OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Nimeangalia takwimu za Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya wenza duniani, Afrika ina rate kubwa ya mauaji kuliko mabara mengine. Kwanza tujue katika mauaji haya, wanawake ni waathirika wakubwa zaidi kuliko wanaume. Data zinaonesha wanawake wanaouawa ni mara mbili zaidi ya wanaume wanaouawa kwenye mapenzi.
Aidha rate ya mauaji kwa Afrika ni kubwa zaidi kuliko mabara mengine
Idadi kubwa ya mauaji inayotokea Afrika mimi inanifikirisha kwa namna kadhaa na kuona kuna haja ya kuangalia upya mahusiano ya kiuchumi kati ya mwanamke na mwanaume katika ndoa/mahusiano ya kimapenzi.
Nikiangalia kwenye data naona nchi ambazo zinausawa wa kijinsia mkubwa kwenye mahusiano ni nchi ambazo zina mauaji machache kuliko nchi zinazotaka mwanaume awe kila kitu. Afrika, mwanaume anatoa kila kitu kumtunza mkewe, hali ambayo inamfanya amshushe mwanamke kutoka kuwa mtu hadi kuwa kitu chake. Ni case kama hiyo kwa wanawake ambao huwahudumia wanaume kwa kila kitu hivyo mtu huwa kitu na sio mtu tena. Hali hii inaathiri sana inapotokea kuna tofauti kidogo kwenye mahusiano, hapo ndipo mtu huweza hata kufikia kuua.
Nadhani kwenye mahusiano kunapaswa kuwa na kutegemeana badala ya kutegemea. Nchi za Afrika mwanaume akiwa na mwanamke mwenye hela basi anategemea, mwanamke anaona kumtegemea mwanaume ni jambo la haki yake ya msingi. Na ukishamtegemea mtu lazima ukubali kuwa "Kitu" na sio "mtu" tena. Jambo hili sio jambo linalohitajika lakini ni jambo litakalookoa wengi kutoka kwenye vifo
Mathalani, ukisikia mtu kamsomesha mtu, kamjengea nyumba, kamnunulia gari, waafrika wengi, huwa wanaona ni halali mtu huyo kuuawa kisa amefanya kosa fulani au hataki kuendelea na mahusiano na mtu aliyemfanyia vitu hivyo. Hii justification inaonesha umuhimu wa mtu kuwa bora kiuchumi badala ya kuwa tegemezi, yaani mtu ambaye ana jenga kwa hela yake nk, akipata madhara watu hujiuliza imekuwaje ikiwa haumuhudumii mtu.
Nirudi kwenye mada kuu, mauaji ya wapenzi yanaweza kuzuiwa ikiwa kwanza tuta-define upya mahusiano ya kiuchumi. Usawa usiishie kwenye siasa, bali hadi kwenye ngazi ya familia ili kuhakikisha kwamba watu wanachangia vyema maendeleo ya familia badala ya kudhani kwamba mmoja inabidi atendewe kila kitu.
Natoa hoja
Inmate Killings | ||
Year | Male | Female |
2010 | 98 | 192 |
2011 | 85 | 166 |
2012 | 94 | 185 |
2013 | 94 | 184 |
2014 | 106 | 208 |
2015 | 112 | 218 |