Usalama wa Taifa: Mpo likizo?

Status
Not open for further replies.

Keil,

wewe jiandae na Popcorn na pepsi, yanayokuja ni makubwa zaidi ya kiwango cha kawaida cha Kikwete na wenzake hao wana usalama na TISS yao kufikiri.

Kikwete anasubiriwa tu kuitoa hiyo anayoita report ya BOT ili aumbuliwe big tyme.
 
Mjadala mzuri!!!

Angalizo tu!

Hoja ziko mbili, na nashauri zijadiliwe kama hoja mbili tofauti zisichanganywe! maana naona inaelekea wanabodi wanatafuta majibu ya hoja ya 2. kutoka kwenye hoja ya 1.

1. Hoja ya EPA account ndio tunaojadili kwa muda sasa. (Mwanzilishi wa hili ni Serikali yenyewe)

2. Hoja ya Deep Green Finance, Tanggold etc...(Mwanzilishi Dr. Slaa na Kambi ya Upinzani). Hili lakiko kwenye scope ya lile la kwanza, wala hakuna independent investigation, kama inafanyika ni ya vyombo vya dola ambavyo vinaripoti back to the government.
 

Kasheshe,

kiutendaji uko sahihi, kilichofanyika ni ukaguzi wa EPA. Kuna swali hapa liliulizwa na memba wa JF hapa. Kama wizi umefanyika kwenye nyumba yako, ukaamuka kufanya uchunguzi ukagundua kuwa fanicha zimeibwa toka living room, ukaenda chumba cha wageni ukagundua kuwa vitu vimeibwa, je si jukumu lako kwenda vyumba vyote vya watoto na ikiwezekana nyumba yote kujua kilichotokea?

Hapa mchezo wa maneno wanaoucheza na sisi tunaujua. Wanachojaribu hapa ni kuwachanganya wananchi wa kawaida wasijue kinachoendelea. Ona leo Kikwete anasema kuwa pesa zilizoibwa ni za watanzania na sio za wafadhili! what a shame!

Hapa ni kusukuma back kwao, wanataka tukubali tu na hayo majina waliyotoa huku wakiacha mapapa malafi na walinzi wao wa usalama wa taifa wakipeta tu na mashangingi ndani ya dar!
 

African Lady;
I love your persistence ! Ama kweli dada yangu king'anaganizi! humwachii mtu apumue ! Huyo ndugu yangu (kama yupo mpe pole) I can just imagine what he is going through🙂 ( with a light touch).

Your point of view accepted and keep up the good fight my girl; We are in this together for a very long haul!
 

Zalendohalisi,

Usijali kabisa kuhusu ninachofanya nikitoka kazini kwa sababu ndugu yako (kama yupo nitampa pole) anago through very good time in deed.

Sio kwamba nimeamua kuwa king'ang'anizi katika hili. Ukumbuke kuwa dosier ya Slaa ilitoka mwaka jana. Watu wakaanza kumkejeli kuwa amechemsha kwa kuhusisha TISS ya kibenki na ya kiusalama. Mimi nikawapa breki kwa sababu nilitaka nikusanye data zangu ili niwe kwenye nafasi nzuri ya kuelezea hili. Ukimuuliza Slaa na wote anaofanya nao kazi wanahakika kuwa TISS hapa imetumika kucover jamaa wanaodai kutunza usalama wa nchi yetu.

Muda umefika sasa hii issue iibuliwe upya. Kwa sasa ushahidi upo wa kutosha wa jinsi jamaa wa usalama wa taifa wanavyotumiwa kwenye mambo ya kifisadi. Waandishi wa habari wameomba wapewe copy ya report ya E&Y wamenyimwa kwa visingizio vya usalama wa taifa. I am sick and tired na hawa TISS na visingizio vyao rundo visivyo na msingi. I was very sickened na ile barua waliyomwandikia mzee wa kasungura na ndege ya kupaa ya richmonduli kumtaka azuie hoja ya Slaa bungeni.

