Inaendelea, SEHEMU YA MWISHO
Siku iliyofata mimi, babe wangu na donor wetu, habari za kutafuta donor nilizileta humu, nilirushiwa mishale sana ila sikujali wala nini, baadae nikapata mtu muelewa, tukaenda hospital na kupata vipimo vyote, kuna ka mzunguko sio mchezo, hiyo siku tuliambiwa wote tuko fresh na tulifanya zoezi la upandikizaji, (sitaiongelea hii ng'o)
Tulisubiri hadi wiki nne nikapima ikawa imoo 🥳, kuna wengine hupima in two weeks ni wewe tu na uharaka wako,
Back to Lily, familia ilifata ushauri wakampeleka sober house mkoa flan bangi na pombe zilimuathiri waswahili tunasema vilimkataa, alikaa kwa miezi mingi, nakumbuka siku hiyo nipo job naendelea na majukumu yangu ikaingia namba ngeni kupokea ni yeye aisee nilihisi kuzimia, nikakata simu, akapiga tena sikupokea akaandika meseji ndeeeeefu ya kuomba msamaha na kudai amebadilika amekua mtu mwema, blah blah, sikumuamini tena nikablock ile namba nikatulia, akaendelea kupiga na kutuma meseji akisisitiza anahitaji msamaha wangu ili aishi kwa amani,
Nilivyorudi home nikamuonesha babe akasema mjibu kua umemsamehe ili abaki na amani zake asikusumbue, nikawaza sana nikaona fresh tu, nikamjibu kua nimemsamehe abaki na amani ila asinitafute tena na namba yangu aifute hadi akilini akajibu kwa kushukuru hakunitafuta tena,
Turudi nyuma nilivyopata ujauzito babe akasema sasa inatosha kazi za mbali, tumejitafuta tumejipata anahitaji kua karibu na familia yake, akamalizia mkataba wake hakuongeza tena akarudi nyumbani, alikuwepo siku tunampokea mtoto wenu duniani awww🥰
Lily alikuja kusikia nina mtoto akanitafuta bila kupokea simu zake siku hiyo akajitoa ufahamu na kuja tulipokua tunaishi akaambiwa tulishahama kitambo, akatuma meseji eti ana zawadi za mtoto atajisikia vizuri kama akimuona na kumpatia, wala sikumjibu, tangu hapo mpaka jana Lily hajawahi kuacha kunipigia simu nakutuma meseji anajua japo nimemblock lakini naziona huenda siku moja nitakuja kumjibu, uzuri kwenye makazi yetu ya sasa hapajui angekua kishafika,
Najua wengine mtasema why nisibadilishe namba ya simu, hii namba ni ya miaka mingi na ipo kwenye vitu vingi kuipoteza ni kuanza moja,
Siwezi kuusahau ule mwaka 2020, mwaka ambao nilikutana na psycho, laiti kama siku zingerudi nyuma kwa hakika ningerudi na kurekebisha hilo kosa, namshukuru Mungu kwa kunipa mtu muelewa kwenye maisha yangu, angeniacha pengine na mimi ningekua kama Lily🥺 (Lord forbid),
Funzo kwa wote mtulie kwenye mahusiano yenu, kuonja onja ndio hayo mnaonja na vyenye sumu,
Nawashukuru kwa muda wenu
MWISHO.