Mkuu wa idara ya usalama wataifa amejitokeza leo na kukanusha tuhuma zilizotolewa jana na Dr.Slaa kuhusiana na tuhuma za idara hiyo kushiriki katika zowezi la wizi wa kura za urais. Akizungumza na TBC leo Mchana kwenye taarifa ya habari Mkuu wa idara hiyo amesema
"Dr.Slaa ameingizwa mjini na na watu waliyo jifanya ni usalama wataifa,hakuna kitu kama hicho, sisi hatuna chama, tupo kwajili ya taifa na siyo chama chochote. Na mtuka kama anaushaidi ajitokeze na auweke wazi.. Najua ameingizwa mjini na na watu waliyo jifanya ni usalama wa taifa ambao sisi hatuwatambui."
Style hii aliyo tumia mkuu wa idara hii ni style inayotumiwa na Russia kuwakana watu waliyo tumwa kufanya kazi na atimaye kuboronga na kukamatwa au kugundulika, Njia hii inatumika kujisafisha...
Nakumbuka mwaka 1978 Mzee wangu alitumwa kwenda kufanya upelelezi nchini Uganda akiwa na wenzie 8, waligundulika na kukamatwa Na serikali iliwakana na kusema haiwatambui na haijawatuma bali walikuwa na mambo yao binafsi...
Na muomba Dr.Slaa asikatishwe tamaa na majibu haya bali akusanye ushaidi na kuutoa hadharani ili kuwaumbua hawa wote..