyo mataifa mengine yanafanya, ikumbukwe kuwa kocha nabi aliletewa beki wa kushoto kutoka Uganda mustapha kiiza lakini alimkataa na uongozi ukaachana naye.

Sasa huku simba hawana kocha je mapendekezo haya ya usajiri ni kutoka kwa nani?

Wamemsajiri Moses phiri je amependekezwa na kocha gani?

Wamemsajiri victor akpan je kocha yupi amependekeza?

Hapa unakuja kugundua wazi simba kuna wizi na upigaji mkubwa sana, naanza kuamini yale mambo ya 10 percent kuna wapiga dili wengi humo.

Halafu kwa mtindo huu eti wanataka waingie fainali huko cafcl!

Utaingiaje ikiwa unao viongozi wezi na wapiga dili?

Utaingiaje ikiwa tajiri yeye ndo anasajiri bila mapendekezo ya kocha?

Utaingiaje ikiwa team ina migogoro ya ndani kwa ndani baina ya viongozi wenyewe ambao kiuhalisia wote ni wezi na wamepishana maslahi yao ya wizi?

Sawa basi tuseme matola ndo amemtaka akpan? What next then?

Halafu akija kocha mpya anapewa wachezaji hawa wa hovyo waliosajiriwa kwa madili na 10 percent eti malengo yetu ni kufika fainali! Fainali ipi hiyo?

Haya bwalya ameachwa, je ni pendekezo la nani kuwa aachwe? Kocha gani?

Vipi kocha mpya asisubiriwe kwanza kisha achague wachezaji anaowataka na wale watakaotemwa sababu yeye ndio mkufunzi wao?

Kuna harufu ya rushwa na upigaji mkubwa sana humo..! Na sio ajabu tukaambiwa pablo ametoka real Madrid kumbe ni wizi na udalali.

Simba ni klabu inayoendeshwa kizamani

Mwisho kuiga wengne wanayofanya ni sawa sio dhambi, yanga apongezwe kwa hili.
 
Wanakwambia kuwa mchezaji ni mali ya club, kocha yeye atafanya kazi na wale wachezaji anao wakuta.
Pili, mkocha wamekuwa mawakala...hivyo wanapendekezaga wachezaji ambao ni wateja wa mawakala wa kocha
Mpe mchezaji kocha anayemtaka, ili akifeli yeye na wachezaji wake wakose visingizio..!

Uliona pablo alivyokuwa anaitemea management shit kufanya vibaya? Angepewa wachezaji anaowataka angesingizia nini?

Kwamba bora madalali wa team ndio walete wachezaji wao wampe kocha kwamba " bwana huyu mchezaji wangu acheze asikae benchi" au sio?
 
Sii unajua tena mjini tunaishi kwa kupiga dili. Maana ukimuachia kocha atampoint mchezaji amabye nyie hamuwezi piga hela.
 
Msimu huu tutawatesa sana!! Subirieni mtaona. Wala usinikatalie wala usinikubalie, tusubiri mtaona.
 
Na walivyo hawana akili wanaingia kwenye mkenge wa kupunguza wachezaji wengi kwenye timu yao
 
Msimu huu tutawatesa sana!! Subirieni mtaona. Wala usinikatalie wala usinikubalie, tusubiri mtaona.
Msimu huu si ndo unaishia hivyo?

Kutesa wapi tena huko? Au pale bunju?
 
Na walivyo hawana akili wanaingia kwenye mkenge wa kupunguza wachezaji wengi kwenye timu yao
Wakati wachezaji wanao wachache sana ambao wanaweza kuwa fiti muda mrefu, wengine ni tia maji tia maji tu Trip shamba trip garage.

Ukiwaambia hawataki kuelewa
 
mimi mwemyewe nimehamia yanga , hu ujinga umenichosha team inaendeshwa bila weledi kabisa,wanajisajilia tu angalia usajili wayanga ulivyotulia walahi hadi raha yaani, kambooole watakoma mabeki mwaka huu
Hata mugalu akienda yanga atafunga sana tu, uongozi mzuri kwanzia juu mpaka kwa kocha kwenda uwanjani.
 
Simba wanafanya kosa lile lile walilokuwa wanafanya Yanga miaka ya nyuma. Ni kitu kiko wazi kabisa Team inatakiwa isajili kocha kisha ifuate kusajili wachezaji. Sasa unasajili wachezaji alafu kocha! Unakuwa umesajili kwa mapendekezo ya nani?

Uswahili huu uliiponza Yanga kwa miaka minne nyuma, Simba wanauiga
 
Wanakwambia kuwa mchezaji ni mali ya club, kocha yeye atafanya kazi na wale wachezaji anao wakuta.
Pili, mkocha wamekuwa mawakala...hivyo wanapendekezaga wachezaji ambao ni wateja wa mawakala wa kocha
Wanasahau mapema zile pigo za Zahera😂
 
Mashabiki wanashangilia kila kitu as long as timu imeamua.

Kocha akija ataambiwa ukifungwa mechi tano mfululizo tunakutimua 😃😃.

Nahisigi makocha wanakuja kufundisha timu ka hizo wanakuaga na njaa sana maana kufanikiwa sometimes huwa ni bahati na sarakasi za nje ya uwanja.
Wakija wale professional basi wataomba kuondoka wenyewe tu kwa figisu za wazawa.
 
Nyinyi ambao Kocha ndie anasajili na anasikilizwa kwa kila kitu mmewahi fika wapi huko Caf champions league??
 
Back
Top Bottom