Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Duh,hakuna aibu kama kubambwa kwa ushahidi😇
 
Extrovert na BRAZA CHOGO hawaendani kabisa,hv ilikuwaje wakafahamiana

Extrovert ni moja ya id ambayo huwa naiheshimu sana humu jf
Sijajua mkuu.....

Lakini huyo braza chogo naona she's joking more....

Lakini kwenye mada serious naona anakuwa serious

Lakini sidhani kama anafanya alichokiandka hapo juu...
 
Inaendelea No 7,

Kipenzi changu akaniuliza kwa upole kabisa, "babe, naomba ufafanuzi juu ya zile voice please" nilikua naangalia chini sikuweza kumuangalia usoni, nikawa nawaza naanzia juu au katikati?

Naomba niwape dondoo chache kuhusu mpenzi wangu, kwanza ni mpole sanaaa, mstaarabu, ana heshima kwa kila mtu, ni mtu fulani anapenda amani muda wote, hua anakasirika sometimes ila hua haweki hasira kwa muda mrefu, mimi ikitokea nimemuudhi hua haongei sana adhabu yangu naikuta kitandani 🙈,
Niseme ukweli wakati tunaanzana mwaka 2015 mimi nilikua bado barobaro yaani ujana mwingi kila sketi nataka niifunue nione yaliyomo yamoooo!? halafu sikai sana yaani tukidate mwezi mmoja wewe umekaa sana,🤫
Wakati nakutana nae yeye hakua na mambo mengi yaan exs zake walikua wawili tu, kiukweli alipambana sana kunituliza, amenizidi miaka mitano siku zote alikua ananiona mtoto ipo siku nitakua na nitaacha (na kweli nimeacha na tunalea mtoto) anavuna matunda ya uvumilivu,

Kipindi chote nipo na yeye sijawahi kuona wala kuhisi kua ananisaliti, katika vitu ambavyo ninamkubali hicho ni kimoja wapo, pia mwenzangu huyu ni mtu yupo focused sana na maisha, mpambanaji asiyekubali kushindwa kwa umri wake wa miaka 35 amefanikisha vingi ambavyo kijana yoyote angetamani kua navyo,
That's my baby sichoki kumuelezea, niko nae proud sana😘🥰

Haya turudi kwenye kikao chetu sasa, nikamfungukia japo sio story nzima nilimwambia tu nilikutana nae kwenye event ya Znz akaniomba tushee room nikamkubalia usiku ndio vile ila kulivyokucha kila mtu aliendelea na mambo yake ajabu kaniganda hadi leo wakati ilikua a one night stand, akaniuliza kwenye voice ulisema "sometimes i miss US" ulimaanisha mlichofanya kiliwakolea, hapo nikaruka nikamwambia "no babe kwanza hata sikumbuki, nilimwambia vile tu kumfanya ajisikie vizuri na sio kingine" nikaongeza "shauri lake lipo polisi alishaitwa akaonywa na sasa nataka nimpeleke tena" akashtuka kusikia habari za polisi akaniuliza ilikuaje nikaeleza matusi na vitisho alivyokua anatuma, alivyokua anaweka nguo za damu getini, alivyomtrick cuzo kupata namba yako, aisee alikasirika sana akasema sasa mimi nitadeal nae tulia, yeye atachagua aende jela au milembe hospital, akanambia nijiandae twende polisi uzuri alishawahi kukiri kwa maandishi kukaa mbali na mimi na sasa anarudia na meseji zipo, safari ya polisi ikawadia, tulisikilizwa wakasema huyu safari hii tukimuita haji, huyu ni kwenda kumkamata tu, ishu ikawa atakua wapi basi nikaambiwa nimpigie nijifanye kama nataka tuonane haraka nina shida, nilipiga sana bila kupokelewa akatuma meseji yupo darasani, nikamjibu akitoka anicheki nimechanganyikiwa nahitaji msaada wake, nahisi pindi lilikua halipandi kwani baada ya dakika 15 akanicall na kuniuliza nini mbaya, nikamwambia mambo ya kazini kuna mahesabu hayaendi sawa nikajifanya kama nalia, akaniuliza nilipo nikamuelekeza akasema anakuja chap, tukapewa askari mmoja na mgambo tukaenda hadi sehemu husika kumsubiri kweli akaja alionekana yupo so worried hapo hapo wakamkamata, nakumbuka alivyokua anapiga kelele za niacheni niacheni, alivyokua anaita jina langu na kuniuliza kwanini namfanyia vile, nilijisikia vibaya sana, nilimuomba atulie hao ni askari anaenda kituoni tu, aliendelea kupiga kelele huku akisema ananichukia, ataniua, sikuweza kupanda gari lile mimi nilichukua bajaji nakuwafata kituoni, nilikuta ameshawekwa selo lakini alikua anaongea na kupiga kelele, alikua anamtukana babe wangu, nakumbuka askari mmoja wa kike alienda akamzaba makofi na kumuamuru anyamaze ni kama alichochea moto ndio alizidi kupiga kelele, aliruka ruka alisema akitoka hapo wote atawaua na yeye atajiua, polisi walitaka familia yake ijue kua yupo pale, akaombwa namba ya mtu wake wa karibu akawa hataki kutoa anaongea vitu havieleweki, nikakumbuka kuna namba iliwahi kunicheki whatsapp huyo mtu alijitambulisha kama rafiki yake, nikaikuta na kuipiga, uzuri iliita na akapokea nikajitambulisha kwake na kumwambia Lily amekamatwa awasiliane na familia yake kituo flani waje wamtoe hayupo sawa, baada ya muda simu zikaanza kuita kwangu, alikua ni dada ake akanihoji hoji nikamwambia sina maelezo zaidi njoeni mumtoe humo na mumpeleke hospital kitengo cha magonjwa ya akili, akasema wanakuja.....

