Usalama wa nyumba zilizozungushiwa nyaya za umeme za ulinzi au electric fence

Usalama wa nyumba zilizozungushiwa nyaya za umeme za ulinzi au electric fence

Nyumba zilizozungushiwa nyaya za umeme za ulinzi au electric fence zinaonyesha ziko salama sana maana zinadili na njia kuu ya wizi au ujambazi kufanyika.

Mara nyingi huduma hii inaambatana na uwepo wa cameras ili kuongeza zaidi ulinzi.

Umewahi kusikia uvamizi umefanyika katika nyumba zenye electric fence?

Je, ukiweka hizo nyaya za ulinzi za umeme bila kuweka cameras, wahalifu wanaweza kata hizo nyaya na kuingia ndani kirahisi?

Nauliza haya maswali kwa sababu nataka kuweka ulinzi wa aina hii katika eneo la heka moja bila kutegemea sana cameras ingawa zitakuwepo chache.
Wazo zuri,si kwamba inazua wezi kwa asilimia 100,but inapunguza uwezekano wa kuingiliwa na wezi...

*Sababu mwizi lazma awe expert wa kutegua mfumo hivyo wezi vilaza watagaili

*Inaongeza usumbufu kwa mwizi,baadhi watagaili

Ukiongeza Camera,na motion sensor utakua umetisha zaidi.
 
Mkuu,
Kwa manufaa ya jukwaa. Umeme unaotumika ni wa majumbani. Tofauti umeme wake ni DC yani direct current na umeme wa majumbani ni AC yani alternate current.

Kinachofanyika ni kuwa controller yake ina AC to DC converter ambayo ubadili umeme wa kawaida AC kuwa wa DC.

Uwepo wa DC power ndio inafanya zile nyaya kuwa hatari zaidi.

Pia controller yake ina inbuilt betri inayokaa masaa manne iwapo umeme ukikatika.

No need of backup generator...
Good explanation ila kwa nilipokua mimi kulikua na generator mkuu na sehemu nyingine hakukua na generator but still ilikua inawaka sababu ya hio battery umesema ambayo imeungwa nayo kutunza umeme, kwenye suala la conversion toka DC to AC mimi sijui chochote kuhusu hilo sababu mimi sio fundi umeme
 
Solar power ya automatic generator?
Kwa upande wangu ningechagua automatic generator maana hiyo unaweza kuiconnect kwenye nyumba nzima unakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja. Solar power ili icover nyumba nzima inahitaji yenye nguvu kidogo labda kama hizo nyaya peke yake ndiyo ziendeshwe na solar muda wote.
 
Hapo inabidi ukutane na maexpert wakusukie huo mkeka maana ni mrefu sana
 
Good explanation ila kwa nilipokua mimi kulikua na generator mkuu na sehemu nyingine hakukua na generator but still ilikua inawaka sababu ya hio battery umesema ambayo imeungwa nayo kutunza umeme, kwenye suala la conversion toka DC to AC mimi sijui chochote kuhusu hilo sababu mimi sio fundi umeme
Pamoja mkuu. Nimejitahidi kufafanua zaidi ili wengi wapate uelewa.
 
Mimi kwangu nilishawahi kuwasha kwa siku mbili wkt mgao ule wa umeme...yani asubui siwashi mpk saa moja usiku ndo nawasha.
Sasa kama ni hilo bateri sijui...
Ndio nenda kule control room check pale juu vizuri kuna battery ya kutunza umeme km sijakosea inakua kwa juu kidogo ya ule mtambo wetu wa kumpiga mwizi shoti na kumbabua ngozi
 
Pamoja mkuu. Nimejitahidi kufafanua zaidi ili wengi wapate uelewa.
Kuna siku ilibakia kidogo tu niziguse zile waya nikijua nimezima kumbe binti wa kazi alienda control room jioni akawasha maana ni muoga balaa sasa sijui nilikua napunguza majani ya mti ilibakia kidogo niguse nasikia usiguse hapo nimewasha kule
 
Tuliweka EF kwa sbb tuliingiliwa mchana kweupee tulikua tukitoka wanatuchora wanajua hakuna watu...siku hyo nimerudi mchana nakuta geti limefungwa kwa ndani nikaona mbona hii ni strange ndo kuita watu kuruka fance kukuta mlango umebomolewa na wameiba...
So tukaweka na camera kabisa...tukaunganisha kwenye simu zetu yangu na ya mr so hata tukiwa mikoani huko kuna muda unareview matukio...na tukiondoka mchana kama hakuna mtu tunaweka on umeme wa Fance....
 
Kuna siku ilibakia kidogo tu niziguse zile waya nikijua nimezima kumbe binti wa kazi alienda control room jioni akawasha maana ni muoga balaa sasa sijui nilikua napunguza majani ya mti ilibakia kidogo niguse nasikia usiguse hapo nimewasha kule
Ilitaka kunitokea juzi na mimi..yani nikajisemea hiii leo ndo ningeadhibiwa na mbwa niliemfuga mwenyewe...ni hatari sana hizi ni za kuwa nazo makini sana...inatakiwa kuwasha wtt wakishaingia ndani aisee...na kuzima mapemaa saa kumi na mbili au kumi na moja mkianza kujiandaa kutoka...
 
Yaan ukikosea hata wewe mwenyewe zinakuadhibu vibaya sana halafu zina umeme mkali hatari sana ule umeme unaobabua haufai kabisa
 
Yani jani la mti likigusa hizo nyaya...utasikia tiii tiii tii tiii tiii.. asubui unakuta limeungua hiyo sehemu...so kama hujui ukigusa huo mti...nadhani utajisikia uko Tanesco... 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Ila wezi wana mbinu sana
Hizo hapo labda atoboe ukuta akitoboa ukuta ndani anakutana na camera na camera ikidetect mtu tofauti sijui ni imetengenezwa mfumo wa AI zinamwamsha mwenye nyumba kwa alarm akiamka anakuchora tu kwenye big screen, ukiondoa hivyo nje kuna mimbwa km mitano ile mimbwa isiyokua na akili akiamiwa shika sio kwamba itatafuna matako tu ila itatafuna mpaka kikojoleo chako inakusubiri na mlinzi juu haya sasa mwizi pita hapo
 
Back
Top Bottom