Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
....Pamoja na kukubali ukweli juu ya mapungufu yaliyoelezwa ni vizuri pia tukumbuke kuwa yapo mazuri mengi tu yaliyofanywa na Idara hiyo. Kwa msingi huo kukihukumu chombo hicho kuwa hakifai, kimeshindwa kufanya kazi yake ni hoja ambayo inahitaji kutazamwa kwa mapana zaidi.....
Malaika (Ibilisi) alifanya dhambi moja tu! (kwa mujibu wa Bible) na dhambi hiyo ilimfanya aadhibiwe milele. Endapo watu au Idara ambayo tunaiamini kuwa inafanya kazi ya kimalaika isiyo na shaka yoyote ikatuhumiwa kuwa kuna ushiriki wa kulitafuna Taifa letu dawa ya taasisi hiyo ni kuifinyanga upya ili kiwe kitu kisafi. We Tanzanian tuna haki ya kuzungumzia ustawi wa nchi yetu kama katiba inavyoelekeza. Iwapo nchi inatafunwa na watu tuliowapa dhamana halafu TISS ipo kuwalinda ili wale vizuri basi siona maana ya kile kiapo wanachokitoa, au tuseme wanaapa kwa viongozi hawa na hawaapi kwa nchi??
Rev> Kishoka
Umeleta hoja mwafaka na ni kweli kwamba kuna mazuri yaliyofanyika na TISS ila ni wajibu wao kufanya hayo mazuri maana haikuundwa ili ifanye mabaya. Ni aibu kwa nchi inayotaka kupiga hatua za maendeleo halafu juhudi hizo zisiungwe mkono na wananchi kwa jumla (ikiwemo idara zote za dola). Kitendo cha kuitisha JF kuwa inaleta uchochezi kwa kusema ukweli basi maana ya uundwaji wa Taasisi ya Usalama wa Taifa inakuwa haipo. Ni bora wataalam wakakaa chini na kuchakatua what we need kwani vita baridi imekuwa MOTO sasa, China inakuja juu kiuchumi kwa bidhaa feki, Fursa mbalimbali za kiuchumi hazitakuwa na maana pasipokuwa na angalizo kutoka kwa Taasisi nyeti yenye nia chanya kwa taifa. Wasomi tunaowalipia kodi zetu wanafisadika kila kukicha kwa kuwa Taasisi za serikali zimelala. Leo hii sio sawa na zile nyakati za ubaguzi na vuguvugu la ukombozi. Tuliowasaidia ukombozi wa nchi zao hakuna la maana wanalofikiria juu yetu zaidi y kutuibia (kiujanja) rasilimali zetu. Hivyo ni muda mzuri kwa mamlaka husika kufikiria how does TAASISIZ za dola zitakuwa formed na kutekeleza majukumu yake.
Hivyo Mzee wa Busara, ni haki sisi WALIPA KODI kuhoji uhalali wa taasisi hizi endapo zinafanya kazi kinyume na matarajio yetu. au wenzetu wanalipwa kwa pesa za misaada? Tusipotoa Kodi wajue watashindwa kuoperate, Ni budi wakafanyia kazi taarifa tunazozitoa badala ya kututishia kwa kutukamatakamata na kufungua mashtaka-kivuli.
Bravo Rev. Kishoka, naunga mkono Hoja