MAMESHO
JF-Expert Member
- Jul 5, 2011
- 1,432
- 1,738
Habari za leo wana Jf.
Hakika ni ijumaa njema yenye baraka.
Hivi karibuni nimefika eneo moja la michezo ya watoto hapa jijini.
Awali lilikuwa limefungwa kwa ajili ya ukarabati kwa sasa wamefungua.
Eneo hilo lilikuwa lina maeneo matatu.
Eneo la kwanza unalipia kuna farasi magari na midoli ambayo inanesa nesa na watoto wanajishika.
Eneo la pili lina bembea, vijumba vya kudumbukia na kutoka, sehemu za kupanda na kushuka na bembea za kuzunguka.
Eneo la tatu ni mabwawa mawili ya kuogelea. Moja ni kubwa jingine ni dogo.
Japo sina utaalamu wa kujua usalama wa maeneo ya michezo ya watoto niliweza kugundua baadhi ya mambo ambayo hayakuwa sawa.
1. Sehemu za mabwawa hazikuwa na kingo kuzuia watoto wadogo kuweza kutumbukia.
2. Waangalizi kuwa mbali sana na kujihusisha na mambo yao wakati wanacheza.
3. Michezo ya umeme kuyokuwa na plug in badala yake nyaya kuchomekwa directly kwenye socket.
4.contol panel za michezo ya umeme kutofanya kazi. Incase wanataka kuzima wanazima ukutani.
5. Kuwepo kwa michezo chakavu ambayo vyuma vyake vinaweza kuleta madhara kwa watoto.
6. Eneo la mabwawa kutohoji ikiwa wanaotaka kuogelea wana uwezo huo na kuwepo muokoaji ikiwa kuna atakayepatwa na shida.
Swali.
1. Je hapa nchini kuna wakaguzi wa maeneo ya michezo ya watoto?
2. Je wanaotaka kufanya biashara hiyo wanapewa orodha ya mambo ya kuzingatia?
3. Kwa vile vifaa vinavyotumika kuna ambao wanathibitisha usalama wake kabla ya kuanza kutumika?
4. Je ikiwa tumeona kuna hatari maeneo haya tufanyeje.
Ni hayo tuu wakuu.
Tuwapende watoto wetu na tuhakikishe usalama wao.