Usaliti wa maisha, una sura nyingi sana 😢

Usaliti wa maisha, una sura nyingi sana 😢

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Shoka lilipoenda msituni kukata kuni, miti ilisema kwa huzuni "mpini ni mwenzetu."

Samaki aligundua hana urafiki na maji, pale yalipotumika kumpikia.

Jogoo aliyewaamsha wenyeji, alichinjwa walipokuja wageni.

Mbwa aliyelinda nyumba usiku kucha, alifungwa bandani mchana ili asiingie sebuleni.

Kipofu alipopata bahati ya kuona, cha kwanza alichotupa ni fimbo yake iliyokuwa ikimuongoza.

Njiwa aliyebeba barua ya amani, alipigwa mawe kwa kudhaniwa ni mwindaji.

Mti uliotoa kivuli cha mapumziko, ulipunguzwa matawi kwa kuni za jioni.

Nuru ya taa ilipowezesha safari, walipoiona alfajiri, waliizima kwa mateke.
 
Yesu alikuja kuwaokoa wanadamu, ila haohao wakamu sulubisha bila hatia.
 
Back
Top Bottom