Usajili Mpya Simba SC: Umakini na utulivu wa kiwango cha juu sana unahitajika

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mtendaji mkuu wa Klabu ya Simba (CEO), Senzo Mazingiza amethibitisha kupokea ripoti ya kocha Sven Vanderbroeck kuhusu Usajili wa msimu ujao Katika ripoti hiyo Kocha Sven anataka wachezaji 5 wa nguvu ikiwa wawili wachezaji wa ndani na watatu wachezaji wa nje na kazi ya kutafuta wachezaji hao imeanza mara moja.

Katika ripoti hiyo Kocha Sven amesema kigezo cha umri na uwezo kitumike haswa kuchagua wachezaji hao wachezaji wanaotakiwa ni mabeki watatu ikiwa wawili wa Kati na moja wa kulia, kiungo mkabaji mmoja na mshambuliaji mmoja. Senzo amesema wameanza kubainisha wachezaji hao kabla ya kuwachuja na kufanya Usajili.

Kimsingi nafasi anazohitaji kocha zina matatizo makubwa,ukweli usemwe. Simba SC haina beki wakushiba. Simba SC ina shida ya striker wa kumsaidia Kagere Meddie.

Repoti inasema kocha anataka wachezaji wa nje watatu. Hapa ndio umakini wa kiwango cha lami unahitajika,tusifanye makosa kama tuliyofanya kwa Wabrazili. Kwa maoni yangu hao wageni wawe ni Striker mmoja msaidizi wa Kagere. Beki mmoja wa kati anahitajika sana maana upepo wa Nyoni umekwisha. Pia mgeni mmoja wa kumsaidia Shomari Kapombe.

Katika hizo nafasi 2 za local prayers napendekeza uongozi wa Simba SC wamuulike Lusajo wa Namungo na Nondo Mwamnyeto.

Kuna strikers kadhaa wa kigeni wanatajwa kufanya mazungumzo na Simba SC, mmojawapo akiwa Justin Shonga wa Orlando Pirates. Kama tetesi hizi ni kweli basi itakuwa bonge moja la usajili. Kiukweli Simba sc inahitaji wachezaji wenye speed kama Shonga.

Wapo wachezaji ambao inabidi wapewe mkono wa kwa kheri hata kama ni kwa mkopo. Mmoja wapo ni Beki wa Kati Mbrazili, Haruna Shamte, John Bocco, Saidi Ndemla, Mlipili na Nyoni. Wako baadhi bado ni wazuri ila sioni namna watakavyoweza kupata nafasi ya kucheza.

Haya ni maoni yangu binafsi. Jambo la msingi ni kuwa usajili uliopita Simba Sc iliboronga. Ni matumani tetu msimu mtatumia akili kubwa kwa sababu ya uongozi imara chini ya CEO Senzo.
 
Trust me
Wanaondoka ni
Tairone
Shamte
Mlipili
Ndemla/fraga
Dilunga kuna biashara



Wanaokuja suggestion
Shonga
Mwamnyeto
Kelvin kijiri
Yondani
Papy Shishimbi 2years contronct /tayar huyu
 
Huyo Justin Shonga ni mtambo hatari, dogo ana vyenga,mashuti na spid moja matata sana...Kama tutampata na tukasajili beki bora hakika Simba tutatisha sana, kuna timu tutazipiga goli 20.

Wasiwasi wangu kwenye malipo tu ya huyo Shonga, jamaa ni ghali sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie mnawajulia wapi hawa? Mnaangaliaga ligi ya South au kwenye Champions League?
 
Huyo shonga ni majerui? Mbona ktk 3 za ufunguja hayupo pale Orlando?

[emoji116]



Sent using Jamii Forums mobile app

Isijekuwa tunapigwa tena[emoji16][emoji23]
 
Huyu shonga tulimkosa msimu uliopita nahisi shida ilikuwa malipo,ila kiukweli Simba na wachezaji wengi ambao wamekuwa mizigo hatustahili kuwa nao mfano Wawa,Bocco,Shiboub,Kennedy,shamte,fraga,tairone,ndemla,nyoni,kichuya siioni nafasi yake,manula anahitaji golikipa mkali wa kumpa changamoto,beno ana makosa mengi ya kujirudia, Kagere bado mzuri ila sio wa kumtegemea kwa hundred percent ametumika sana.Simba tunahitaji mabeki wa kati wakali na wenye uzoefu mkubwa, tunahitaji kiungo mkabaji anayemzidi Jonas mkude vitu vingi sio tu kukaba, tunahitaji striker atlest wawili wazuri hapa Africa hawakosi,ila ombi langu tuache kusajili wachezaji waliomaliza mikataba ikibidi tuvunje benki huwezi kupata mchezaji mzuri akiwa free huu ndio ukweli,Kama tupo serious na mpira wa Africa tuvunje benki na tutumie hela nyingi ktk usajili,pia wachezaji wa ndani tuchukue wale wenye quality ya Hali ya juu sio kwasababu Yanga wanataka na sisi tumo hii sio akili.
 
Nimekupata, ila wachezaji 5 wengi sana,

3 wanatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
Watatu hapana mkuu, useless player wapo wengi sana pale Simba,ukisema watatu hebu piga hesabu za kawaida tu kwa beki za kati Wawa, tairone,nyoni, Kennedy,mlipili hao wote hakuna wa afadhali labda nitamtetea mlipili hapati nafasi,haya njoo kwa beki wa kulia kapombe hatabiliki muda wote anaweza majeruhi nani mbadala wake shamte?, huwezi kumpanga shamte mbele ya mawinga wasumbufu na wazuri atakuwa uchochoro muda wote,hadi hapo watatu wameishia kwa mabeki tu,ukija kwa kiungo mkabaji mkude sio yule tunayemjua ubora na spidi vimepungua, ukija kwa striker ukimtoa Kagere ktk ufungaji magoli mengi ya Simba yamefungwa na viungo hatuna striker pale.
 

Nyinyi mnaweza kuwapata wachezaji wanaowataka Yanga?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…