Usaliti wa kisiasa: Ukraine wameuona zaidi kuliko pengine

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Kwenye kampeni ya kuomba kuchaguliwa kuwa rais Zelensky alisema hivi:

“Our first priority is a ceasefire [in Kiev’s war with the Donbass]…I would not hesitate to lose my position for the sake of peace.”

Yaani "Kipaumbele chetu cha kwanza ni kusitisha vita (kati ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa majimbo ya Donbass yaliyojitenga). Sitajali kupoteza nafasi yangu kwa ajili ya kusaka amani"

Mara baada ya kuupata urais, Zelensky aliachana na ahadi yake na kuwasaliti watu wake watumike kutekeleza mpango wa Marekani kuidhoofisha Urusi!! Ili kufanikisha. lengo hilo Ukraine ilitiwa kiburi kuwa iendelee kuyashambulia majimbo yaliyojitenga kwa kuahidiwa kuingizwa NATO.

Ikadanganywa kwamba lazima itaogopa kupambana na NATO. Lakini Marekani ilijua kabisa kuwa Urusi haitaweza kuvumilia lazima itaingia vitani. Ndiyo lengo la Marekani, kupigana na Urusi kwa kutumia mikono na damu ya wa-ukraine. Zelensky kawasaliti watu wake!

A president elected on a promise to bring peace is offering his people as cannon fodder for external powers who are using them to fight a proxy war!

Marekani haikuweza kufikiria kuwa Urusi itaweza kuhimili kupigana vita huku ikikabiliwa na vikwazo lukuki vya kiuchumi!! Mpaka kufikia hapa Marekani inajua kabisa kuwa ilikosea mahesabu na mwisho wa siku watamgeuka Zelensky na kumfanya mbuzi wa kafara!!
 
Mantiki ya ajabu sana hii. Hakuna kiongozi duniani anayechaguliwa kuwa Rais wa nchi kwa mategemeo kwamba ataleta amani kwa kugawa sehemu ya nchi yake kwa taifa jingine linalowaletea chokochoko.

Yaani kama vile Idd Amin alivyodai eneo la Kagera kuwa sehemu ya Uganda kisha kuvamia kijeshi na kumuua Mkuu wa Mkoa basi Nyerere angeachia tu kwa ajili ya amani! That would've been stupidity of the highest order. Hata kama mleta mada ni sadist mwenye kutamani Urusi iikalie na kuiangamiza Ukraine kimabavu basi angalau uelewe mantiki ya uongozi wa taifa ikoje. Sio kienyeji hivyo. Hii vita itapigwa hadi hitimisho hata kama ni hadi mwisho wa dunia.

Watu wakorofi hawatulizwi kwa kuachiwa wanachopora. Never! Ukiwaachia kidole, watataka mkono mzima kisha mwili wote hadi kichwa chako. Walianza Crimea, wakaachiwa, wakaja Donbas kisha wakaamua kuchukua Kyiv na Ukraine yote kwa masaa 24 na vitisho kibao. Eti special operation: kabidhini kila kitu kwa maafisa wa Urusi mrudi makwenu mkajifungie! Hapo kila mtu akashtuka. Wakapelekewa moto wa uhakika wakasambaratika. Sasa wanapambana na adabu tele. Acha zipigwe tu, hakuna namna.
 
Ni
Wewe unaongelea Vita ya 2022. This thing has been building for almost a decade + the sovereignity ya Ukraine na Tz are incomparable. These have been nchi moja in the past. Ukraine has Russians and not vice versa. Hivyo ina interests huko. Don't forget the CIA staged coup
 
Sasa kwa nini Tz ilivuka mipaka . Si wangeishia Mutukula?
 
Watu wenye ufahamu mdogo wanaamini aliyevamia ndio mkosaji vilevile hata Uganda ndio maana vyomba vya dunia vilikaa kimya pamoja na AU wakati kambarage anapiga kelele
 
Vita ya 2022? Huna habari na 2014? In any case, unatamani Rais wa Ukraine angesalimu amri mara baada ya uwanja wa ndege na air force ya Ukraine kubomolewa na ule msafara wa vifaru vya Warusi wa kilometer kadhaa kufika nje ya Kyiv 2022? Kisha Putin kutoa amri wajisalimishe kwa majeshi ya Urusi mara moja? Do you live in a dreamworld; sort of utopia?

Halafu, unadai Ukraine na Urusi ni nchi moja in the past? Unafahamu historia na demography ya nchi zote za Ulaya? Unafahamu demography ya USA? Tunajadili nini hapa? Hivi umewahi kusoma na kuelewa historia ya continental Europe? This is utter wastage of time!
 
Sasa kwa nini Tz ilivuka mipaka . Si wangeishia Mutukula?
Sijui elimu wala taaluma yako. Najua utakuwa bado mdogo sana. Nashauri hilo swali lichukue kama homework yako kalifanyie kazi upate jibu. Linaweza kukusaidia hata kuelewa hoja potofu Urusi wanayoitumia kuvamia Ukraine. Zinafanana kwa kiasi fulani. Ingawa ya Tanzania ilikuwa na mashiko.
 
amna cha time will tell kuanzia leo na kuendelea kaa ukijua hakutakuwa na nchi inaitwa ukarine tena inamegwa mdogo mdogo ....afu inakuwa sehehem ya urusi....sawa bwasheee..

Ukraine itaendelea kuwepo, ila tofauti na nyuma hawato vamiwa kirahisi tena, hili ni funzo kubwa kwao
 
Pole sana
 

Shida unasoma bila kutafakari ndo maana unajibu off context
 
Sasa ulivo na akili finyu hivi, unahoji elimu au taaluma ya watu, wewe ni mjinga na hakuna unacho kielewa humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…