Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,618
Sasa nimeelewa. Hiyo kwenye mpira wa miguu nimeshawahi kusikia
Ukifuatilia vizuri utakumbuka kuna kipindi Shigongo na Magazeti yake waliongoza harakati za Ali K ni bora zaidi ya Diamond, hii ilikuwa baada ya kushindwa kufika bei kwenye tamasha la Matumaini.
Baada ya kushindwana na D ndo kukubaliana kuwa atakuwepo Ali K, so ilibidi washabiki waaminishwe kwamba Ali K (King) ni bora kuliko D.
Clouds waliwahi hadi kutengeneza clip ya King is Back ambayo Joti alishiriki pia, wakatengeneza kundi la kumzomea D atakapopanda Jukwaani nk, hii yote ilikuwa ni kuwaonesha wale washabiki wasiofungamana na upande wowote kwamba Ali K ni bora zaidi, na hivyo waone sawa tu ikitokea D asiwepo akawepo Ali K.