Kama ni ung'ang'anizi, hawa jamaa ndio wamezidi na sasa ninarudisha the muziki back to them. Hii TISS iliyotumika hapa kwenye issue ya Tangold lazima ifunguliwe ili ijulikane aliyelipwa hapa ni nani. For now, uchunguzi na ushahidi mwingi uanaonyesha kuwa TISS ya usalama wa taifa imehusika hapa big time.

It is time to come out clean!
 
Zalendohalisi,

Usijali kabisa kuhusu ninachofanya nikitoka kazini kwa sababu ndugu yako (kama yupo nitampa pole) anago through very good time in deed.

Keep it up!

... Ukimuuliza Slaa na wote anaofanya nao kazi wanahakika kuwa TISS hapa imetumika kucover jamaa wanaodai kutunza usalama wa nchi yetu.

That's the point, wana abuse TISS kwa manufaa yao, and the guys can't do thing about it, poor fellows! Hapo nakubaliana nawe fika. Wanatumia bango la usalama wa taifa kuficha madhambi yao. Sawa na baba kikojozi anayemsingizia mtoto! Hata huku Bush ana abuse National Security tag kuficha mambo mengi tu, lakini isiwe sababu ya sisi kunyamaza, nakubaliana nawe.


Agreed na kwa hilo namwonea huruma sana JK kwa vile ana nafasi ya kuacha legacy hata zaidi ya JKN kama atatumia mwanya huu kuwatosa hao wenzake ( damu nzito), moreover everyone for themselves and God for all, asafishe uchafu huo na tuanze upya. Akilifnay hilo atakuwa amejiwekea retirement scene yenye amani na sifa kemkem. Lakini kama ulivyosema mara nyingi,sidhani anaelewa wala kuliona hilo.

... Hii TISS iliyotumika hapa kwenye issue ya Tangold lazima ifunguliwe ili ijulikane aliyelipwa hapa ni nani.
It is time to come out clean!

You can't say it better; huyo aliyepelekewa hizo pesa through TISS ni nani (of course ni CCM money laundering system na majina tunayo, wala siyo siri e.g Lotto Kitita, Amiko etc) kwa vile we have been duped (to quote Meghji). Na Salome Mbatia kafa na mengi tu kifuani, she knew it all.

(BTW I used kin'ganganizi in a positive way meaning insistence on make a point understood )
 
FISADIST hu the f****c r u to deserve her attention,
go to h***L,,If you cant them join them

BIG UP MWAFRICA WA KIKE

****USHINDI LAZIMA*****
 


Kalamu hiyo TISS ya benki tafsiri yake sahihi ni

TISS - Tanzania Inter-Bank Settlement System na wala sio Services kama huyo mchovu alivyosema hapo juu.


Kwa kuzingatia mabandiko hayo hapo juu thread hii ishapoteza maana na pengine tunajadili kitu kisichokuwepo!

Mie nshapoteza kompasi yangu sijui kaskazini wapi pls help....
 
ur right mamaaaa hapa lazima tujue huyu usalama wa taifa kila hela ya ufisadi kapelekewa yeye ni nani,,na anaishi wapi haiwezekani kila mtu anataja yeye,,lazima watujulishe,,,,tuombe mungu
 
Kwa kuzingatia mabandiko hayo hapo juu thread hii ishapoteza maana na pengine tunajadili kitu kisichokuwepo!

Mie nshapoteza kompasi yangu sijui kaskazini wapi pls help....

Masatu,

Hili la kupoteza kompasi ndilo walitaka waliotumia neno TISS kwenye malipo ya mwisho ya Tangold. Walicover na kutaka isijulikane kabisa nani amelipwa.

Waliofuatilia hili walipouliza, waliambiwa kuwa hili ni suala la usalama wa taifa (TISS) kwa hiyo wa-back off. Dr Slaa kwa kujua mchezo unaoendelea akaamua kuunganisha both literal and technical definitions ya TISS iliyotumika kwenye dosier yake.

