Usalama wa Taifa saidieni kumpa Rais Samia taarifa sahihi

Usalama wa Taifa saidieni kumpa Rais Samia taarifa sahihi

Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza hapo juu.Ninaomba usalama wa Taifa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa mpeni mhe Rais taarifa sahihi ili afanye maamuzi sahihi.Kama nyinyi mnampa taarifa sahihi ila yeye hachukui hatua? hilo ni swala jingine.
Kwenye hili swala la sensa na makazi ya mwaka 2022 sitaki kuamini kuwa nyinyi hamjui yanayoendelea ngazi za chini hasa taarifa za unyanyasaji unaofanywa na mamlaka za ngazi ya wilaya. Kwa mfano Kuna halmshauri za wilaya hazijalipa makarani na watu wote hadi Leo je Maafisa usalama wa wilaya na mkoa wamechukua hatua gani kuripoti kadhia hii kwa mamlaka husika ?? ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika.
Serikali Inatumia mabilion ya fedha katika swala hili iweje mtu alihujumu zoezi kwa kutowalipa.
Kuanzia Jana makarani walipaswa wahudhurie mikutano kwa ajili ya kutoa elimu ya sensa 2022.Lakini baadhi ya wilaya hata vifaa hawajapewa.Narudia kutoa wito usalama wa Taifa msaidieni mhe Rais kwa kumpa taarifa sahihi ili kazi yake iwe nyepesi
Ni uzembe wa wakurugenzi wa halmashauri. Nadhani Mh Rais kama ana mkeka wa ma DED, DC Ndiyo wakati muafaka wa kuwapima, maana serikali ilishatuma hela zote kitambo ila hawa wakurugenzi wapo wapo tu na hizo hela watu mpaka wanafanya migomo ya kazi. Ila Mh. Rais ana kazi sana maana kila sehemu anahujumiwa kisa ni mpole.
 
TISS Kitengo cha Economic Intelligence kiko mahututi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Uyu mother na yee ni mchawi tuu .anajua kila kitu tuache kumuona mwema sana amna mtu palee
 
Kumbe hadi kwenye sensa!nilijua ni ajira mpya tu ambapo mtu unatumia nauli yako kutoka huko hadi halmashauli kulipoti lakini hakuna cha pesa ya kujikimu pia mshahara hupati,yani unaishi kiyatima mpaka basi
Kweli Mwigulu ameshindwa kuelekeza pesa sehemu husika.hivi mtu umemwajiri na ana familia hata pesa ya kujikimu hakuna achilia mbali mshahara! ama kweli kuwa uyaone!
 
Tatizo ungezitaja hizo wilaya siyo unakuja Happ kulialia huku taja wilaya wakuu na wakurugenzi wake wapo humu humu watapitia na kutoa ufafanuzi Ni hofu gani unapata ikiwa ujatukana mtu Wal kudhalilisha taja wilaya tuko hapa ss wakurugenzi tuko hapa kukuzikiliza[emoji3]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Vijana wa Bongo mnakwama wapi? Mnasubiri kufanyiwa kila kitu? Amkeni teteeni haki zenu. Viongozi wanajua uoga wenu ndiyo maana hawajali. Mnachonga vijago halafu vinawatisha?
Ukiwaeleza ukweli huu wanakua wakali, uzuzu,uoga,unafiki na middle class kujifanya wapo mbali na reality on the ground, working class ndio centre ya kuleta msukumo pamoja na wanafunzi, kwetu hapa kila siku kulalama na viajira uchwara hivi kwenye keyboard humu, kuna tatizo kwenye idara yako pigana, sio kukimbilia JF
 
Kama kichwa Cha habari kinavyojieleza hapo juu. Ninaomba usalama wa Taifa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa mpeni Rais taarifa sahihi ili afanye maamuzi sahihi.

Kama nyinyi mnampa taarifa sahihi ila yeye hachukui hatua? hilo ni swala jingine.
Kwenye hili swala la sensa na makazi ya mwaka 2022 sitaki kuamini kuwa nyinyi hamjui yanayoendelea ngazi za chini hasa taarifa za unyanyasaji unaofanywa na mamlaka za ngazi ya wilaya.

Kwa mfano Kuna halmshauri za wilaya hazijalipa makarani na watu wote hadi Leo je Maafisa usalama wa wilaya na mkoa wamechukua hatua gani kuripoti kadhia hii kwa mamlaka husika ?? ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika.

