Sishangai na nakusamehe kwa kunipotezea muda wangu ila kwa kuwa mimi ni mtu wa Mungu, watu kama nyie ni wa kuwasamehe tu. Nimekwambia usome hizo references, either umegoma au haujaelewa au hautaki kukubaliana na ulichokisoma. Mkifeli mnasema elimu ngumu.
CAF CUP pamoja na kwamba zawadi ya mshindi ilitolewa na Abiola yalibaki kuwa ni mashindano ya yaliyoendeshwa na CAF na yalifanyika kwa miaka 10 na mwaka 2004 mashindano hayo hayo yaliunganishwa na hayo mengine kutengeneza kombe la shirikisho. Hili nilishakwambia hapo juu lakini kwa kuwa kichwa chako chepesi bado unalileta.
Kuhusu timu zilizoshiriki baada ya hapo, kwa taarifa yako Yanga alishiriki mwaka uliofuata 1994 na kwa kuwa ni jadi yenu kutofanya vizuri mashindano ya kimataifa, mlitolewa round ya kwanza, imagine aibu hiyo!
Baada ya hapo walioshiriki Malindi 1995, Small Simba ya Zanzibar 1996, Simba 1997, Mlandege 1998, Yanga 1999 (mkatupwa tena round ya kwanza), Mtibwa 2000, 2001, 2002.
2004 ndiyo yakaunganishwa na kombe la washindi kutengeneza kombe la shirikisho.
Kukusaidia zaidi, vigezo vilikuwa timu oliyoshika nafasi ya pili katika ligi ya nchi yao, kwa hiyo vigogo wengi tu wameshiriki mashindano hayo.
Kwa lugha nyingine, mashindano hayo ambayo Simba alicheza fainali na kombe uwanjani, Yanga ameshiriki mara mbili na haijawahi kuvuka round ya kwanza.