Wasiojua kinachoendelea wakaanza kumkejeli kuwa amechemsha kuwa kutumia tafsiri ya moja kwa moja ya neno TISS kwa kulihusisha na usalama wa taifa. Walichosahau ni kuwa uchunguzi wa haya malipo ulikuwa unakwamishwa kwa visingizio kuwa the last payment ni ya usalama wa taifa (kitu ambacho kinawaweka TISS ya usalama kwenye spot).

Kwa hili, neno TISS likatumika twice, kwenye taratibu za kawaida za kibenki lakini pia kwenye kufunika wahusika halisi huku wakitajwa kuwa ni usalama wa taifa.

Mchezo wa maneno haya ndio utaendelea kutumika hapa mpaka hii TISS (ya taratibu za kibenki) na ile TISS (inayozuia uchunguzi hapa kwa vile haya malipo ni ya usalama wa taifa) viwekwe pamoja na wazi na kuwaibua wezi na mafisadi wanaotumia usalama wa taifa kujinufaisha!

the game has just started!
 

Kuna wakati nilitaka kumuamini JK kuwa angefanya kitu ila kadri siku zinavyoendelea ninapoteza kabisa matumaini na this guy.



Hili ndilo Dr Slaa alitaka litokee ila tu akakosa wabunge wengi na media ikamtosa. Shika bonge la bango kwa huyu kiumbe asiyejulikana anayejiita TISS ili atoe rangi zake zote wazi. Mpe majina yote anayotumia na kisha weka mpira upande wake ili afanye the first move. Tatizo tu mpiganaji akaachwa mwenyewe na mafisadi wakadhani wameshinda. The game is back. It is now Tanzanians vs TISS, sijui nani atashinda this round.


(BTW I used kin'ganganizi in a positive way meaning insistence on make a point understood )

usijali sana I usually dont take things personal here!
 
ur right mamaaaa hapa lazima tujue huyu usalama wa taifa kila hela ya ufisadi kapelekewa yeye ni nani,,na anaishi wapi

Pdidy unanikumbusha nyimbo ile ya Mmasi inayosema "Yiero mbona kosa yote kubwa ni ya jinai, huyo jinai ni nani, unaiba.. kosa ya nani .. jinai, unaua .. kosa ya nani .. jinai, unabaka ndito ya sule .. kosa ya nani .. jinai. Sasa naulisa hii jinai mbona yeye kosa yote ni yake au hatoi hela kidogo kwa polisi ndiyo maana kosa yoote imekuwa yake. Mwambie jinai achangamuke!

Ndiyo hayo ya Usalama Wa Taifa - hata Meghji inabidi aponee huko huko.
 
Mwafrika wa Kike:
I am absolutely flabbagasted by this male chauvenist ZalendoHalisi.

Kwa nini wewe MwK you have time with such a sick mind? Huoni anatafuta njia za kukusitisha kwa kukupaka matope?
Anaacha kuongelea mambo yanayohusika, yeye anaongelea MwK!

Usikatishwe tamaa na watu kama hawa, kwani unagusa maslahi yao hawa.
 


MWK,

Ushauri wangu kwa upinzani na kwa wanaharakati wote! twende step by step! Let reduce speed a little bit.

1. Tuache serikali ikamilishe hili la EPA ambalo si dogo! Wakishamaliza yaani miezi 5.5 ijayo tuwapongeze kama wakifanya vizuri au tuwahukumu wakiboranga.

2. Bila kujali kwamba wamefanya vizuri au Lah! wakati huo ukifika tuanze na hili la upande wa pili ...deep... deep.... Green ... Green...Tanga... Tengo.. mwana... Gold Gold ...etc.

Kwa nini nasema hivi, vyama vya upinzani vikiyalundika haya pamoja wananchi wataona kwamba Upinzani unalalamika tu wakati wanaona matendo ya serikali yako +ve
  1. Rais amemsimamisha Gavana!
  2. Rais ameunda task force
  3. Rais amesimamisha/freeze EPA account mpaka taratibu zingine zitungwe.
  4. Gavana Mpya anabadilisha uongozi wa Ndani wa Central Bank.
  5. Waziri ameteua au kubadili board members
  6. Task force iko kazini etc
  7. etc

3. Wananchi wetu hawana uwezo wa kupokea na kuchambua mambo mengi kwa pamoja, hapa JF wenyewe watu wanachanganyikiwa, je vijijini itakuwa je? Opposition wanaweza kukosa maximum gain wasipokuwa makini!
 

