Hii Yanga ni next level, Eng Hersi ni mtu mbad na hana nia njema na ligi yetu, yaani hataki timu yoyote kupata japo droo mbele ya Yanga.
Mi naona kila idara imejaa, hakuna gepu, Yanga inaweza kuwa timu pekee duniani yenye vikosi vya kwanza viwili na nusu, yaani unatoa 11 unaweka 11 na goli ni zile zile 5 - 0 kama kawa.
Mbumbumbu kazini kwao kuna kazi. Ni ngumu sana kwao kurudia ufalme wao zilipendwa!
Yanga washambuliaji ni moto mkali, viungo moto, mabeki moto na kipa la dunia Diarra limesalia jangwani.
Ili kuitendea haki timu, Yanga iombe friendly match na Madrid au PSG. Hiyo ndio level yetu kwasasa!!
Hersi hafai, ametisha mno. Na tumpe maua yake kwa usajili wa kuua ligi. Yaani Hersi ameleta SMG kuua mbu tu!