Serikali Inatumia mabilion ya fedha katika swala hili iweje mtu alihujumu zoezi kwa kutowalipa.

Kuanzia Jana makarani walipaswa wahudhurie mikutano kwa ajili ya kutoa elimu ya sensa 2022.Lakini baadhi ya wilaya hata vifaa hawajapewa.

Narudia kutoa wito usalama wa Taifa msaidieni mhe Rais kwa kumpa taarifa sahihi ili kazi yake iwe nyepesi
Nina mashaka na IQ za watumishi wa idara ya usalama wa Taifa wa Tanzania.
Pengine kigezo kikubwa cha kuwapata ni kadi ya CCM?.
Haiwezekani mtu anatoa rushwa ili apate ajira ya sensa,na nyie idara ya usalama wa Taifa mpo mpo tu.
You're useless.
 
Nina mashaka na IQ za watumishi wa idara ya usalama wa Taifa wa Tanzania.
Pengine kigezo kikubwa cha kuwapata ni kadi ya CCM?.
Haiwezekani mtu anatoa rushwa ili apate ajira ya sensa,na nyie idara ya usalama wa Taifa mpo mpo tu.
You're useless.

Kazi kubwa ya usalama wa taifa ni kuhakikisha CCM haitoki madarakani kwa njia yoyote ile.
 
Ningekuwa mimi. Kuhusu sensa. Ningewafundisha mabalozi aunwajumbe w nyumba kumi wote Tanzania hatua muhimu za kuchukua siku ya sensa. Pili, ningewafundisha wenyeviti wa mitaa na vitongoji hatua hizo hizo.
Hao ndio watu wanaoujua nyumba zote Tamzania nzima.
Ningetayarisha dodoso la.sensa na kulisambaza kwa viongozi hao mapema kabisa likiwa limefungwa lakiri. Seal. Ningewaelekeza siku ya kufungua dodoso hilo iwe siku moja kabla ya 23.8.2023. Na kuwapa mabalozi.
Siku ya sensa. Mabalozi wangegawa madodoso ili familia zote zitajaze. Wale wasiojua kusoma na kuandika wangesaidiwa na majirani. Walioko safarini na kazini wangepelekewa madodoso na viongozi makazini.
Jioni madodoso yangekusanywa na mabalozi na kuyapeleka kwa wenyeviti wa mitaa.
Hapo karaninwa sensa angekaa na kuyajaza kwenye kiskwambi chake na kutuma taarifa.

Kwa utaratibu wa sasa. Kuna nyumba hazitafikiwa, pia kuna sehemu hazina mtandao.
 
Ndugu Watanzania wenzangu zoezi la sensa ni muhimu sana kwa serikali ili ipate takwimu sahihi kwa ajili ya kuiwezesha kupanga MAENDELEO ya nchi yetu.Si hivyo tu lkn serikali Inatumia mabilioni ya shilingi ya walipa Kodi wa nchi hii kugharimia zoezi hili.Kama michakato ya kuwapata makarani ilijaa ubabaishaji na mafunzo ya makarani nayo yamejaa ubabaishaji je takwimu zitakazo kusanywa zitakuwa sahihi.Hofu yangu ni kuwa serikali inaweza pata takwimu zisizo sahihi maana kitovu Cha sensa ni makarani ambao Kila kukicha hawapewi stahiki zao. Kuna jamaa yangu sehemu anasema Jana waliitwa wakashindishwa njaa hebu fikilia hili.Sasa najiuliza Mkoa huo hauna usalama wa Taifa wa kuripoti haya sehemu husika ili yapate ufumbuzi.Mwisho nitoe wito kwa makarani wa sensa wakafanye kazi hii kwa kutanguliza Uzalendo kwa taifa lao japo wametendewa sivyo ndivyo maeneo mengi ya nchi mfano kule Moshi.
 
Kwamba hata wewe unajua hayo madudu alafu yeye hajui ?!!!!

Sasa si bora tukupe hata wewe nchi....
 
Mkuu sijui kushika hata bastora ila ninataarifa hizi sahihi kutoka Kilimanjaro, Tabora, Mara na Kwingineko.Halfu tuna mtu analipwa kwa kazi hiyo ila hana taarifa
Kwamba hata wewe unajua hayo madudu alafu yeye hajui ?!!!!

Sasa si bora tukupe hata wewe nchi....
 
Back
Top Bottom