Kalamu,

Usijali kabisa na anachokifanya huyu kwa sababu so far vijembe vyake vinafunikwa na elimu nzuri anayoitoa. Kumbuka kuwa nimebishana sana na nafsi yangu kabla sijaweka hii thread hapa. Ninajaribu kuelewa frustration wanayopata watu kama Slaa kila mara wanvyojaribu kufuatilia mambo yanayopewa dubious names kama hili la TISS.

For now ninafurahia kuona elimu zalendo anayotoa kuliko vijembe
 

Kasheshe,

Kiutendaji nakubaliana nawewe katika hili na ningependa sana kufuata ushauri wako. Usiwe na wasiwasi kwa maana viongozi wa upinzani watafanya kile tu wanachoweza - kumbuka pia kuna alot of things kama Buzwagi, richmonduli, rada na kadhalika na yote yanahitaji attention.

Kwa sasa ninachofanya ni kuweka part yangu ya movement. Maelezo ya kujichanganya ya serikali kuhusu nini kimefanyika katika uchunguzi wa BOT ndiyo yanakatisha tamaa. Sasa hivi serikali inataka kusisitiza kuwa kilichochunguzwa ni EPA peke yake wakati watanzania wanategemea uchunguzi wa kina katika hili na yote yaliyofanyika BOT.

Mimi naona the best way ya kuyapatia ufumbuzi haya ni kuyaunganisha wakati moto bado upo ili yapatiwe ufumbuzi. Ukisubuiri miezi sita kuanzia saasa wasanii watakuambia kuwa uchunguzi wa benki kuu ulishakamilika na wahusika watashughulikiwa. Kutakuwa hakuna cha uchunguzi wa Deepgreen au Tangold na TISS yao!


Kwanza kabisa, ninachoelewa mimi ni kuwa Gavana amejiuzulu na ushahidi upo ila Kikwete anajikosha kuwa amemsimamisha kazi. Hayo mengine ukifuatilia kwa makini utaona ni longolongo la task force ya kuchunguza kamati ya uchunguzi ya kampuni ya uchunguzi ambayo inachunguza kilichochunguzwa na maofisa wachunguzi walio kuwa nakazi ya kuchunguza..........

3. Wananchi wetu hawana uwezo wa kupokea na kuchambua mambo mengi kwa pamoja, hapa JF wenyewe watu wanachanganyikiwa, je vijijini itakuwa je? Opposition wanaweza kukosa maximum gain wasipokuwa makini!

Ndugu yangu,

tatizo hapa sio maximum gain ya upinzani. Tatizo hapa ni maximum gain ya watanzania bila kujali upinzani utapata nini. Mambo mengine yanaangalia na inabidi yaangaliwe kitanzania zaidi ya kuyaangalia kisiasa.
 

Hilo la TRA ni jingine tutalivalia njuga, nakuomba MH uanzishe Thread yake wenye nondo, mawe na moto wa Gas Songosongo wapo hapa wamejaa tele.

Lakini kwa kipande ya Muda huu tuongelee BOT Kihenge Chetu.
 
..ndio zama za uwazi na ukweli hizi!zikisaidiwa na kasi,ari na nguvu mpya!

..ukitunga nyimbo iwe nzuri,itatumika kukusindikiza kaburini!

..asaalam aleykhum!
 
Fisadi kama kweli wewe ni Mkatoliki na ulikuwa na wakatoliki Bostona no wonders umetoka maana una akili kama za hao TISS.Shame on you kuja hapa na kutaka kutueleza Mwafrika wa Kike anakaa wapi .Hatuhitaji hilo ila issue za kuokoa mali za Tanzania .
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…