Usalama wa Taifa saidieni kumpa Rais Samia taarifa sahihi

Usalama wa Taifa saidieni kumpa Rais Samia taarifa sahihi

F4B

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2022
Posts
336
Reaction score
429
Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza hapo juu. Ninaomba usalama wa Taifa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa mpeni Rais taarifa sahihi ili afanye maamuzi sahihi.

Kama nyinyi mnampa taarifa sahihi ila yeye hachukui hatua? hilo ni swala jingine.
Kwenye hili swala la sensa na makazi ya mwaka 2022 sitaki kuamini kuwa nyinyi hamjui yanayoendelea ngazi za chini hasa taarifa za unyanyasaji unaofanywa na mamlaka za ngazi ya wilaya.

Kwa mfano Kuna halmshauri za wilaya hazijalipa makarani na watu wote hadi Leo je Maafisa usalama wa wilaya na mkoa wamechukua hatua gani kuripoti kadhia hii kwa mamlaka husika ?? ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika.

Serikali Inatumia mabilion ya fedha katika swala hili iweje mtu alihujumu zoezi kwa kutowalipa.

Kuanzia Jana makarani walipaswa wahudhurie mikutano kwa ajili ya kutoa elimu ya sensa 2022.Lakini baadhi ya wilaya hata vifaa hawajapewa.

Narudia kutoa wito usalama wa Taifa msaidieni mhe Rais kwa kumpa taarifa sahihi ili kazi yake iwe nyepesi
 
IMG_20220103_071415 (1).jpg
IMG_20220103_071415 (1).jpg
 
Watu huwa wanaona kila kitu dili, unawezaje kula posho za makarani au unapangaje kuwazulumu posho zao.
 
Nikajua jambo kuubwa kumbe ni kulipa makalani 😄😄😄😄..

MakaRani watalipwa ila wawe wazalendo, kazi kwanza malipo baadae..
 
TISS Kitengo cha Economic Intelligence kiko mahututi
 
Back
Top Bottom