Pre GE2025 Useful pointers to CHADEMA: Civil disobedience and passive resistance

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ushauri tu

Usibet kabisa kwa chadema…. Wana badilika mno kulingana na wallet

Unakumbuka 2015?
 
Ujinga ni mtaji wa wanasiasa Tanzania. Mtaji kwa watawala na hao wengine.

Tusingekuwa wajinga lowasa asingepewa kugombea urais chadema 2015, hakuwa na sifa za kuiwakilisha chadema.
Huwa nashangaa chadema kuona kwamba ujinga wa watanzania upo kwa wenye kushabikia ccm tu ila wao wana akili hawana ujinga wenye kutumika na viongozi wa chadema.

Hilo la Lowassa na Chadema ni mfano mzuri sana.
 
Ni bahati mbaya sana kwamba hayo uliyoyasema hakuna linalowezekana wanaloweza kujaribu ni kususia uchaguzi lakini napo hawatofanikiwa vyama vingine vitashiriki na italeta mtafaruku na hatimaye kukigawa chama maana kuna wapenda madaraka hawatakubali kususia uchaguzi
 
Naunga mkono hoja

Mm kitambo nimeshaanza kususia baazi ya huduma zinazotolewa na serikali piah zinapatikana kwa watoa huduma wa binafsi
 
Chini ya carpet, kugomea uchaguzi ni kuinua mapandikizi ndani ya chama kufanya Yao kama NCCR mageuzi.

Maandamano ndio njia sahihi kuhakikisha bila Tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya, haufanyiki uchaguzi wowote.

TABIA za kususa tuwaachie wamama!!
 
Chini ya carpet, kugomea uchaguzi ni kuinua mapandikizi ndani ya chama kufanya Yao kama NCCR mageuzi.

Maandamano ndio njia sahihi kuhakikisha bila Tume HURU ya UCHAGUZI na KATIBA mpya, haufanyiki uchaguzi wowote.

TABIA za kususa tuwaachie wamama!!
Tulio bongo tunajua… hayana impact
 
These useful pointers are still valid……
 
Anaetoa huu ushauri yupo marekani anakula maisha sasa wewe mtumishi wa umma jichanganye
 
Anaetoa huu ushauri yupo marekani anakula maisha sasa wewe mtumishi wa umma jichanganye
So just because the principal place of abode of the person that gave the pointers is the US, therefore, those pointers proffered are, ipso facto, invalid?
 
Tukianza na kugomea chaguzi zote, itakuwa ni mwanzo mzuri sana.
Kugomea chaguzi mnawapa mteremko, usifikiri na wao watasusa hivyo vyeo πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€. Dawa ni kupiga kura na kuzilinda. Mnyika alitoa ushauri mzuri sana,inabidi kuanza na uchaguzi huu wa serikali za mitaa ambapo kura zinahesabiwa hapo hapo kituoni!
 
CHADEMA watawahamasisha vipi/kwa njia zipi wananchi ambao nimateka wakuu wa CCM? Uchaguzi wowote ambao hata watu milioni moja wakijitokeza kupiga kura, huo tayari ni ushindi kwa CCM.

Ninacho kubaliana na wewe ni kwa CHADEMA kuelimisha na kufanya kazi na wananchi wawe tayari kujitokeza kwa wingi wao wote kwenda kupiga kura; na baada ya kupiga kura, wananchi hao hao wahakikishe kura zao hazitachezewa na mtu yeyote, awe polisi, msimamia uchaguzi au mwingine yeyote.
Wananchi kila kituo cha kupigia kura wahakikishe kura sahihi zilizo pigwa ndizo matokeo yake yanatangazwa.

Ni wananchi pekee wanaoweza kulitekeleza hili wakiwa wameandaliwa vizuri na kuwa na elimu ya kutosha.

Kuharibu kura za wananchi kunakofanywa na serikali na CCM huo ni uhalifu. Kwa hiyo wananchi wakiongozwa na CHADEMA wawe tayari kuzuia uhalifu huu kwa gharama yoyote.
 