Itaendelea

Leejay49 , Lamomy , Joannah ,
ephen_ , Dejane , Demi , realMamy

Na wengine wooooooooooote
 
Inaendelea No 8,
Baada ya nusu saa ya kelele na matusi hatimae Lily akatulia, tukaitwa ofisi ya askari, katika maongezi akasema huyu dawa za kulevya zimemuathiri aende sober house, nikamwambia inawezekana maana anavuta sana bangi na stress na bangi haviendani, akasema kumuweka hapa ni kumuongezea tatizo anahitaji msaada wa akili, nikamwambia familia yake inakuja tafadhali waelezee hayo maana kwa alipofikia anaweza kweli akaua mtu au akajiua yeye, hata babe wangu kwa hali aliyoiona alikubaliana na sisi hakua na pingamizi,
Askari akaamuru Lily atolewe selo akaletwa kwenye ofisi tuliyokuwepo, alipotuona alituangalia kwa jicho la chuki na hasira kali akakaa na kuanza kuhojiwa akawa hajibu kitu analia tu, baadae tukajulishwa familia yake imekuja, wakaingizwa ofisini alikua dada ake mkubwa na mume wake, dada ake waliofatana kuzaliwa na shangazi yao, dada zake wakaanza kulia kumbe walikua hawajamuona siku nyingi yaan Lily tangu abadilike tabia na muonekano wake alikaa mbali na familia yake walikua wanawasiliana nae kwa simu tu, alikua amekonda, amepoteza nuru, na ile style ya nywele, zile tattoos alionekana wazi anapitia kipindi kigumu,

Askari akawaeleza kinachoendelea na akatoa wazo lake la kupelekwa sober house na mimi nikasema au hospital kitengo cha akili, Lily alikurupuka "mimi sio chiziiii, niacheni niondoke mimi sio kichaa" kila mtu akaona hapa kazi ipo,
Familia yake wakajitahidi sana kumtuliza hadi akatulia, wakamalizana na mambo ya polisi si unajua kuingia bure kutoka na cash,😀
Wakampandisha kwenye gari na kuondoka, na sie tukawashukuru maafande pale, ofcourse mkono mtupu haulambwi 😊 tukaondoka,
Ilikua ni siku ndefu na ngumu tukaimalizia beach,

Tukiwa beach nikamuomba msamaha mpenzi wangu kwa ujinga nilioufanya nilimuahidi kutulia na yaliyotokea hayatajirudia tena, akanisamehe kwa moyo mkunjufu kabisa akanambia tuangalie yajayo, tukagonga cheers 🥂

Mara nikapokea simu kutoka hospital, vipimo viko tayari niende tu na donor kwa ajili ya process zinazofata, tulifurahi sana ilikua a night to remember (wakubwa mshaelewa 😋)

Itaendelea
 
Usituweke sasa
 
Imenoga😃
 
Sijajua mkuu.....

Lakini huyo braza chogo naona she's joking more....

Lakini kwenye mada serious naona anakuwa serious

Lakini sidhani kama anafanya alichokiandka hapo juu...
Hata mim nimeshamshutkia,huenda analipwa na mabeberu kufanya hyo mizaha
 
Goma linaendelea kutambaa, hiyo episode ya 7 na 8 ya moto 😍😍😍

Yani kila saa nachungulia km nimeinjika kuku 😹😹😹 dr puliizzz endelea kabla wachawi hawajamaliza kikao cha kuanza kuripoti uzi ufutwe..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…