Usajili wa Okrah: Simba SC leo wamepiga kwenye mshono haswa

Usajili wa Okrah: Simba SC leo wamepiga kwenye mshono haswa

Namaanisha kwenye mshono kweli.

Hii ni baada ya kutangaza usajili wa winga/kiungo mshambuliaji Augustine Okrah.

Huyu jamaa nilijua yupo kwenye timu ya taifa ya Ghana, lakini sikujua kumbe kutoka kwenye ligi ya ndani [ligi kuu ya Ghana], jamaa ametoboa kwenye kikosi na mwenzie mmoja pekee.

Namaanisha, kutoka ligi kuu ya Ghana, wachezaji waliofanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu yao ya taifa ni Okrah na mwenzie mmoja, wengine wote wametoka nje ya nchi.

Sasa hapa utamlinganisha Okrah na nani? yule mvuta bange anayelilia kuitwa timu ya taifa ya kwao lakini haitwi? au wale wazee waliokuwa rejected Congo, Angola, na Ulaya ambao tunapigiwa kelele kila siku za kuwasifia na wasiojielewa?!

Kwa hili teke la chini ya mkanda walilopiga Simba SC leo kwenye usajili, nawashauri watoe siku tatu za mapumziko kwa utopolo mpaka watakapopata nafuu ndio watangaze kifaa kingine, uto wasije kutoka damu buree..
Tutawafungulia bendi ya taarab muwe mnatuimbia humu jukwaani. Maana muda wote mmekalia vijembe na mipasho tu.
 
Tutawafungulia bendi ya taarab muwe mnatuimbia humu jukwaani. Maana muda wote mmekalia vijembe na mipasho tu.
Kama unaona Okrah kuitwa timu ya taifa na mwenzie toka ligi yao ya ndani ni mipasho, basi Morisson kutokuitwa ndio fact kwako!.

Uto juu..!!
 
Ha ha hii comment inasadifu kichwa cha uzi pole mkuu, ndiyo utofauti huo wa Timu ya kimataifa na wanaoigiza huku wakiwa na kelele nyingi
Yes, maumivu ya kwenye mshono hayo, ndio maana nimeshauri wapewe siku tatu wakusanye nguvu tusiwatoe damu!
 
Mmekuwa wapole kwani mmenyeshewa na mvua leo?!
Huo upole unatupa wewe,hamna hata mchezaji wa kufanya tuwe wapole pale,nyie endeleeni kujifariji ndio wakati wenu huu,sie hatuna habari tunawasikilizia msuva na aziz ki wetu
 
Ghana hiyo hiyo ambayo morisson anatokea ndio Ghana hiyo hiyo ambayo Simba wamesajili mshambuliaji ambaye anakiwasha QATAR
Sikutegemea na wewe kufikia levo ya umbumbumbu kiasi hiki .Qatar gani alikokiwasha ya Buza au ? hujui kuwa huenda hata asipate nafasi ya kuitwa tena timu ya Taifa baada ya kuja ukoloni vilevile mchezaji anaweza akaitwa timu ya Taifa mechi moja au mbili halafu akapigwa pini ?

Nafasi yake ya kuitwa tena labda akiwashe kwa kiwango kikubwa tena Simba kwani hapa ni bongo mchezaji anaweza kuja na Cv kubwa mwisho wa siku akachemsha vibaya .
 
Ghana na Nigeria bila kuhonga uitwi timu ya Taifa. Ata Azam ilikua na wachezaji wanaitwa timu ya Taifa kwakua walikua wakijiongeza.
 
Huo upole unatupa wewe,hamna hata mchezaji wa kufanya tuwe wapole pale,nyie endeleeni kujifariji ndio wakati wenu huu,sie hatuna habari tunawasikilizia msuva na aziz ki wetu
Alaah, kumbe matumaini yenu yako kwa wawili tu?!
 
Ghana na Nigeria bila kuhonga uitwi timu ya Taifa. Ata Azam ilikua na wachezaji wanaitwa timu ya Taifa kwakua walikua wakijiongeza.
Uto tuwekee ushahidi, hapa sio kijiwe cha porojo.
 
Sikutegemea na wewe kufikia levo ya umbumbumbu kiasi hiki .Qatar gani alikokiwasha ya Buza au ? hujui kuwa huenda hata asipate nafasi ya kuitwa tena timu ya Taifa baada ya kuja ukoloni vilevile mchezaji anaweza akaitwa timu ya Taifa mechi moja au mbili halafu akapigwa pini ?

Nafasi yake ya kuitwa tena labda akiwashe kwa kiwango kikubwa tena Simba kwani hapa ni bongo mchezaji anaweza kuja na Cv kubwa mwisho wa siku akachemsha vibaya .
Wacha ramli, usimuonee wivu mwenzio, mbona Morisson hata kuitwa hiyo mara moja tu bado..!!
 
Viongozi wao wanawajua kwamba wao wakiona Cv wanaridhika ndio maana wakaletewa Pablo kutokea Real Madrid ya Buza.
20220521_002908.jpg

Tushawazoea hao
 
Back
Top Bottom