Hujawahi kumsoma 'Kalamu' kuhusu hili?

Hata hivyo, CHADEMA wamechelewa sana kuwaendea wananchi na kuwaandaa kwa kazi hiyo muhimu.
 
Ccm imeshakuwa mhimili wa 4 wa nchi, tena wenye mamlaka kuliko mihimili yote.

Katiba mpya pekee ndiye itakayoweza kusawazisha hilo.
Taratibu mkuu 'Proved'. Hivi huoni ulivyo jichanganya hapo? Hiyo Katiba itapatikana vipi kama hali ni kama hiyo uliyo ielezea!
 
Chadema wakisikia Tu neno RUZUKU mate yanawajaa mdomoni....COVID19 wamewatoa kamasi..
Njaa ni mbaya Sana?
 
Hili la kugomea chaguzi Chadema wanaflip-flop tu, mara waseme kwa katiba hii hawatoshiriki chaguzi , mara wageuke kuwa watashiriki hivyohivyo. Kiufupi maslahi binafsi yanawekwa mbele ya masilahi mapana ya nchi
 
Hili la kugomea chaguzi Chadema wanaflip-flop tu, mara waseme kwa katiba hii hawatoshiriki chaguzi , mara wageuke kuwa watashiriki hivyohivyo. Kiufupi maslahi binafsi yanawekwa mbele ya masilahi mapana ya nchi
Hapo ndo CHADEMA waliponipoteza kabisa.

Dawa migomo tu!

Wananchi wakigoma hata kwa siku tatu tu, CCM itanyooka na katiba mpya itapatikana.
 
Namba 2 na 3 tayari , wengine unaowaona ni Chawa au wale watu wa misiba wanaojiita Mama ongea na Mwanao
Huyo anaweza kuwa na mawazo ya namna hiyo akidhani anasaidia chochote, lakini sioni katika andiko lake lolote la maana sana mbali ya kusaidia tu hao wananchi kuhusu hizo namba 2 na tatu.

Ushauri wa "KUSUSIA UCHAGUZI", bila ya kuwa njia nyingine mbadala ya kuwaondoa CCM madarakani ni wenda wazimu ule ule wa siku zote.

CHADEMA walitakiwa wakati huu, Septemba 13, 2024 wawe wamefanya kazi kubwa zaidi na wananchi katika maandalizi ya chaguzi zinazofuata. Wananchi wawe tayari wanayo elimu ya kutosha, na wawe wanaielewa barabara mikakati ya kuhakikisha kura zao haziharibiwi kwa njia yoyote ile. Haya tulianza kuya shauri tokea miaka mitano iliyo pita.
 
Hili la kugomea chaguzi Chadema wanaflip-flop tu, mara waseme kwa katiba hii hawatoshiriki chaguzi , mara wageuke kuwa watashiriki hivyohivyo. Kiufupi maslahi binafsi yanawekwa mbele ya masilahi mapana ya nchi
Kwa hali ilivyo nchini kwa sasa hivi; CHADEMA wakidhamiria kufanya kazi na wananchi wenyewe kuhakikisha uhalifu unaofanywa na serikali na CCM nyakati za uchaguzi hautavumiliwa tena, ninaamini uchaguzi utafanyika na matokeo sahihi ya uchaguzi huo yatappatikana.

Kinacho takiwa sasa ni CHADEMA na wengine wote wanaoitakia mema nchi hii ni kuwaelimisha wananchi kuhusu 'sanctity' ya kurav zao; na kubuni mikakati sahihi ya kuhakikisha hali hiyo inakuwepo wakati wa uchaguzi.

CHADEMA walivurugwa hapo wakati wa "mazungumzo ya Maridhiano". Sasa wame tambua ulaghai ulio waingiza mkenge. Ni vyema basi, wajisahihishe na kuanza kazi ii ngumu mara moja bila kupoteza muda zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…