Usajili wa Kampuni Brela

Usajili wa Kampuni Brela

Habari, kwenye usajili wa kampuni mmiliki anaweza kuweka mtaji wowote ambao anajua ataweza kuufanyia biashara yake hata kama kwa muda huo asiwe nao mkononi au benki. Hii ni kutokana na kwamba zipo njia mbalimbali ambazo mmiliki anaweza kutumia kukuza mtaji wake wakati wowote ikiwemo kukopa benki au kuongeza mwekezaji mwingine mara tu baada ya usajili ili kuufikia mtaji anaohitaji kufanyia biashara. Hata hivyo inashauriwa mmiliki kusajili mtaji ambao unauhalisia na biashara anayofanya au anayokusudia kufanya.
Brela naomba utofauti kati ya kusajili jina na kusajili kammpuni.

Maana kuna wanasheria niliwapa kazi ya kusajili kikundi kama partnership.

Wameniambia wamesajili Jina ambalo litatupa uhalali wa kununua na kuuza any proparties like ardhi na miradi mingine.

Naomba kufahamu je tutakuwa na uhalali huo?
 
Habari, kampuni ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye nia ya kufanya biashara halali na kuusajili mjumuiko huo chini ya Sheria ya kampuni, aina za kampuni kampuni inaweza kuwa kampuni ya kigeni,kampuni binafsi au kampuni ya umma, kwa upande wa jina la biashara ni utambulisho wa biashara fulani inayofanywa na mtu au kikundi cha watu, hivyo mtu mmoja au kikundi cha watu wasiozidi 20 wanaweza kusajili jina la biashara, mfano wa majina ya biashara ni Ali Entreprises, Rose Beauty Salon au John Urassa Investments. Kwa aina ya biashara ambayo unatarajia kufanya inawezekana lakini unatakiwa kufanya maombi ya leseni ya biashara husika kutoka BRELA kupitia mtandao wetu wa business.go.tz
 
Eleza hapa kama kuna tofauti kati ya TEMBO LIMITED na ELEPHANT BREEDERS LIMITED. Hii ndiyo muhimu ili na wengine waelimike.
Ila Brela akili zao. Sasa hapo usikute wameamua kulinganisha tembo na elephant. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
NAdhani gharama za kuanzisha kampuni Tanzania ni kubwa mno; hizo nilizowekea rangi hapa chini. Hazichochei uanzishwaji wa makampuni

-------------------------------------------------------------------

WAKALA wa wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) wamezitaja ada za usajili wa kampuni mpya ambapo gharama zake zinaanzia Sh.20,000, Sh.1000,000, Sh.5,000,000,Sh.20,000,000 mpaka Sh.50,000,000 na kwamba viwango hivyo ni kutokana na mtaji wa kampuni husika na kwa usajili wa kampuni za kigeni gharama za usajili ni Dola za Marekani 1,190,Filing fee ni Sh.66,000 na Stamp Duty 6,200.
 
Habari, ilikuweza kupata taarifa sahihi za ada za usajili wa kampuni kulingana na mtaji wa kampuni tembelea katika tovuti yetu ya www.brela.go.tz au wasiliana nasi kupitia namba yetu ya kituo cha miito BRELA 0222 212 800 kwa maelezo na ufafanuzi zaidi.
 
Back
Top Bottom