mpimamstaafu
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 4,445
- 4,707
Duniani kote mchezaji wa mpira kabla ya kusajili hufanyiwa uchunguzi wa kiafya na madaktari maalumu wa michezo.Hivi karibuni Klabu ya Yanga imekuwa inafanya Usajili kwa kasi kubwa kama vile Wachezaji wazuri wanakwisha.Pili Tumekuwa tunasikia mchezaji hatari kwa chenga amesajiliwa lakini hatusikii kuwa Mchezaji fulani amefanyiwa vipimo vya afya kisha baada ya vipimo kuwa sawa kasajiliwa.Natoa taadhari sana kwa Uongozi wa Yanga kushughulikia Vipimo kwanza kabla ya kumsajili hao wachezaji wamekwisha tumika sana kabla ya kuja Yanga.